Video ya "Gidi'' ya Diamond Platnumz yakosolewa vikali mtandaoni kwa kutumia bendera inayohusishwa na ubaguzi

Unapotumia alama ambayo inaakisi unyama waliofanyiwa (na kwa kiasi wanaendelea kufanyiwa) kundi fulani, halafu unapoambiwa kuwa alama hiyo inawaumiza ukakataa kuiondoa, ni kukosa utu. Sawa tuseme aliitumia kwa bahati mbaya au kutokujua, ila unapofahamishwa, tumia busara kuomba msamaha na kuiondoa.
Unamfahamisha ww kama nani?
 
Nafikiri huyu Mondi alitamani 'kufanania' na Lil Nas X, sasa akawa anaweka vitu bila ufahamu. Nimeona pia RODEO pale juu. Tahadhari tu asije kufanya video kama ya INDUSTRY BABY.
Video imefanywa na director wa south africa basi naye ni wakulaumiwa.

Kuna muda mwingine unakuta setting, script na mengineanayafanya director msanii ye anavutiwa tu na anachoona.

Sasa tuseme diamond alikiwa hajui, je na huyo director hakujua maana ya hiyo symbol
 
Ameandika Wakazi kuhusu ishu ya wimbo wa Diamond...

"NIENDE PRIVATE SIO?!

"Kilio cha baadhi yenu ni kwa nini sijaenda Private kuwaelekeza. Kwamba wafanye kitu PUBLIC alafu mimi nitoe maoni in PRIVATE… Sawa good suggestion!

"Ila ikumbukwe kuwa Wao sio wa kwanza kufanya makosa ya namna hii, na pia sio wa kwanza kwa sisi kuwasema hadharani tena kwa kushauri na sio kuwa zodoa wala kukejeli.

"2017: Q Boy Msafi alivaa Mavazi ya Ku Klux Klan (Kundi ya kibaguzi la Marekani) na pia nguo zenye Nembo ya Swastika (Ya Hitler wa Ujerumani) kwenye video yake na tukamsema HADHARANI.

"2019: Mr Blue alitoa video amevaa Gestupo Uniform na Nembo ya Swastika pia (Uniform za Police wa Nazi) na yeye tukamsema HADHARANI.

"2021: TCRA waliwafungia Wasafi Media miezi 6 kwa ile issue ya Gigy Money (ambae nae alionewa) na sisi tukapaza sauti kuwatetea Wasafi HADHARANI.

"So moja, sisi hatuna kinyogo nao, na wakionewa huwa tupo nao, na hatuna hila wala kisasi wa wivu. Mbili, pengine Dai angejifunza kutoka kwa hao ambao walifanya mistakes hizo akahakikisha harudii same mistakes.
Wasanii wa TZ kwa makosa tunayofanyaga kwenye videos na picha zetu huwa yanafanya tuonekane shallow sana nje huko. Na ni vyema kuweka mapungufu haya hadharani ili tuwasaidie Wasanii wa kizazi kijacho! Mbali na yote, wananchi wamefurahia kufahamu kidogo historia. Sio mbaya!! "

Wakazi

Pia Soma

Diamond Platinumz: Akosolewa mitandaoni Marekani kwa kupiga picha ilio na bendera ya 'ubaguzi'

22 Februari 2022
Imeboreshwa 23 Februari 2022
.

Chanzo cha picha, Diamond Platinumz
Mwanamuziki wa Tanzania Diamond Platnumz anakosolewa mtandaoni kwa kuangazia bendera ya Shirikisho kwenye kanda yake ya video ya wimbo wake mpya Gidi.
Shirikisho lilikuwa ni kundi la majimbo ya kusini ambayo yalipigana kudumisha utumwa wakati wa Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Marekani - na bendera hizo zinaonekana kama ishara ya mivutano ya ubaguzi wa rangi nchini Marekani.
Moja ya matukio ya picha hizo za Diamond ina bendera mbili zilizoonyeshwa wakati akicheza huku akiwa na muonekano wa Cowboy.
Baadhi ya watumiaji wa Twitter wametoa hisia zao kuhusiana na video ya msanii huyo.

