tinkibiruka mhaya
JF-Expert Member
- Jul 28, 2016
- 926
- 790
Yaani nimeitafuta hata siioni
Mwanamuziki wa Tanzania Diamond Platnumz amekosolewa mitandaoni kwa kutumia bendera yenye utata katika video ya wimbo wake mpya wa Gidi.
Bendera hiyo ni ya kundi la Shirikisho la majimbo ya kusini ya Marekani ambayo yalipigania kudumisha utumwa wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe na bendera hiyo inaonekana kama ishara ya mivutano ya ubaguzi wa rangi nchini Marekani. Moja ya kipande cha video atika wimbo wa Gidi kina bendera mbili zilizoonyeshwa wakati akicheza huku akiwa na muonkeano wa Cowboy.
Nini maoni yako juu ya video hii?
================================================================
Diamond Platinumz: Video ya wimbo mpya Gidi yakosolewa mitandaoni Marekani
Mwanamuziki wa Tanzania, Diamond Platnumz anakosolewa mtandaoni kwa kuangazia bendera ya Shirikisho kwenye video ya wimbo wake mpya.
Shirikisho lilikuwa ni kundi la majimbo ya Kusini ambayo yalipigana kudumisha utumwa wakati wa Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Marekani na bendera hizo zinaonekana kama ishara ya mivutano ya ubaguzi wa rangi nchini Marekani.
Moja ya matukio ya video ya Diamond katika wimbo wa Gidi ina bendera mbili zilizoonyeshwa wakati akicheza huku akiwa na muonekano wa Cowboy.
Baadhi ya watumiaji wa Twitter wametoa hisia zao kuhusiana na video ya msanii huyo.
"Bendera ya Muungano katika video yako inasumbua," aliandika mtumiaji mmoja.
"Bendera ya Muungano?"Clyde Blaise aliandika na kujuumisha emoji ya pipa la taka.
Kufikia sasa Diamond hajatoa tamko lolote kuhusiana na madai hayo.