Vidonda vinamyima raha hata ya mapenzi

Emasa

Member
Nov 14, 2008
38
2
Ndugu wana JF nina jamaa yangu anahitaji msaada wa haraka.

Huyu jamaa ana girlfriend wake wa muda mrefu sasa na ameamua angependa waoane lakini tatizo ni kuwa jamaa ana vidonda kwenye sehemu ya haja kubwa anasema ilianza kuwashwa miaka kama mitatu ilopita na alimueleza huyo mpenzi wake.

Yule mpenzi wake akamshauri kuwa anajisafisha vizuri kitu ambacho jamaa anasema hufanya tena kwa kumaanisha, ameendelea kuwashwa na akawa anakosa raha maana kila wakati anatia vidole huko kujikuna, yule mpenzi wake akamshauri waende kucheki magonjwa ya zinaa ambapo jamaa alikubali na wakaenda kupima maana hali ilikua inazidi kuwa mbaya na hasa pale ambapo anakuwa ana discharge.

Walipima pamoja (magonjwa yote ikiwemo Ngoma) na kukuta kuwa wako salama.

Ameshakwenda kwa madaktari kadhaa wanaishia kumchungulia na kutomsaidia anasema manake anapewa dawa ambazo hazijampa relief mpaka sasa anawashwa na anasema kumekua na vidonda na pia anadischarge mara kadhaa na wakati mwingine hushindwa kuenjoy na mpenzi wake sababu anakua anajihisi ana haruf mbaya inayotokana na matatizo hayo ikiwemo kudischarge.

Anahitaji msaada wenu waheshimiwa Afanye nini? maana mwishowe anahisi atampoteza hata mpenzi wake kutokana na kutopendelea kuwa nae kimapenzi mara kwa mara na akihofia kumkera huyo mrembo wake kutokana na hali inayomkuta.
 
aache kujishika na vidole huko awe anatumia toilet paper au kitambaa kisafi , ukishika utumbo wako na vidolelazima utapata infection na awe anakula mchicha , bamia , mapapai maparachichi ili awe anapata choo laini . kama unaweza ni pm maana siwezi kutumia lugha kali naogopa kufungiwa.
 
mi naona aende kwa kakobe!

Nadhani ushauri huo ni mzuri ila hilo naona ni swala la kiimani zaidi ambalo sijui msimamo wake wa kuamini juu ya hilo japo nadhani ushauri wa kitabibu ungemsaidia zaidi pia.
 
dah,mpe pole sana!
ila nadhani maombi ni daktari wa kwanza!
Na zaidi aende kwenye hospital kubwa maana anaweza kuwa kaenda hosp ndogo ambazo vipimo ni vidogo na haviwezi kuonesha tatizo hata kama lipo kweli!

Kwa mara mshauri aende bunda ddh,ingawa sidhani kama kuna vipimo vikubwa ingawa ndio hosp ya maana mara!
Au anaweza kwenda bugando mwanza,nk atapata tatizo lake na itakuwa rahisi kili fight
 
mi naona aende kwa kakobe!

Tatizo sio kwenda kwa mchungaji au askofu gani,kinacho takiwa ni imani tu,na ukiita jina la Yesu utapona!
Hizi imani tunazo weka kwa watu sio nzuri hata kidogo.
 
Naona aende hospitali yoyote kubwa aombe kuonana na Daktari specialist anayehusika na tatizo lake anaweza kupata ufumbuzi. Mfano mimi niliwahi kupata kikohozi mzee kilinitesa sana, siku moja nilibanja kwenye ndege mpaka abiria mwenzangu alinihama, mke wangu hata mi mi mwenyewe nilifikiri nimepata TB lakini nilipokwenda kumuona daktari bingwa wa ENT (ear nose and throat) Agha Khan Hospital aliniambia ni tatizo la kawaida tu ila nilikuwa sijapata tiba sahihi, alinipa dozi ya wiki mbili tu nikapona. Namshauri ndugu yangu aende hospitali kubwa aone specialist atapona.
 
mwambie atumie dawa hizi PREPARATION H ( Zipo za kuingiza na za kupaka) zipo na nyingine Ointiment nazo za aina mbili
 
mwambie atumie dawa hizi PREPARATION H ( Zipo za kuingiza na za kupaka) zipo na nyingine Ointiment nazo za aina mbili

mmmmmh,we hata kama ni dawa nzuri lazima apime kwanza na iwe recommended na daktari sio kila dawa uingize utapata "the fistula style"
Nenda hosp,..
 
Acheni kujificha nyuma ya wenzenu. Matatizo yako unampandikizia mwingine.
Mkuu hili jibu linahusika na ugonjwa? hata ikiwa tatizo ni la nani nadhani swal ani ushauri juu ya ugonjwa hata ingekua nani bado jina liko kwenye nickname so nadhani ulichokisema hapa kwangu mimi hakina maana....samahani kama hutopenda nilichosema.
kama una ushauri wa maana utafanyiwa kazi.
 
