Video ya kusikitisha ya Rah P Akielezea Alivyoteswa na Kuzalishwa Watoto Wawili Marekani

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,080
Kwa muda mrefu rapper wa kike aliyewahi kutikisa nchini Tanzania, Rah P amekuwa kimya na kuendelea na maisha yake nchini Marekani.

Lakini wengi hawajui tabu na shida alizozipata baada ya kwenda nchini humo kutafuta maisha na kufuata ndoto yake. Hii ni interview iliyofanywa na Kali TV Online ambapo anasimulia jinsi alivyohangaika baada ya kuzalishwa watoto wawili na mwanaume ambaye alikuja kugundua kuwa ni muuzaji wa madawa ya kulevya.

Baadaye mwanaume huyo alikuja kukamatwa na hivyo kubaki mwenyewe akiwahudumia watoto wake wakati hakuwa na kazi. Baada ya hali hiyo alijikuta katika wakati mgumu na kusongwa na mawazo mengi kiasi cha kumfanya awe mlevi na kujikuta akifungwa jela.

Sasa anataka kufufua tena ndoto yake ya kufanikiwa kimuziki nchini Marekani. Atafanikiwa akiwa tayari ni mama wa watoto wawili?
 
Last edited by a moderator:
nampenda huyo binti, watoto wake wazuri pia, kama kapewa uraia fresh,mambo mengine yatajiset ,time will tel.l
 
Hayo ndiyo maisha kupanda na kushuka, kitu cha msingi awe focused ili aweze kuwajengea future nzuri watoto wake
 
Angekuwa bongo huyu sasa hivi angekuwa tayari anamaisha mazuri.. ....anadrive gari kali.........anaishi mjengo mzuri........kuna wanaume kibao wanapesa zao wangemuweka ndani na kumtunza.......yeye anaenda kukaa majuu akijua atakimbiza life......kule ukiwa mzuri utaishia kugeuzwa sex toy tu......watu wamevurugwa balaa na maisha
 
Dah anasikitisha sana ,anaongea kwa hisia mpaka analia ,kaacha shule kisa jamaa gani sijui alifall naye ,
Kumbe jamaa ni zungu la unga
Hapa ndio naposhindwa kuwaelewa baadhi ya wanawake anaacha ku persue dreams zake kisa mwanaume

Ila Kingereza chake kitamu kweli huwezi fikiri ni msukuma huyu


Sijui mdogo wake Caren Peyton kamaliza chuo pia


Usa baby

Siku nyingine mkikumbana na hayo rudini nyumbani na Marekani ndio hivyo haruhusiwi kufanya kazi popote

Nyumbani ni nyumbani tu
 
Dah anasikitisha sana ,anaongea kwa hisia mpaka analia ,kaacha shule kisa jamaa gani sijui alifall naye ,
Kumbe jamaa ni zungu la unga

Ila Kingereza chake kitamu kweli huwezi fikiri ni msukuma huyu


Sijui mdogo wake Caren Peyton kamaliza chuo pia
Nakjua kalisoma Loreto, klikuwa kazuri sana, chuo kalienda wap?
 
Back
Top Bottom