Vifaa gani natakiwa kuwa navyo ili kuwa mpiga picha

stacygab

Member
Jan 12, 2019
16
4
Msaada tutani,

Napenda kazi ya kupiga picha. Je, ni vifaa gani muhimu natakiwa kuwa navyo kwa kuanza?

Je, nitumie camera aina gani yenye specification zipi ili niweze pata picha nzuri, nimeshawahi fanya kazi hii nilipokua shule nilitumia digital camera (sony)..

Kwasasa nataka niboreshe zaidi. Kuna maslahi kwenye hii kazi. msaada wenu tafadhali
 
Unatakiwa uwe na camera aina ya Nikon au Canon camera,kama utakuwa na kijiwe kwa maana ya ofisi basi uwe na printer pia aina ya Epson pia reflectors kwa ajili ya indoor na outdoor photoshoot.

Ila kwa kuanza ni camera tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuleta ushindani kwenye soko kwa hiyo sekta ilipofikia saa hizi hapa Bongo, inabidi ujipange sana kuanzia vifaa, utaalamu na kujitangaza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
jiulize wewe, unataka kuwa mpiga picha wa level zipi, ndio utajua uwe na nini.

Kuna mwingine camera tu inamtosha.
Mwingine anataka awena printer yake ili mambo yawe fasta fasta, mwingine anaona awe na studio ya kuvutia, mwingine anataka awe videographer kabisa.

Sasa, wewe unataka kuwa wa aina gani?

Je, kama wale wanaoshinda flyover wanasubiri wapita njia walioenda kushangaa daraja?

Je, wa kualikwa kwenye events kama harusi na shehere nyingine?

Nk

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msaada tutani,

Napenda kazi ya kupiga picha. Je, ni vifaa gani muhimu natakiwa kuwa navyo kwa kuanza?

Je, nitumie camera aina gani yenye specification zipi ili niweze pata picha nzuri, nimeshawahi fanya kazi hii nilipokua shule nilitumia digital camera (sony)..

Kwasasa nataka niboreshe zaidi. Kuna maslahi kwenye hii kazi. msaada wenu tafadhali
Fimbo tu.

Kila picha unayo kutana nayo we piga tu.
 
Back
Top Bottom