MMMMHHHH nimependa sana comment za JF ukiacha comment moja ya kimajungu!!! tuendelee kuwasaidia wenzetu leo kwao kesho kwetu!! have a blessed day
 
Pia mwambie awe anatumia detol kile nusu kifuniko anachanganya na maji ya uvugu uvugu halafu anakalia kwa muda wa dakika 5 mara 2 au 3 kwa siku. hata akiedna haja akijisafisha atumie maji uvugu vugu yaliyochanganywa na detol huku akitumia na hizo dawa nilizotaja hapo juu. wakati mwingine inakuwa ngumu kupatikana ila kwa Dar naweza kukuelekeza wapi zinapatikana
 
Pole sana wewe unayesumbuliwa n huo ugonjwa. Mi naona ungemuona jamaa mmoja anayetwaDr. Isaac Ndodi, ni bingwa wa kutumia daw za asili kama matunda na mbogamboga. Amewasaidia wengi sana na huwa anakuja Mwanza. Unaweza kuwapigia Startv wakakuelekeza vizuri ratiba yake. Naamini ukimuona ukiwa na imani utapona kabisa maana ameshawatibu wengi wenye matatizo kaa yako.
 
atafute doctor specialist.but pia anaweza kusearch solution kupitia google.anaweza kupata overview ya tatizo lake na kwa nini mpaka hivyoo.not all doctors bongo ni professional.wengine ndo hivyooo mtaani tu.
 
Ndugu wana JF nina jamaa yangu anahitaji msaada wa haraka, Huyu jamaa ana girlfriend wake wa muda mrefu sasa na ameamua angependa waoane lakini tatizo ni kuwa jamaa ana vidonda kwenye sehemu ya haja kubwa anasema ilianza kuwashwa miaka kama mitatu ilopita na alimueleza huyo mpenzi wake,yule mpenzi wake akamshauri kuwa anajisafisha vizuri kitu ambacho jamaa anasema hufanya tena kwa kumaanisha, ameendelea kuwashwa na akawa anakosa raha maana kila wakati anatia vidole huko kujikuna, yule mpenzi wake akamshauri waende kucheki magonjwa ya zinaa ambapo jamaa alikubali na wakaenda kupima maana hali ilikua inazidi kuwa mbaya na hasa pale ambapo anakuwa ana discharge,walipima pamoja (magonjwa yote ikiwemo Ngoma) na kukuta kuwa wako salama,
Ameshakwenda kwa madaktari kadhaa wanaishia kumchungulia na kutomsaidia anasema manake anapewa dawa ambazo hazijampa relief mpaka sasa anawashwa na anasema kumekua na vidonda na pia anadischarge mara kadhaa na wakati mwingine hushindwa kuenjoy na mpenzi wake sababu anakua anajihisi ana haruf mbaya inayotokana na matatizo hayo ikiwemo kudischarge.
Anahitaji msaada wenu waheshimiwa Afanye nini? maana mwishowe anahisi atampoteza hata mpenzi wake kutokana na kutopendelea kuwa nae kimapenzi mara kwa mara na akihofia kumkera huyo mrembo wake kutokana na hali inayomkuta.

Mpe pole huyo MjengaNchi,

Ingefahamika ni dishcharge ya aina gani ingekuwa rahisi ingekuwa rahisi ku narrow down possibilities.

Ushauri wangu:
.Kama ni blood discharge:
>>Ajaribu ku check digestive system diseases for possible portal-systemic anastomosis varicose(anal- rectal anastomisis varicose),hususwan chronic liver diseases.
>>Hemorrhoids.
>>A check pia possibility ya deep and superficial(hii angekuwa na michirizi ya mishipa ya damu iliyovimba na migumu miguuni,pia hupelekea bleeding and NOT just discharge) venous thrombosis....hii ni obstruction ya veins----------->venous congestion in the lower limbs-------> bleeding,pruritus (kuwasha),coldness,vulnerability to infection,ulcerations etc
.Kama discharge ni usaha:
>>Acheck possibility ya microbial infection,particularly Bacteria.Hii atahitaji kufanya Culture kujua ni aina gani ili ipatikane tiba muafaka.

.Afanye pia stool test,endoscopy(rectoscopy),biopsy etc ili kuangalia other alimentary canal disease including cancer

Otherwise namtakia afya njema

Peace

Qadhi
 
Tatizo sio kwenda kwa mchungaji au askofu gani,kinacho takiwa ni imani tu,na ukiita jina la Yesu utapona!
Hizi imani tunazo weka kwa watu sio nzuri hata kidogo.

Sidhani kama uko serious, yaani unamshauri asiende hospitali afanye maombi tu? No wonder tunazika kila siku!
 
aende aka-check digestion system, yawezekana akawa na stage za mwanzo za kansa ( saratini ya utumbo) asione aibu kwani mficha maradhi kifo kitamfichua.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom