VIDEO - Wanawake Waiba Bia na Kuzificha Kwenye Nyeti...

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,083
VIDEO - Wanawake Waiba Bia na Kuzificha Kwenye Nyeti...
5839914.jpg
Tuesday, July 26, 2011 3:08 AM
Wanawake hawa wawili wamekuwa wanawake wanaotafutwa kwa uhalifu kuliko wanawake wote nchini Marekani kutokana na staili yao ya wizi ya kuiba pombe za gharama na kuzificha kwenye sehemu zao za siri.
Wanawake hao wawili wanatafutwa na polisi wa Florida, Marekani baada ya kufanya matukio mawili ya uhalifu kwa kuiba chupa za pombe zinazouzwa kwa bei kubwa sana na kuzificha kwenye sehemu zao za siri.

Wanawake hao wawili waliingia kwenye duka moja la pombe na kuuiba chupa nne za mvinyo unaoitwa Moet Rose. Chupa hizo nne zilikuwa na thamani ya jumla ya dola 400.

Wanawake hao kama kawaida yao walizificha chupa hizo kwenye sehemu zao nyeti na kutoka ndani ya duka hilo bila kugundulika.

Kamera za ulinzi CCTV zilinasa tukio hilo LIVE na polisi hivi sasa wanazitumia video zilizopatikana kuwatafuta wanawake hao wezi.

Mwezi Oktoba mwaka jana, duka la pombe lililokaribu na duka hilo nalo lilitiwa hasara kwa dizaini hii na wanawake ambao wanahisiwa kuwa ndio hawa hawa walionaswa kwenye CCTV.

Angalia VIDEO ya wanawake hao vibaka wakizisunda chupa za bia kwenye sehemu zao nyeti.

VIDEO - Wanawake Waiba Bia na Kuzificha Kwenye Nyeti...

<tbody>
</tbody>


:dance:
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom