mo effect
JF-Expert Member
- Aug 27, 2014
- 567
- 637
nyuma ya pazia,
kumekuwa na maswali mengi ujio wa rais wa vietnam Tanzania, Vietnam ni moja ya nchi zilizokuwa na uchumi mdogo sana sawa na Tanzania lakini kwa sasa huwezi kuzilinganisha kabisa iko level nyingine hii imetokana na nchi hiyo kuwekeza kwenye nyanja mbalimbali za kimaendeleo kwenye nchi mbalimbali za Africa kama kitega uchumi.
Ujio wa rais wa Vietnam umetokana na kuja kuimarisha au kuweka wazi mikataba iliyokuwa na utata kidogo mfano kampuni ya mawasiliano ya Halotel iliyoanzishwa rasmi kisheria mwaka jana mwezi wa sita
Halotel ni kampuni ya mawasiliano ya Vietnam inayomilikiwa na serikali ya Vietnam ikijulikana kama Viettel na inaendeshwa na jeshi la Vietnam na hao hao wanaendesha makampuni yote yaliyoko Africa chini ya kampuni la Vietel Group
Viettel Group imezaa makampuni mengine ya mawasiliano kama Lumitel, Movitel, Nextel na Halotel ambayo yapo Mozambique, Burundi, Cameroon na Tanzania.
Serikali ya Vietnam ilianza kuwekeza Tanzania mwaka 2011 baada ya rais Kikwete kuitembelea nchi hiyo kama kawaida yake kuomba msaada kwa serikali ya Vietnam kuipiga kampani Tanzania kidogo kiuchumi. Makubaliano ya Tanzania chini ya utawala wa Kikwete ilikuwa kusambaza Halotel mikoa yote Tanzania hasa vijijini na kuweka cable za internet kwa kujitegemea (optic fiber cables) kwaakuwa jeshi hilo la Vietnam cable hizo kwa namna fulani kuimarisha ulinzi wa nchi yao pia ndio waendeshaji wakuu wa Viettel Group kupitia wizara ya ulinzi.
Viettel (Halotel) walijaribu kuingia mkataba na shirika la umeme Tanzania (TANESCO) kutumia minara ya umeme ya Tanesco kuwa kama antennas kama walivyokubaliana hapo mwanzo lakini baadae Tanesco wakatia ngumu na kuwapandishia bei na ikawa vigumu kwa serikali ya Pombe tofauti ilivyokuwa vyepesi kwaserikali ya Kikwete. Kwakuwa rais J. Pombe kutoelewa vizuri mkataba huo wa Halotel na mikakati yao ya kuanzisha V-money kama mfumo wa kubadilishia pesa kama ilivyo m-pesa, hivyo rais wa Vietnam akaamua kuja kuweka sawa na kufanya mazungumzo na J.Pombe pia kuangalia fursa nyingine zaidi kwa serikali hiyo ya Vietnam kuwekeza Tanzania.
powered by Mohagachi