Vifahamu vyakula vya kuepuka kuvila ikiwa una kisukari

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,874
.

Katika msururu wa kuadhimisha Siku ya Uelewa kuhusu ugonjwa wa Kisukari tunakupatia vidokezo vya namna kukabiliana na ugonjwa huo na jinsi ya kuulinda na jamii nzima.
Idadi ya watu wenye kisukari duniani kote inakadiriwa kufikia milioni 422 lakini ukweli ni kwamba hata watoto wanaambukizwa.

Dkt. Sakariye Mohamud Mohamed anafafanua vyakula vinavyohitajika kwa mtu mwenye kisukari na jinsi anavyoweza kujikinga dhidi ya hatari ya ugonjwa huo.
"Vyakula muhimu zaidi ambavyo mtu mwenye kisukari anaweza kutumia ni pamoja na, kama vile ngano, maharagwe, dengu, mafuta ya ufuta na mafuta ya mizeituni."

Dkt Sakariye ambaye amekuwa akiwatibu wagonjwa wa kisukari kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita, anazungumzia vyakula bora na vibaya zaidi kwa mtu mwenye kisukari na baadhi ya mambo hatari ambayo watu hawayajui.

"Mambo mengine ambayo yanapendekezwa ni pamoja na kula nyama nyeupe, maji safi, na kuepuka bidhaa za wanyama."

Kwa hivyo ni vyakula gani ambavyo mtu mwenye kisukari hapaswi kula. "Vyakula ambavyo unapaswa kuepuka kila mara ni pamoja na vyakula vya makopo, ndizi, maembe, papai, tikiti maji, tende, asali na maji ya makopo yanayozalishwa viwandani," alisema Dk Sakariye Mohamud Mohamed.

Asali na tende zinasemekana kutothaminiwa na watu wenye kisukari, lakini ni vyakula hatari ambavyo havipaswi kuliwa na watu wenye kisukari.

"Kitu cha kawaida tunachokiona kwa wagonjwa ni tende na asali ambayo wanaamini ni ya asili na haimdhuru mtu. Asali na tende ni hatari zaidi kuliko vyakula vya kawaida."

.

Kula vyakula hivi ikiwa una kisukari​

  • Ngano
  • Maharage
  • Mafuta ya siki
  • Mafuta ya mizeituni
  • Nyama nyeupe
  • Maji ya kawaida

Epuka vyakula hivi ikiwa una kisukari​

  • Vyakula vya makopo
  • Ndizi
  • Maembe
  • Tikiti maji
  • Tende
  • Asali
  • Maji ya makopo yanayozalishwa na viwanda
BBC Swahili
 
Hivi mtu akinywa visoda,vi pipi n.k mara kwa mara ana risk ya kupata kisukari pia ?

MÊmENtO HoMO
 
Maji ya kwenye chupa yanasukari kutoka wapi? Hawa Waganga NJAA taabu kweli kweli hata yale ya ukweli yatakuja puuzwa kwa kuweka vitu vya ovyo.
 
.

Katika msururu wa kuadhimisha Siku ya Uelewa kuhusu ugonjwa wa Kisukari tunakupatia vidokezo vya namna kukabiliana na ugonjwa huo na jinsi ya kuulinda na jamii nzima.
Idadi ya watu wenye kisukari duniani kote inakadiriwa kufikia milioni 422 lakini ukweli ni kwamba hata watoto wanaambukizwa.

Dkt. Sakariye Mohamud Mohamed anafafanua vyakula vinavyohitajika kwa mtu mwenye kisukari na jinsi anavyoweza kujikinga dhidi ya hatari ya ugonjwa huo.
"Vyakula muhimu zaidi ambavyo mtu mwenye kisukari anaweza kutumia ni pamoja na, kama vile ngano, maharagwe, dengu, mafuta ya ufuta na mafuta ya mizeituni."

Dkt Sakariye ambaye amekuwa akiwatibu wagonjwa wa kisukari kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita, anazungumzia vyakula bora na vibaya zaidi kwa mtu mwenye kisukari na baadhi ya mambo hatari ambayo watu hawayajui.

"Mambo mengine ambayo yanapendekezwa ni pamoja na kula nyama nyeupe, maji safi, na kuepuka bidhaa za wanyama."

Kwa hivyo ni vyakula gani ambavyo mtu mwenye kisukari hapaswi kula. "Vyakula ambavyo unapaswa kuepuka kila mara ni pamoja na vyakula vya makopo, ndizi, maembe, papai, tikiti maji, tende, asali na maji ya makopo yanayozalishwa viwandani," alisema Dk Sakariye Mohamud Mohamed.

Asali na tende zinasemekana kutothaminiwa na watu wenye kisukari, lakini ni vyakula hatari ambavyo havipaswi kuliwa na watu wenye kisukari.

"Kitu cha kawaida tunachokiona kwa wagonjwa ni tende na asali ambayo wanaamini ni ya asili na haimdhuru mtu. Asali na tende ni hatari zaidi kuliko vyakula vya kawaida."

.

