vifaranga tunachoma moto, ng'ombe tunauza, kama hofu ni mafua ya ndege, Sotoka haiambukizi?

jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,558
25,322
Tumeshuhudia vifaranga kutoka kenya wakiteketezwa kwa kuchomwa moto kwa amri ya mamlaka za serikali ya tanzania!

Tumepewa sababu ikiwemo kuzuia uwezekano wa maambukizi ya magonjwa ya mifugo na ndege kuvuka mipaka ya nchi moja kwenda nchi nyingine, tukaambiwa na sheria ipo inayosimamia utaratibu huu.

Tunajiuliza kama kwa vifaranga tuliogopa mafua ya ndege n.k ilikuwaje tukasahau ugonjwa hatari sana wa SOTOKA na homa ya mapafu kwa ng'ombe?

Imekuwaje wenye mamlaka serikalini this time hawakusoma zile sheria na kanuni walizozisoma kwenye sakata la vifaranga wa kuku?

Je ni halali kwao kutuchagulia aina ya hatari inayopaswa kuingia nchini? Hawakupaswa kutuhakikishia usalama?
 
mambo ya kitaalami waachie wataalamilu sio kujifanya kila kitu unajua ..
fu...afu sana
 
Back
Top Bottom