designer spenko
Member
- Jun 8, 2011
- 76
- 10
mm personal ni architect kwenye nondo n kokoto kuna vitu vingi vya kuzingatia !!be carefull,
RMshauri, Nabaki Africa nimepachungulia juu juu tuu juzi. Kuna hadisi nasikia watu wanasema kwa nyumba ya 150SQM inaweza kula Million 20-30 jee hii habari ni kweli kaka? Kama kweli sasa itabidi tupige bati la south lol. Maana hapo sijaongea na madirisha, tiles chini na makolokolo mengine.
Mkuu thread ni long tyme. Hem niambie kwa sasa kagorofa kamoja kujenga inaweza ikala shs ngapi kila kitu roughly.Wakuu kwa wale wenye uzoefu katika shughuli za ujenzi hebu tusaidiane hapa. Nahitaji kujua wapi naweza kununua nondo imara kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya ghorofa moja na bei yake ikoje kwa tani (eg za mm 8, 12 na 16). Je kweli kokoto nyeupe za mawe hazifai mpaka zile nyeusi tu za Lugoba na Msolwa? Je naweza kupata wapi tofali imara za concreate au vibrated? Bei zake zikoje?
Natanguliza shukrani zangu wakuu.
Mkuu hiyo 150 sqm una maanisha saizi ya paa au? Kama ni paa si kweli maana paa langu lilikuwa ni sqm 354 na limekula Tshs. 27.3 mil. Hii ni gharama ya material yote yaliyotumika kwenye paa zikiwemo mbao na gharama za ufundi.
Mkuu thread ni long tyme. Hem niambie kwa sasa kagorofa kamoja kujenga inaweza ikala shs ngapi kila kitu roughly.
Mkuu nilitaka kushangaa, basi nimeshatoa hofu sababu najua kwa M20 naweza maliza kazi yote na chenji ikabaki. Basi tuombe Mungu plan inaanza January Mungu akijalia.
Naulizia bei ya nondo za mm 16 kwa bei ya rejareja
Asante dada Belinda. Hizo nondo ulishawahi kuzitumia na ukajua ubora wake? Maana naambiwa kuna nondo zingine zinazotengenezwa TZ zinavunjika kama kuni. Hivi kuna watu wanao-import nondo kutoka nje zenye ubora zaidi?
Na mimi kidogo nina kaproject kama kako, hila kama wenzangu walivyo zungumza humu nondo zinauzwa kwa tani bila kujali size yake, na nondo nyigi nzuri zinatoka nje hasa Uturuki, Malyasia, Africa Kusini hakuna nondo zinazo toka Urusi wale warusi pale TABATA nondo wanazo huza zinatoka Uturuki na bei zake kwa tani na kama walivyo quote wenzangu, hila mimi nilkuwa nataka kukupa ushauri kwamba kwa unafuu wa bei kanunue nondo katika kiwanda cha wahindi opposite na Kioo limited, nondo zao zinatengenezwa kutokana na billets kutoka nje kwa hiyo ni za kiwango cha hali ya juu sana na demand yake hapa nchini ni kubwa kwa sasa hivi wamesimamisha kidogo kutokana na kusubili mali ghafi kutoka nje.
Kuhusu kokoto mimi natumia kokote ngumu kama mawe na siyo ubuyu, au za kutoka msolwa au nini. Hizi za msolwa packing density yake ni kubwa sana na sidhani unahitaji kitu kama hicho kwenye ujenzi wako, nyenzo nyingine za ujenzi zinapatikana kirahisi tu.
Hahaha,mihela yote hiyo kha.Ni bilioni 1.5 mkuu. Vipi umezichanga za kutosha?
Hahaha,mihela yote hiyo kha.
Mie nilidhani ni around 300m.
Mkuu ntakutafuta.Mkuu ukiwa na 300M unajenga mjengo wa maana sana tu pengine wenye mvuto kuliko hata huo wa mchungaji. Hapa kuna mambo mengi ya kuangalia. Je kiwanja chako ni tambarare na hakiko kwenye udongo wa mfinyanzi? kama jibu ni ndiyo ina maana utatumia pesa kidogo kujenga msingi ambao ndo hula pesa nyingi sana kwa ghorofa. je umetumia kampuni kujenga? Gharama za ujenzi hapa ni kubwa ukilinganisha na aliyetumia mafundi wa kawaida. Pia usimamizi wako wa karibu ni muhimu kuhakikisha kuwa pesa zako zinatumika ipasavyo na si kuishia mifukoni mwa watu.