Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,009
- 9,874
Katika msururu wa kuadhimisha Siku ya Uelewa kuhusu ugonjwa wa Kisukari tunakupatia vidokezo vya namna kukabiliana na ugonjwa huo na jinsi ya kuulinda na jamii nzima.
Idadi ya watu wenye kisukari duniani kote inakadiriwa kufikia milioni 422 lakini ukweli ni kwamba hata watoto wanaambukizwa.
Dkt. Sakariye Mohamud Mohamed anafafanua vyakula vinavyohitajika kwa mtu mwenye kisukari na jinsi anavyoweza kujikinga dhidi ya hatari ya ugonjwa huo.
"Vyakula muhimu zaidi ambavyo mtu mwenye kisukari anaweza kutumia ni pamoja na, kama vile ngano, maharagwe, dengu, mafuta ya ufuta na mafuta ya mizeituni."
Dkt Sakariye ambaye amekuwa akiwatibu wagonjwa wa kisukari kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita, anazungumzia vyakula bora na vibaya zaidi kwa mtu mwenye kisukari na baadhi ya mambo hatari ambayo watu hawayajui.
"Mambo mengine ambayo yanapendekezwa ni pamoja na kula nyama nyeupe, maji safi, na kuepuka bidhaa za wanyama."
Kwa hivyo ni vyakula gani ambavyo mtu mwenye kisukari hapaswi kula. "Vyakula ambavyo unapaswa kuepuka kila mara ni pamoja na vyakula vya makopo, ndizi, maembe, papai, tikiti maji, tende, asali na maji ya makopo yanayozalishwa viwandani," alisema Dk Sakariye Mohamud Mohamed.
Asali na tende zinasemekana kutothaminiwa na watu wenye kisukari, lakini ni vyakula hatari ambavyo havipaswi kuliwa na watu wenye kisukari.
"Kitu cha kawaida tunachokiona kwa wagonjwa ni tende na asali ambayo wanaamini ni ya asili na haimdhuru mtu. Asali na tende ni hatari zaidi kuliko vyakula vya kawaida."
Kula vyakula hivi ikiwa una kisukari
- Ngano
- Maharage
- Mafuta ya siki
- Mafuta ya mizeituni
- Nyama nyeupe
- Maji ya kawaida
Epuka vyakula hivi ikiwa una kisukari
- Vyakula vya makopo
- Ndizi
- Maembe
- Tikiti maji
- Tende
- Asali
- Maji ya makopo yanayozalishwa na viwanda