"Bendera ya Muungano katika video yako inasumbua,"aliandika mtumiaji mmoja.

"Bendera ya Muungano?"Clyde Blaise aliandika na kujuumisha emoji ya pipa la taka.

Kufikia sasa Diamond hajatoa tamko lolote kuhusiana na madai hayo. Diamond ambaye ndiye msanii maarufu zaidi katika eneo la Afrika mashariki hajaepuka migogoro katika siku za hivi karibuni.

Mwaka uliopita msanii huyo maarufu alijipata mashakani miongoni mwa wapenzi wa tuzo za BET.

Chanzo; BBC Swahili News
 
Ameandika Wakazi kuhusu ishu ya wimbo wa Diamond...

"NIENDE PRIVATE SIO?!

"Kilio cha baadhi yenu ni kwa nini sijaenda Private kuwaelekeza. Kwamba wafanye kitu PUBLIC alafu mimi nitoe maoni in PRIVATE… Sawa good suggestion!

"Ila ikumbukwe kuwa Wao sio wa kwanza kufanya makosa ya namna hii, na pia sio wa kwanza kwa sisi kuwasema hadharani tena kwa kushauri na sio kuwa zodoa wala kukejeli.

"2017: Q Boy Msafi alivaa Mavazi ya Ku Klux Klan (Kundi ya kibaguzi la Marekani) na pia nguo zenye Nembo ya Swastika (Ya Hitler wa Ujerumani) kwenye video yake na tukamsema HADHARANI.

"2019: Mr Blue alitoa video amevaa Gestupo Uniform na Nembo ya Swastika pia (Uniform za Police wa Nazi) na yeye tukamsema HADHARANI.

"2021: TCRA waliwafungia Wasafi Media miezi 6 kwa ile issue ya Gigy Money (ambae nae alionewa) na sisi tukapaza sauti kuwatetea Wasafi HADHARANI.

"So moja, sisi hatuna kinyogo nao, na wakionewa huwa tupo nao, na hatuna hila wala kisasi wa wivu. Mbili, pengine Dai angejifunza kutoka kwa hao ambao walifanya mistakes hizo akahakikisha harudii same mistakes.
Wasanii wa TZ kwa makosa tunayofanyaga kwenye videos na picha zetu huwa yanafanya tuonekane shallow sana nje huko. Na ni vyema kuweka mapungufu haya hadharani ili tuwasaidie Wasanii wa kizazi kijacho! Mbali na yote, wananchi wamefurahia kufahamu kidogo historia. Sio mbaya!! "

Wakazi
Tatizo. La watu wengi,hawafanyi kitu chochote wanasubili watu wafsnye Ili wakosoe,sasa unajiuliza kama Mond asingetoa hiyo video,wangesema nini?
Hawana wanachokifsnya,wapo wapo tu,wanasubili wengine wafanye,Ili nao waseme
 
kwanza huyo ni nani? Pili, ikiwa mtu kakosea na wewe utamfuatisha makosa yake kisa wewe siyo wa kwanza? Tusihalalishe makosa.
Kwa hiyo humjui ila nawe umeamua kubisha?

Huyo ni Ludacris na pamoja na kuvaa hiyo bendera bado ana pata mashavu ya movie za Fast and Furious.
 
Mwanamuziki Diamond Platnumz, wiki hii amejikuta mashakani kwa kukutana na ukosoaji mkubwa kwenye mitandao ya kijamii kutokana na kuonekana kwa bendera inayoonekana inaunga mkono vitendo vya ubaguzi wa rangi na utumwa.

