Vidonda pembeni ya mdomo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vidonda pembeni ya mdomo

Discussion in 'JF Doctor' started by Mhafidhina, Feb 22, 2009.

 1. Mhafidhina

  Mhafidhina JF-Expert Member

  #1
  Feb 22, 2009
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Wanajamii naombeni msaada wenu...!

  Eti ni nini chanzo au kitu kinachosababisha mtu kutokwa na vidonda pembeni ya mdomo! KUna baadhi ya watu huwa wanasema inatokana na labda homa/maleria ndio inakua inatoka mwilini wengine wanahusisha vidonda hivyo na mambo ya zinaa pamoja na mambo mengine chungu nzima!

  Ninaombeni msaada wenu ili nipate kujua kwani kuna jamaa yangu vina mtokea mara kwa mara! So nikaona wacha nililete hapa hili suala ili nipate utaalamu wenu kuhuu chanzo cha hivo vidonda na tiba yake!
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Feb 22, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 68,290
  Likes Received: 22,960
  Trophy Points: 280
  Hiyo ni herpes...
   
 3. Mr Kiroboto

  Mr Kiroboto JF-Expert Member

  #3
  Feb 22, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 321
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  hivyo vidonda vipo pia katika sehemu zingine kama ulimi,midomo,ndani ya cheeks,na fizi?
   
 4. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #4
  Mar 1, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 4,868
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  This. There is also no cure. But you can reduce the symptoms, with some creams.
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Mar 1, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 55,727
  Likes Received: 20,438
  Trophy Points: 280
  Mwambie ale matunda na mboga za majani.
   
 6. Saikosisi

  Saikosisi JF-Expert Member

  #6
  Mar 1, 2009
  Joined: May 4, 2007
  Messages: 528
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Vidonda pembeni ya mdomo vyaweza kusababishwa na vitu vingi. Ili kujua nini chanzo specifically kwa huyo jamaa yako haina budi kukaa chini na mtaalam amweleze historia nzima (history taking), kisha mtaalam ataviangalia hivyo vidonda (physical exam) na pengine aweza hata kufanya baadhi ya vipimo (kama lab investigations) kujua chanzo.
  Wachangiaji waliotangulia wanaweza kuwa sahihi kuwa baadhi ya sababu za vidonda kama hivyo ni pamoja na virusi (eg. herpes simplex) na fungus (eg. candida - oral thrush). Lakini kuna vitu vingine chungu nzima kama upungufu wa madini mwilini (eg. iron) ama vitamin (eg. folic acid).
  Kwa vidonda vya herpes ni kwamba unakuwa na virusi vimekaa dormant mwilini, ukipata upungufu wa kinga mwilini (sio lazima HIV) hata kama ni kwa malaria ama stress vile virusi vinakuwa active na kusababisha vidonda hivyo- usually inapona vyenyewe mpaka upate stress tena.
  Nini cha kufanya; muone mtaalam wa afya akijua sababu atakutibu inavyotakiwa; ukila majani na matunda tu ama kutumia petrolleum jelly tu utakuwa hujitendei haki.

  Kila la kheir.
   
 7. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #7
  Mar 1, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 68,290
  Likes Received: 22,960
  Trophy Points: 280
  Heheheheee...najua vidonda ni profession yako....
   
Loading...