Video ya Ngono ya Walimu Uingereza Yawaletea Balaa

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,138
Video ya Ngono ya Walimu Uingereza Yawaletea Balaa
2100558.jpg

Walimu wawili nchini Uingereza wako kwenye hatari ya kupoteza kazi zao baada ya video yao waliyoitengeneza wakati wakiepeana uroda nyumbani kwao kuonekana kwenye mitandao ya ngono. Kasheshe iliwakumba walimu hao wakazi wa Bargoed kusini mwa Wales baada ya mzazi mmoja wa mwanafunzi katika shule wanayofundisha walimu hao kuiona video ya ngono ya walimu hao na kuwaripoti kwa uongozi wa shule.

Mwalimu wa shule ya msingi Jane Moyle, 44, inasemekana alijiuzulu kufundisha baada ya wadaku kusambaza habari za kuwepo kwa video ya ngono ya mwalimu huyo kwenye internet.

Mume wake Colin, 49, mwalimu wa sheria katika sekondari moja mjini humo alikuwa amechukua likizo ya miezi kadhaa kwa kuwa mgonjwa wakati walipotengeneza video hiyo. Walimu hao wako kwenye ndoa kwa miaka 20 sasa na watoto watatu.

Video yao hiyo inaaminika kuwa waliichukua kwenye nyumba yao iliyopo Merthyr Tydfil, kusini mwa Wales.

Inaaminika pia baadhi ya wazazi na wanafunzi wa walimu hao waliiangalia video hiyo kwenye internet kabla haijaondolewa baada ya taarifa kuzagaa.

Haijajulikana wazi kama walimu hao waliiweka wenyewe video hiyo kwenye internet au kama kuna mtu aliiiba na kuiweka huko.

Maafisa wa elimu wanachunguza kujua ni jinsi gani video ya ngono ya walimu hao iliwekwa kwenye internet.

Walimu hao wako kwenye hatari ya kupigwa marufuku kufundisha.
 
Hii nayo habari ya kisiasa au ume kosea jukwa mkuu? Maana siku za karibuni naona thread zikijaa jukwaa la siasa wakati hazina uhusiano wowote na siasa. Au ndiyo njia ya kufanya post ionekne na wengi kabla ya kuhamishwa kwa maana hili jukwa lina wasomaji wengi zaidi?
 
Back
Top Bottom