Sehemu ya video ya wimbo huo unaoitwa 'Gidi' iliyotoka hivi karibuni inamuonyesha msanii huyo akiwa amesimama kwenye sehemu inayoonekana ya kuuzia vinjwaji 'kaunta' sehemu nyuma yake kwa juu ya kaunta hiyo kuna bendera hizo zinazofahamika kama 'Confederate flags'.

Ukosoaji huo ulianza kushika kasi zaidi mara baada ya mmoja wa wasanii wa muziki wa hip Hop Tanzania, Webiro Wakazi Wassira, ambaye pia ni mwanasiasa wa Chama cha ACT Wazalendo, kukosoa uwepo wa bendera hizo kwenye video hiyo alipoandika kupitia mtandao wake wa Twitter.

Wakazi alimtaka Diamond kurekebisha vipande vya video vinavyozionyesha bendera hiyo.
ConfederateFlagSitecore.jpg


Nini asili ya Bendera za Confederate Flag?
Bendera hizi zinawakilisha muungano ulioitwa Confederate States of America (CSA au Confederacy), ulioanzishwa mwaka 1861 baada ya majimbo 11 ya Marekani kuamua kujitenga katika nchi hiyo iliyokuwa na umri wa takribani miaka 85.

Majimbo hayo ni Alabama, Arkansas, Florida, Georgia, Louisiana, Mississippi, North Carolina, South Carolina, Tennessee, Virginia na Texas.

Uasi wa majimbo hayo 11 ulichochewa zaidi na kuchaguliwa kwa Abraham Lincoln kuwa rais. Rais Lincoln alikuwa na msimamo wa kusitishwa kwa biashara ya utumwa, huku majimbo hayo yalikuwa yanatetea vitendo hivyo.

Kukazuka vita kubwa kati ya majimbo hao na majeshi ya Marekani. Ni vita vilivyodumu kwa miaka 4, vikionekana kama vita kati ya watu weupe na watu weusi, kabla ya kumalizwa mwaka 1865, ikionekana kama ushindi dhidi ya utumwa na ubaguzi wa rangi.

Baada ya vita hiyo, kumekuwa na harakati za muda mrefu za kukabiliana na utumwa, kwa zaidi ya miaka 155 nchini Marekani, lakini harakati zinazoonekana kuwa tata, wamarekani wengi weupe, hasa wa Kaskazini mwa taifa hilo, wameonekana kutojitoa sana kupambana dhidi ya ubaguzi.
Mondiii.jpg


Kupigwa marufuku kwa bendera za"Confederate Flag'
Bendera na viashiria vyote vinavyoonekana kutukuza utumwa na ubaguzi wa rangi, vilianza kutoweka kidokigo ikiwemo makao makuu ya Bunge la Marekani, huku maeneo mengine mengi wakipiga marufuku.

Wachuuzi wa bendera walitangaza kutoziuza kutokana na namna zinavyochukuliwa, huku kifo cha mmarekani mweusi, George Floyd, kilichocheza zaidi hasira za kutokomezwa kwa viashiria vya ubaguzi ikiwemo bendera hizo.

Ingawa ni zaidi ya miaka 150 sasa tangu majimbo hayo 11 yashindwe vita kutetea utumwa, bado bendera hiyo inaendelea kuigawa Marekani, lakini kuleta msigano pia hata nje ya taifa hilo hasa kwa watu weusi.

Watu wanaoonekana kuwa na bendera hizo katika himaya zao wanachukuliwa kama ni watu wanaotukuza vitendo vya utumwa na ubaguzi wa rangi.

Kwa watu weusi, bendera hiyo inawapa hasira wakirejea mateso na maumivu ya utumwa na ubagunzi yaliyofanyika kwa miaka mingi wakati wa utumwa. Watu wengi weupe hasa nchini Marekani wanaopeperusha bendera hizo hukutana na mashambulizi ya mara kwa mara na wengine wakihukumiwa.

