Vifaa gani vinahitajika kutengeneza home studio?

sauti

Member
Nov 2, 2010
13
0
wana jf,
ningependa kujua vifaa muhimu, hardware na software, kwa ajili ya kutengeneza home music studio na Gharama za vifaa hivyo.
 
Kama hufahamu ni vifaa gani, basi hufai kuwa producer.

Hizo hela zitumie kwa biashara nyingine maana hii imeshakushinda hata kabla hujaanza.

Kuna vyombo vya aina nyingi sana na vingine kama vya akina The Rolling Stones, EMI, SONY nk ni bei mbaya.

Kila la kheri. Usikate tamaa kwa maneno yangu. Ila ni vema nikikupa onyo mapema.
 
Last edited by a moderator:
Labda alikua anataka ku-establish yake ya entertainment na si ya biashara au u-pryodyuza
 
Mimi si prodyuza, lakini ninapenda sana mziki, na kujifunza kuproduce. Si kwa ajili ya biashara, nimesha anza kujifunza fruity loops 8.0, na nataka nianze kujifunza kinanda.
 
Nunua kwanza hicho kinanda na mashine ya Sampler. Pia nunua Computer yenye Sound Cad nzuri na hiyo program yako uwe unarekodi hizo sampler zako kutoka kwenye kinanda na Sampler mashine na baadaye zote unaziunga kwenye hiyo program yako na kuwa na mziki tayari. Utakavyokuwa ukiendelea, ndiyo utaanza kuona umuhimu wa kuwa na aina nyingine ya mashine. Hapo utakuwa na uhakika, mashine gani hasa unahitaji na siyo kuruka na kusema nataka vyombo vya Studio.

Njia nzuri sana ambayo hata Producer kama Larock walifanya ni kufanya kazi Studio na huko unapata shule moja nzuri sana. Unaweza kuwa unafanya hata BURE. Unamwambia jamaa akuonyeshe na unakuwa ukifanya kazi zake kidogokidogo. Hatakuonyesha vyote ila siku zinavyokwenda, mengine utajisomea mwenyewe maana ngumu siku zote ni kuanza.

Kila la kheri katika safari yako.
 
shukrani sana!
 
Back
Top Bottom