Kula vyakula hivi ikiwa una kisukari​

  • Ngano
  • Maharage
  • Mafuta ya siki
  • Mafuta ya mizeituni
  • Nyama nyeupe
  • Maji ya kawaida

Epuka vyakula hivi ikiwa una kisukari​

  • Vyakula vya makopo
  • Ndizi
  • Maembe
  • Tikiti maji
  • Tende
  • Asali
  • Maji ya makopo yanayozalishwa na viwanda
BBC Swahili
Kama taarifa hii imeandaliwa na BBC basi sio ya kuamini hata kidogo.
Mje na majibu kwa nini kisukari kinazidi kuongezeka sio kuwakataza watu kula vyakula bora.
Sasa mimi nakuja na majibu.

Kwanza ujue kisukari kinaanzia wapi!!
Kisukari kinaanza baada ya organ mwilini kuchoka kufanya kazi, Organi hiyo ni Ini na Kongosho. Naongea si kama daktari bali mtu wa kawaida mwenye uelewa.
Kazi ya ini ni kama Maabara/laboratory ya mwili.Dawa/kemikali za mwili zote hutengenezwa au kuchakatwa hapa, maana yake hata sense za kongosho kuwa insulin ambayo ni dawa ya kuondoa sukari hutoka hapa. Sasa kama ini limechoka nani kalichosha?
Kwa uelewa wangu ni hivi, kila siku watu wanakula kemikali kwenye vyakula na vinywaji.
Natoa mfano Soda zote na vinywaji vinavyotoka viwandani ni kemikali ambazo mwili unaona kama ni sumu na sumu hizo anazitoa Ini zikiwa nyingi jamaa ini anachoka kuzichakata zitoke na hivyo Kongosho hana uwezo wa kuzalisha insulin kwa sababu baba yake ini anaumwa na ugonjwa wake wanauiya Homa ya Ini kwa sababu ya kuchoka kutoa sumu.
Ulaji wa nyama ambao mtu hulenga kupata protini, tumefundishwa ujinga shuleni kuwa protini ni chakula bora. Kule Marekani RDA ( recommended daily allowance) ya protini ni gram 30 kwa siku, watu leo kutwa kuchwa kwenye milo yao wamejaza mayai, maziwa na nyama nyingi wengine hula hadi nusu kilo ya nyama kwa siku.
Nakuja kwenye point ya hiyo protini maana hamchelewi kusema kwa hiyo tusile nyama?
Mwili naturally hauhitaji protini nyingi (only below 30grms) kwa mtu mzima protini ni kwa ajili ya ukuaji wa nywele, kucha, na homoni kama shahawa nk.
Na hakuna hifadhi (storage) ya protini mwilini na kama kinahifadhiwa ni "negligible" sasa umekula nyama nusu kilo au umeagiza chips na nusu kuku, au nasema uongo ndugu zangu?
Huo mzigo wote unatokaje ndani ya mwili maana ukienda chooni unakunya mavi sio hiyo nyama? Maana yake Ini ndo huichakata hiyo nyama na kuitoa mwilini kama Amino acid kisha Urea mtu anakojoa., ndo maana kuna connection ya kuongezeka kwa ugonjwa wa kisukari , homa ya ini pamoja na ugonjwa wa figo na moyo.chanzo ni ulaji. Umekula nyama pamoja na majuice ya viwandani ambayo yamewekwa additives na food colours vyote hivyo ni kemikali sumu kwa mwili.
Bado watu wanongezea ladha kwenye vyakula kama ndimu ya mchina ni kemikali, bado nyama zinawekewa ajinamoto ambayo pia sumu ili kuilainisha, bado sukari inayotumika kwenye cake na ice cream ambayo sio hii ya miwa bali ni "aspartame" na hii aspartame wauza Ice cream na wenye viwanda kama Azam na Mo (mnisamehe Mods kwa kuwataja hawa) na wengineo kama hao wanawa target watoto kwa Icecream zao ambazo zinawekwa sukari ile kali, lakini cheap , hii kibiashara inalipa.
Nimechoka kuandika mtanisamehe, lakini hata siku moja hospitali hazisemi sababu za kujikinga na kisukari kwa sababu, it is a multibilions bussiness.
Na tiba yake ni kinyume na nilichosema.
Acha kutumia then rudi kwenye nature utapona bila gharama kubwa ya pesa.
Asikudanganye mtu njoo Pm nina dawa, hao wote wanataka kutajirika kwa mateso ya ugonjwa ya watu wengine.
Saidieni watu elimu wapone magonjwa, na herbs ndo solution.
 
Sijawahi sikia kuwa kuna dawa ya kisukari na endapo itapatikana basi duniani huyo mtu atakuwa ni tajiri wa kutupa. Sema lazima auawe maana anaweza haribu biashara nyingi Sana kwani atazitaja zote na hizo business zinalipa Sana na kodi zinatoa Sana.
Nafikiri hapo ishu kubwa ni tahadhari ya vyakula na kurudi katika asili yetu. Nchi za kiafrika Mungu amezipa kila kitu sema uzungu na maisha yetu ya mababu zetu tumedharau hasa sisi tunaoishi mjini
 
Wanao Ishi na kisukari acha kula matunda yoote yakiwa mabichi huwa na Rangi ya kijani na yanapo komaa hubadilika rangi na kuwa na Rangi ama nyekundu,njano au pink
 
Back
Top Bottom