Vidokezo vitano vya kufuata ikiwa unaamua kutafuta mpenzi mtandaoni

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
FUIKV.png

Unapoanza kuwa na hisia na mtu, kumbuka kwamba ikiwa hamjawahi kuonana ana kwa ana, hisia hizo sio halali. Kwa kuwa akili yako haina habari na taswira halisi kuhusu mtu huyo, kama ambavyo ungekuwa kama mngeonana ana kwa ana.

Usijihusishe tu katika mahusiano ya kimtandao. Ni sawa kuanza kumjua mtu kupitia anachokiandika, lakini hatua hii haipaswi kuendelea kwa muda mrefu. Ili kuweza kumjua mtu vizuri ni vyema ukapanga kukutana naye mda mfupi baadaye.

Usijenge uhusiano na mtu anayeishi katika nchi tofauti. Kuwa na uhusiano na mtu ambaye yupo nchi nyingine na hakuna uwezekano wa kuwa pamoja ni kujitesa. Watu ambao hufanya hivi hushiriki katika mapenzi ya kufikiria.

Sahau juu ya watu ambao wameoa. Usikubali kuanzisha mahusiano na watu hawa hata wakisema uhusiano uko karibu kuisha. Watu wengi wamejiingiza katika udanganyifu wa aina hii. Ikiwa una uwezo wa kuanzisha uhusiano na watu ambao huna haja ya kusubiri watengane kwanini uhatarishe kwa kusubiri mahusiano mengine yaishe ndipo wewe uingie itakuwaje kama watarekebisha tofauti zao .

Kumbuka kwamba huwezi kujua ni mtu wa aina gani unazungumza naye. Mtu yeyote anaweza kuwa mkarimu, anayejali na makini kupitia skrini. Lakini nyuma ya skrini hiyo inaweza kumficha mtu aliye na matatizo mengi ambayo kimsingi unaweza kushindwa kuendana naye.
 
Sehemu rahisi ya kumjua mtu ni mtandaoni kuliko mtaani,hasa sehemu kama hii ambayo watu wanatumia fake names.

Kwa sababu mtu ambaye hajulikani na yeyote anakuwa huru kuongea atakavyo,kama hapa JF kuna watu wanajiachia na kuongea watakalo kwa sababu wako free,sasa unashindwaje kumjua mtu huyo tabia zake ?

Na mtu akiwa yuko huru ndo unajua tabia zake,hapa jf kuna uhuru mkubwa sabababu watu hawajuani hivyo tabia ya kila mtu utaijua kwa kuangalia kitu gani anacomment.

Mtaani unaweza kwenda lakini ukakuta mtu anajifanya sio muomgeaji wala mtukanaji kwa sababu anajua akitukana ataonekana na jamii.

Hivyo humu jamvini au mitandao mingine inaweza kuwa ni sehemu sahihi ya kupima watu ikiwa wewe mwenyewe utakuwa mhusika wa kumfuatilia mtu huyo.

Lakini pia huyo ambaye unataka kuanzisha nae mahusiano hakikisha hajui kama unamchunguza tabia,kwa sababu ukimchunguza mtu kisha akajua basi ataigiza ili tabia ambazo wewe unatarajia kuziona kwake ili apate ndoa tu.

Tulia,wasome watu
 
Mm nimeishia kusoma hapo hisia sio halali tu sijui ntakua na shida gani

Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom