Uchaguzi 2020 VIDEO: Wachambuzi wa siasa Kenya washangazwa na muundo wa uchaguzi wa Tanzania, wasema walitoka huko kitambo sana

Kiukweli wakenya wana haki ya kutucheka! Katiba yao na jinsi wanavyoheshimu haki za makundi ya kiraia ni darasa tosha kwa Tanzania! Yote hayo ni matokeo ya kukitupa nje chama kikongwe cha KANU!

Sisi huku bado tunaendeleza sisasa za kikoloni kwasababu bado tunatawaliwa na chama kikongwe kilichong'ang'ania hadi sheria za kikoloni na ulaghai wa kila aina! Mkiongeza pressure ya kudai katiba mpya, wakija kwenye kampeni wanawambia chagua flani ataleta katiba mpya, mkshamchagua mnaambiwa katiba mpya sio kipaumbele!
Hakuna kitu kama hichoJJuzi ulisikia mkwaruzano baina ya mahakama kuu na bunge
Mahakama kuu inamtaka rais Kenyatta kulivunjilia mbali bunge la nchi hiyo kwakuwa limeshindwa kutekeleza takwa la kikatiba katika kuweka usawa wa kijinsia na makundi mbali mbali
 
Pale Kenya sasa hivi ni kama hamna mkubwa! Kila mtu ni kambare! Wamejaa ukabila, hayo ndio waliyoendelea hakuna kingine.

Fikiria uchaguzi bado miaka 2 lakini ofisi ya rais Kenyata ina mgogoro wa kugombea madaraka ya 2022
Do not project your problems to your neighbor. If the same neighbor tells you have a bad eye accept and treat it.
 
Tanzania ni nchi ambayo vijana waoga mno wanaishia kujipendekeza tuu kwa viongozi wawo...mwisho wasiku wanaishia dustbins.... Mfano mnzuri Bashite.......Polepole watch out.
 
Kiukweli wakenya wana haki ya kutucheka! Katiba yao na jinsi wanavyoheshimu haki za makundi ya kiraia ni darasa tosha kwa Tanzania! Yote hayo ni matokeo ya kukitupa nje chama kikongwe cha KANU!

Sisi huku bado tunaendeleza sisasa za kikoloni kwasababu bado tunatawaliwa na chama kikongwe kilichong'ang'ania hadi sheria za kikoloni na ulaghai wa kila aina! Mkiongeza pressure ya kudai katiba mpya, wakija kwenye kampeni wanawambia chagua flani ataleta katiba mpya, mkshamchagua mnaambiwa katiba mpya sio kipaumbele!
2015 ilibaki kidogo tukiondoe tumpe LOWASA.
 
Niliyoyazungumza ndiyo mada yenyewe...mada ni tume huru na demokrasia..huko Kenya ni Nani anateua hiyo tume inayodaiwa ni huru?! Composition ya wanaoteua ikoje?! Na composition ya walioteuliwa ikoje?! Suala hapa siyo Nani anateua?! Issue hapa no utendaji wa tume na impartiality katika utendaji...je, hiyo tume ya Kenya iko impartial?! To what extent?! Kama iko impartial ni vipi Kila baada ya uchaguzi kunakuwa na shida na hata mapambano ya silaha na mamia kuuawa?! Hujui kuwa viongozi wa Kenya waliwahi kushirakiwa kwenye mahakama ya kimataifa baada ya uchaguzi?! I hate watu wanaozungumzia demokrasia wasijue maana ya demokrasia...do you think in Kenya media iko free?! To what extent?! Do you think media Kama the Daily Nation itakosoa miradi ya Aghakan? People are talking of democracy and they mean liberal democracy. Do you think liberal democracy is feasible in Africa in each and every aspect?!
1.If Electoral Commission is partial can you challenge the results in the court??=Yes as Rafki wa Magufuli(Odinga) disputed the election results
2.Is judiciary independent =Yes as they nullufied the presidential election though Rafik wa Magufuli(Raila) knew better Uhuru aka UK wasnt his class
3.Is media free=yes freedom of expression is considered as one of the birth rights hakuna kulazimisha KBS
 
Hawa ni wachambuzi wa kisasa nchini Kenya wakishangazwa na namna Tanzania ilipo bado kwenye ukoloni japo ni wa watu weusi.

