Video: Wanajeshi wa Ukraine zaidi ya 900 waliojificha Azovstal, Mariupol wajisalimisha kwa majeshi ya Russia

Sikirimimimasikini

JF-Expert Member
Dec 27, 2019
2,919
15,604
Russia imesema wanajeshi wa Ukraine mia tisa na hamsini na tisa (959) waliokuwa wamejificha kwenye kiwanda cha chuma huko Azovstal, Mariupol wamesalimu amri hadi kufikia jana (juma nne). Kati ya hao 959, wnajeshi 80 walikuwa wamejeruhiwa na kati yao 51 walipelekwa hospitali iliyo chini ya uangalizi wa Russia kupatiwa matibabu.

Wakati Zelensky na vyombo vya habari vya magharibi vikisema kuwa Ukraine imefanya misheni ya kuwaokoa wanajeshi hao waliokuwa wamejificha kama panya kwenye mahandaki ndani ya kiwanda cha cha chuma, Azovstal, wanajeshi hao wamejikuta wakiingia mikononi mwa majeshi ya Russia. Kwa upande wake Russia yajiandaa kuwafungulia mashitaka ya kigaidi wapiganaji wa Azov, ambapo wataishia kula shaba badala ya kuchukuliwa kama wafungwa wa kivita.

Ifuatayo ni video ikionesha wanajeshi hao wa Ukraine, wakisalimu amri na kusachiwa na majeshi ya Russia.

========

Screenshot_20220518-135247_Chrome.jpg
Screenshot_20220518-135444_Chrome.jpg
 
Russia imesema wanajeshi wa Ukraine mia tisa na hamsini na tisa (959) waliokuwa wamejificha kwenye kiwanda cha chuma huko Azovstal, Mariupol wamesalimu amri hadi kufikia jana (juma nne). Kati ya hao 959, wnajeshi 80 walikuwa wamejeruhiwa na kati yao 51 walipelekwa hospitali iliyo chini ya uangalizi wa Russia kupatiwa matibabu.

Wakati Zelensky na vyombo vya habari vya magharibi vikisema kuwa Ukraine imefanya misheni ya kuwaokoa wanajeshi hao waliokuwa wamejificha kama panya kwenye mahandaki ndani ya kiwanda cha cha chuma, Azovstal, wanajeshi hao wamejikuta wakiingia mikononi mwa majeshi ya Russia. Kwa upande wake Russia yajiandaa kuwafungulia mashitaka ya kigaidi wapiganaji wa Azov, ambapo wataishia kula shaba badala ya kuchukuliwa kama wafungwa wa kivita.

Ifuatayo ni video ikionesha wanajeshi hao wa Ukraine, wakisalimu amri na kusachiwa na majeshi ya Russia
View attachment 2229312
========

View attachment 2229298View attachment 2229299
Vita ni vita muraa!! Hatari sana,yaani ukishakuwa POW(prisoner of war),jamaa wanaweza kukufanya chochote!!
 
Rudi nyumbni haraka sana mkuu Filand nao wameshupaza Kauli ya Kaka Putin Soon litawakuta Jamboo

Hawezi kutuvamia, sema haya majitu ni maoga tu. Ila hata akivaamia huku jamaa wamejiandaa. Tuna mihandaki watu wanaweza kuishi na maisha kuendelea hata miaka miwili bila kutoka huko chini.

Huu ni mfano mmoja tu.

wafini wanajua nuclear war is coming soon. So wanajianda kwao na raia wao thr same na Swiss wanajenga underground all over the country. Huku sie tusubiri kudra tu za Mungu. Ila wanafini walishapigana na ussr huko nyuma so wanajuana. Kwenye yale mabarafu wanawezana 50/50 . tofauti na ukraine....so sidhani kama putin ataivamia hii nchi.
 
... mambo ya kawaida sana hayo katika medani za kivita; sioni la ajabu hapo! Anyway, Mungu husimama upande wa haki siku zote.
 
Back
Top Bottom