Haishangazi, ukosoaji unaofanyika sasa dhidi ya Msanii Diamond, ni kwa dhana hiyo hiyo ya kwamba ni bendera isiyofaa kutokana na kuhusishwa kwake na vitendo vya kitumwa na kibaguzi.

Wako watu wengi maarufu waliojikuta matatizoni kwa sababu ya bendera hizo. Hawa ni baadhi ya wasanii wengine maarufu waliojikuta matatani kutokana na kutumia bendera za "Confederate Flag' kwenye kazi zao za Sanaa.


KANYE WEST
Mwaka 2013, Kanye West alipigwa picha akionekana amevalia jaketi ambalo lilikuwa limenakshiwa na bendera za Confederate flag' kabla ya kuuzwa kwenye mdana wakati wa tamasha lake la Yeezus.

Wengi walimshambulia kabla ya kujitokeza huko Los Angeles na kufafanua kwa nini alivaa kama alivyonukuliwa na mtandao wa the dailybeast.com:

"Semeni mnavyotaka," West alisema wakati huo. "Nguvu yoyote ni nguvu. The Confederate flag inawakilisha utumwa kwa namna fulani. Hicho ndicho nachofahamu. Kwa hiyo niliandaa wimbo 'New Slaves.' Nikatumia bendera hiyo."
Wasanii.jpg


LUDACRIS
Msanii wa Hip Hop wa Marekani ambaye alishambuliwa vikali baada ya kuvaa mavazi yenye bendera hiyo ya 'Confederate flag' wakati akitumbuiza wimbo wake uliovuma "Georgia" kwenye tuzo za VIBE, huko Atlanta.

Ludacris ilibidi ajitokeze kuweka sawa hali ya hewa, na kusema hakulenga kutukuza ubaguzi bali kupinga.

"Bendera hii inawakilisha ukandamizaji ambao sisi waafrika tumepitia kwa miaka mingi; hii ni alama ubaguzi sio tu Kusini lakini ni Marekani. Mi nilivaa kuwakilisha tulipotoka kwa sababu ya ubaguzi. Mwishowe nilivua na kuvaa bendera nyingine yenye rangi nyeusi, nyekundu na kijani, hizo ni rangi za Afrika,” alisema Luda.

ANDRÉ LAUREN BENJAMIN 'ANDRE 3000'
Huyu ni mmoja wa wasanii wawili wanaounda Kundi la OutKast. Mwaka 2000 Andre 3000 na yeye alishambuliwa na baadhi ya Wamarekani baada ya kuonekana kwenye moja ya video za OutKast akiwa na bendera ya Confederate flag.

Andre 3000 alionekana na bendera hizo kwenye mkanda wake wa suruali kwenye moja ya video maarufu za kundi hilo ya "Ms. Jackson."

Licha ya kutojitokeza hadharani kueleza kinagaubaga kwa nini alivaa, watu wengi waliendelea kwa muda mrefu kumsakama.

Msanii wa kufokafoka wa muziki wa Crunk, kama ilivyo kwa Diamond na yeye ameonekana akiwa na bendera hizo kwenye wimbo wake maarufu wa "This Tha City" uliotoka mwaka 2000.

LIL JON
Lil Jon & the Eastside Boyz's kupitia kava ya albamu yao iliyoitwa Put Yo Hood Up na kuibua makelele.



Source: bbc
 
Huyu kukaa marekani anajifanya George Bush. Yote aonekane anayajua ya ndani ya amerika.
 
Jamaa anajifanya mjuaji Sana anachokifanya wakazi ni kama yeye ni shabiki badala ya kuwa msanii lengo kuu lilikuwa ni kutaka kiki kwanini usigeuze mziki wako uwe kiki
 
Nafikiri huyu Mondi alitamani 'kufanania' na Lil Nas X, sasa akawa anaweka vitu bila ufahamu. Nimeona pia RODEO pale juu. Tahadhari tu asije kufanya video kama ya INDUSTRY BABY.
Na avyopenda kuiga Sasa🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom