Video ya Eric Omondi yamtoa povu Barakah The Prince

chilamanyika

JF-Expert Member
Nov 20, 2016
405
272
Video ya Eric Omondi yamtoa povu Barakah The Prince

Baada ya Eric Omondi kuachia video ya parody ya wimbo wa ‘Kuliko Jana’ wa Sauti Sol, msanii wa Bongo Fleva Barakah The Prince amemjia juu mchekeshaji huyo.

Hitmaker huyo wa Nisamehe ameonyeshwa kuchukizwa na baadhi ya vipande vya kwenye video hiyo na kuamua kuweka wazi kupitia mtandao wa Instagram.
15101563_1134229833359198_5851538889465921536_n.jpg

Kupitia mtandao huo, Barakah ameandika:

Ukiona unakosa cha kuchekesha watu bora utafute kazi nyingine ya kufanya kuliko alichofanya huyu sijui ndio anaitwa nan…kawakosea sana watu wote wenye imani ya kikristo…tafuta kazi nyingine… maana vichekesho nahisi umefikia mwisho…huyu jamaaa kafanya asubuhi yangu kuwa mbaya sana..shukuru wakristo ni wapole..ukifanya kitu ichi kwa Muslim..ungefanywa mfano..

 
Kwani video original ambayo yeye "kaigerezea" ya hao Sauti sol haiko hivo ........??
 
Kawakosea kitu gani maana katumia maneno yaleyale ya wimbo wa saut sol.. Labd jinsi alivyoigiza kama yesu
 
Kwani video original ambayo yeye "kaigerezea" ya hao Sauti sol haiko hivo ........??
Unatuuliza au unatupa jibu? Kafanye research halafu uje na jibu hapa usipende kuropoka
 
Nadhani jamaa ka~react kitoto bila kufikiria, yeye anadhani Omondi anamkejeli Yesu kwa kukaa msalaba ulioandikwa "Mwizi Forgiven" ila anasahau kitu kimoja, kua Yesu aliwekwa msalabani pamoja na watu wengine wawili ambapo moja wao alikua ni mwizi ambaye Yesu alimsamehe, kwa hiyo Omondi anaweza kua alikua anamuigiza yule mwizi aliyesamehewa.

Ni vizuri kutumia akili kidogo kabla ya kukurupuka mwisho wa siku mtu anaaibika kama hivi kwa kua alipata wrong idea. Watu wa dini hua mna mihemko ya ajabu mkiweka akili pembeni.
 
Huyo nae kwanza wakristu hatupo hivyo tunaunyenyekevu na hekima,na sheria ya kuwekwa msalabani kwa wayaudi ni kitu cha kawaida kwa muharifu yeyote.
 
Video ipo kawaida sana ingawa alichokisema Baraka de Prince ni kweli.
Hapo angekua ni mtume Leo hii Kuna majengo yangeungua moto!
 
Huyo nae kwanza wakristu hatupo hivyo tunaunyenyekevu na hekima,na sheria ya kuwekwa msalabani kwa wayaudi ni kitu cha kawaida kwa muharifu yeyote.
Kwa hiyo jesus alikuwa muhalifu hadi wamtundike msalabani?
 
Back
Top Bottom