Video: Wataliban wakisherekea baada ya Wanajeshi wa Marekani kuondoka Afghanistan

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
414
Ndege ya mwisho iliyowabeba wanajeshi wa Marekani imeondoka jana nchini Afghanistan na kuashiria kumalizika kwa vita vya miaka 20, vinayotajwa kuwa virefu zaidi katika historia ya Marekani.

Kuondoka kwa Wanajeshi wa Marekani kunakuja wakati dunia ikishuhudia kushindwa kwa wanajeshi hao kudhibiti utawala wa Wanamgambo wa Taliban wanaotajwa kuwa na kikosi dhaifu chenye wapiganaji takriban 75,000 dhidi ya kikosi cha Wanajeshi zaidi ya 300,000 wa Afghanistan waliopewa mafunzo na silaha za kisasa na Jeshi la Marekani, ikiwa ni maandalizi ya wakati kama huu. Hata hivyo, wapiganaji wa Taliban walifanikiwa kuchukua utawala nchini Afghanistan kwa njia rahisi, wakichukua baadhi ya majimbo bila upinzani wowote, huku rais wa Taifa hilo, Ashraf Ghani akikimbia taifa hilo siku moja kabla ya Wapiganaji wa Taliban kuchukua udhibiti wa Mji Mkuu, Kabul.

Ndege hiyo ya mwisho ya Jeshi la Marekani, aina ya Boeing C-17 imeondoka huku kati ya Wamarekani 100 hadi 200 wakiwa bado nchini humo, pamoja na maelfu wengine waliosaidia utawala wa Marekani nchini humo kwa miaka 20 iliopita.

Rais Biden, ambaye anakabiliwa na ukosoaji mkubwa kwa jinsi Wanajeshi wake walivyoondoka nchini Afghanistan, amewapongeza Wanajeshi wa Marekani waliokuwa nchini Afghanistan na kufanikiwa kuondoka kwa muda uliopangwa bila kutokea vifo zaidi.

"Ndani ya siku 17 zilizopita, Wanajeshi wetu wamefanikiwa kuwaondoa watu wengi zaidi kwa njia ya anga katika historia ya Marekani, zaidi ya watu 120,000 wamefanikiwa kuondolewa nchini Afghanistan. Wanajeshi wetu wamefanikisha jambo hilo kwa weledi mkubwa," taarifa ya Biden ilisema, huku akitarajiwa kuzungumza baadaye hii leo.

Wapiganaji wa Taliban wameonekana wakipiga risasi hewani kusherekea kuondoka kwa Wanajeshi wa Marekani usiku wa leo.
"Wamarekani wameondoka, Afghanistan imejipatia uhuru kamili," Zabihullah Mujahid, Msemaji wa Taliban aliviambia vyombo vya habari baada ya ndege ya mwisho ya Marekani kuondoka nchini humo.



1630385140933.png


Mwanajeshi wa mwisho wa Marekani nchini Afghanistan, Meja Jenerali Chris Donahue akipanda ndege ya Jeshi la Marekani, C-17 katika Uwanja wa Ndege wa Hamid Karzai mjini Kabul kuashiria kuondoka kwa Wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan
 
Ni heri vita na adui unayemuona kuliko vita na adui usiyemuona.

Marekani anarudi tena hapo kupitia makundi ya wana mgambo na itakua ni hatari zaidi kwa hao Taleban maana maswala ya humanitarian hayatazingatiwa katika vita hiyo.
US ameshasoma ramani ya kudeal na maadui; they train your people, then equip you with all sorts of deadly weapons, kisha anawaacha mwuane wenyewe kwa wenyewe. Support pekee atakayokupatia ni utetezi na justifications (labda na kuwashawishi marafiki wawakopeshe fedha za kuendeleza vita vingine zaidi), thousands miles away, kwenye mabaraza ya usalama ya Umoja wa Mataifa!!!
 
Muda mfupi uliopita iran imelitangaza kundi la talban kuwa limeshinda vita. Wakati huo huo marekan inapanga kukimbia huko iraq
 
Msiongee Kama mmelewa , nitajie Vita ambayo marekani ameshinda kuanzia vietnam, Iraq, Syria, Yugoslavia etc
" Wanajeshi wa marekani ni waziri ktk ndege ambapo hiyo siyo Vita ya ushindi ni Vita ya kubomoa majengo, powerplants, miundombinu mbalimbali ili ushuke kwa ground forces hapo ndipo marekani na wazungu wa ulaya wanapogeuzwa mboga.
Kule Afghanistan ilifika hatua Askari waliotumwa vitani , nao wanatumia Askari wa kiafghan kwa kigawana posho .ni aibu
 
Ni heri vita na adui unayemuona kuliko vita na adui usiyemuona.

Marekani anarudi tena hapo kupitia makundi ya wana mgambo na itakua ni hatari zaidi kwa hao Taleban maana maswala ya humanitarian hayatazingatiwa katika vita hiyo.
Tayari Ant-Taleban Resistance wapo
 
Marekani ni Uharo tu,wanafikiri watu wanaect movies kama wao?watu wamechoka kitambo wanafanya kweli tu Damn
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom