Vifaa vya Sh 95.8 milioni vyayeyuka MUWSA

mwanaizaya

Senior Member
Apr 26, 2008
133
1
Vifaa vya Sh 95.8 milioni vyayeyuka MUWSA
Na Mwandishi Wetu


VITENDO vya wizi na ubadhirifu wa mali ya umma vinazidi kuitikisa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Mjini Moshi (MUWSA) baada ya Tume Maalumu kubaini upotevu wa vifaa vyenye thamani ya Sh 95.8 milioni.


Kubainika kwa wizi huo katika bohari ya MUWSA kumekuja wakati Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ikiendelea kuchunguza vitendo vya ufisadi ndani ya mamlaka hiyo.


Taarifa ya Tume hiyo, ambayo Mwananchi inayo nakala yake, inaonyesha kuwa wizi huo ni katika kipindi cha miezi 11 tu hadi kufikia Juni mwaka huu na imebainisha kuwa huenda miezi ya nyuma kukawa na wizi zaidi. Tume hiyo iliyokuwa na wajumbe wanne, iliundwa kutokana na agizo la Bodi ya Wakurugenzi wa MUWSA iliyokutana Juni 9, mwaka huu.


Agizo hilo lilitokana na taarifa za kuibwa kwa vifaa 1,841 vinavyojulikana kama Get Valves, vyenye thamani ya Sh 16.5 milioni uliotokea Aprili 22, mwaka huu na taarifa hizo kuripotiwa kwa mara ya kwanza na gazeti hili.


Hata hivyo, katika uchunguzi, tume hiyo ilibaini madudu zaidi ambapo vifaa hivyo vilivyoibwa vilifikia 1,890 vikiwa na thamani ya Sh17,955,000 na kugundua pia upotevu wa vifaa vingine vyenye thamani ya Sh77,880,702.


Vifaa hivyo ni Connector na Bib Cock ambavyo ndivyo vinavyotumika kuunganishia wateja huduma ya majisafi na kwamba wizi huo umetokana na uzembe wa baadhi ya watumishi.


�Ni dhahiri vifaa tajwa viliibwa kutokana na uzembe au ushiriki wa watumishi," imesema sehemu ya taarifa hiyo. Taarifa hiyo imeongeza kueleza kuwa vifaa hivyo vimepotea au kuibwa stoo pasipo kuvunjwa na huenda vilivushwa kidogo kidogo au kwa wingi na kwa vyovyote vifaa hivyo vilipitishwa getini.


Tume imependekeza kurejeshwa kazini kwa watumishi watatu, Jane Koromia, Rose Uisso na Aggrey Makia baada ya kutobaini dalili zozote za ubadhirifu dhidi ya wafanyakazi hao ambao walisimamishwa kazi.


Pia tume hiyo imependekeza kurejeshwa kazini kwa mafundi wawili, Emanuel Mlay na Anthony Mathias kwani hakuna ushahidi kuwa walishiriki katika wizi uliotokea Aprili 22 kwani walikuwa kihalali kazini.


Kampuni binafsi ya ulinzi ya Supreme International ambayo imepewa dhamana ya ulinzi na usalama MUWSA imetakiwa kulipa fidia kwa vifaa vilivyoibwa Aprili 22 kwa kuwa wizi huo ulitokana na uzembe wao.


Tume hiyo imeshauri menejimenti ya MUWSA kutotumia mfumo wa Tally katika kitengo cha Manunuzi na Ugavi kwa kuwa mfumo huo unaruhusu salio hasi na pia inakubali mwingiliano wa takwimu za miezi iliyopita.


Taarifa ya Tume ilijadiliwa katika kikao cha Ajira na Nidhamu cha wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi kilichofanyika wiki iliyopita na kuagiza Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Mahesabu (CAG) afanye ukaguzi wa kina MUWSA.
 
Back
Top Bottom