Vifahamu vifurushi vingine nje ya vipya vya sasa

Besta Mlagila

Senior Member
May 29, 2018
101
191
Kumekuwa na upotoshaji unaoenezwa na baadhi ya wanasiasa kuwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) unafanya suala la Afya kuwa biashara baada ya kuanzisha vifurushi vipya vyenye makundi ya ulipaji kulingana na uhitaji na hali ya mwananchi.

Tukiacha vifurushi vipya vilivyo anzishwa hivi karibuni vipi vifurushi vingine kama ifuatavyo:

BIMA KWA TAASISI ZA UMMA
  • Taasisi hizo ni kama Wizara, Idara za Serikali zinazojitegemea, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Mawakala wa Serikali, Taasisi za Serikali zinazojitegemea.
  • Ambapo mwajiri atalipa 3% na Serikali 3%
BIMA KWA WASTAAFU
Bima hii baada ya kustaafu mwanachama hatachangia tena na atatibiwa bure yeye na mke wake pekee mpaka watakapoaga dunia.

WAFANYAKAZI WA MADHEHEBU YA KIDINI
Mashirika au Taasisi za kidini, kiongozi au mtumishi wa dhehebu hilo, pamoja na sheikh, maimamu, maaskofu, mapadri na vikundi vingine vyote ambavyo hufanya shughuli zinazofanana kulingana na sheria za nchi.

TOTO AFYA KADI
Ni kadi ya Bima ya Afya ya NHIF inayotolewa kwa watoto wa chini ya miaka 18 wanaosajiliwa na NHIF ili kuwawezesha kupata huduma za matibabu katika vituo vilivyosajiliwa na NHIF nchi nzima.

Madhumuni ya kuanzisha Toto Afya Kadi:
  • Kuwapa fursa kwa wazazi/walezi ambao ni wanachama wa Mfuko kusajili watoto ambao hawakuweza kusajiliwa kwa sababu nafasi za wategemezi za mwanachama zimejaa, kwa mfano mwanachama ana watoto 6 lakini nafasi za wategemezi zilizopo ni 4 tu.
  • Kutoa nafasi kwa watoto ambao hawanauhusiano wa damu na mwanachama mchangiaji kujisajili na kupata huduma kwa kulipiwa na mzazi au mlezi mfano, mtoto wa shangazi n.kKutoa fursa kwa wafadhili au wahisani kuwalipia gharama za usajili watoto walio kwenye mazingira magumu na vituo vya kulelea watoto yatima
BIMA KWA WANAFUNZI
  • NHIF inatoa huduma za Bima ya Afya kwa wanafunzi wa Taasisi za elimu ya Juu au taasisi yoyote ya kujifunza kwa kipindi ambacho atakuwa amesajiliwa kama mwanafunzi.
  • Kwa taasisi ambazo hazijasajiliwa na Mfuko, wanafunzi wanaweza kuomba uanachama katika vikundi vya wanafunzi wasiopungua 50.
  • Mchango kwa kila mwanafunzi ni TZS 50,400/=
BIMA YA AFYA KWA VIKUNDI (KIKOA)
  • NHIF inatoa fursa kwa vikundi vya wafanyabiashara binafsi katika sekta mbali mbali za uchumi kujiandikisha washiriki wa vikundi na wategemezi wao.
  • KIKOA ni mpango wa bima ya afya kwa vikundi kwenye sekta isiyo rasmi katika vikundi maalum vya wajasiriamali waliosajiliwa kama dereva boda boda, mama/baba lishe au kikundi chochote cha ujasiriamali chenye wanachama kisichozidi 10.
  • Wanachama watachangia TZS 76,800 kwa kila mtu kila mwaka na hupewa vitambulisho vya uanachama wa NHIF vitumike kwa matibabu ya mwaka mmoja.
BIMA YA AFYA KWA BINAFSI
  • Mwanachama binafsi atapata fursa ya kuwa na wategemezi kama ilivyo kwa mwanachama aliyeajiriwa. Wategemezi wanaokubalika ni wale tu wanaotambulika chini ya utaratibu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya. Wategemezi hawa ni pamoja na mwenzi wa mchangiaji, (mke au mume), watoto wa kuzaa au kuasili chini ya miaka 18 au wazazi wa mwanachama mchangiaji na wa mwenza wake.
  • Mwanachama binafsi atachangia kiwango cha TZS 1,501,200 kwa mkupuo mmoja kila mwaka kabla ya kuanza kupata huduma.
 
Back
Top Bottom