Ni sisi wanaotubeza Tuliwaokoa Wasichinjane, Tungekuwa Wa Ovyo Tusingefanya Hayo. Kinachowasumbua Kinajulikana...
Na mfumo wao ungekuwa Imara, Mahakama ISINGE TENGUA MATOKEO NA KURA KURUDIWA
TUME YAO INGESIMAMIA VIZURI TU WALA MAHAKAMA ISINGEKUWA NA HAJA YA KUTENGUA MATOKEO..
SABABU Za Kutengua Nini UCHAGUZI HAUKUSIMAMIWA VIZURI , ULIKUWA WA WALAKINI
 
Bungeni wapinzani huwa hawasikilizwi na hasa akikaa Batina pale mbele au Spikaccm ndungai, wewe bure kabsa hujui kuwa bunge nalo kwenye utawala huu wa kishamba na kishetani hakuna haki kwa wabunge wa upinzani pindi wawapo Bungeni.
Yaani eti kila mtu anawatetea wabunge! Kama kazi hailipi au ina mazingira magumu, waambieni waache! Kwa nini walazimishe kazi mbaya na ngumu? Sasa hivi wanapigana vikumbo kuitafuta tena kazi hiyo kwa kujidai wanatupigania, ujinga huo!
 
Bwana jela,

Umesoma katiba ya Kenya? Huwezi kuilinganisha na ya Tanzania. Ni nzuri mno!
Ufahamu ni tatizo! Tuseme ni katiba nzuri sana! Je, imewasaidia wakenya? Tatizo siyo maandiko ndani ya katiba, ni akili ya watekelezaji na hao watu Kenya hawapo! 2022 watakuwa vitani tena, si wameshaanza? Wanagawana uongozi kikabila kwani imo ndani ya katiba?
 
Unapoleta habari kama hii toka Kenya, naelewa tu kwamba uelewa wako ni mdogo. Yaani Kenya itufundishe nini? Umesema ni wachambuzi, wewe unasemaje? Tunatafuta uelewa siyo copy-paste ya yanayotokea Kenya ambayo ni foolishness. Tunaoifahamu Tume ya uchaguzi ya Kenya ni lini imekuwa impatial? Tume yao haiko huru hata siku moja na ndo maana kamishna Chris Msando aliuwawa, Makamishna wakajiuzuru. Mwanzoni upinzani uliandamana kutaka wajiuzuru ikashindikana hadi watu kuuwawa!

Tafadhari lete vitu vyenye mantini. Hii ni TZ haiko hapa kukopi mambo ya kenya ambayo ni majivuno ya kijinga tu! Wao wanatamani wawe kama wazungu hata kwenye magonjwa kama corona, wakati wako hapa Afrika. Kwa nini wameshindwa kuiga mambo yetu hadi leo au nawe unaamini Corona inatuua sana? Stop these nonsense!
Chris Musando (Rip) alikuwa ni mkuu wa kitengo cha mawasiliano IT katika tume ya uchaguzi Kenya na wala hakuwa Commissioner.

Ni kweli kabisa kuwa tume ya uchaguzi Kenya sio huru kihivyo na madhaifu yake yanaonekana zaidi hasa kwenye kura ya urais. Tume hiyo haina kabisa tatizo kwenye maeneo mengine kama udiwani na ubunge.

Kwenye kura za udiwani na ubunge nchini Kenya hakuna kabisa figisu na anayeshinda au kushindwa ni kwa uhalali 100%.

Sasa turudi hapa Tanzania, tume ya uchaguzi inaanza kuipendelea ccm hata kabla ya uchaguzi kwa kuwaengua wagombea wa vyama vya upinzani katika ngazi zote ili kuipa ccm urahisi wa kushinda uchaguzi.

Ili rais akuteue kwenye tume ya uchaguzi Tanzania sifa kuu kabisa lazima uwe mwanachama hai wa chama cha Mapinduzi tofauti kabisa na Kenya.

Kwa hiyo huwezi kulinganisha muundo au utendaji kazi wa hizi tume na ndio maana Kenya makamishna wa tume ya uchaguzi wanathubutu kujiuzulu endapo wakiona wanataka kuingiliwa katika shughuli zao kitu ambacho Tanzania hakiwezi kutokea kamwe.

Tume ya uchaguzi Tanzania watumishi wake wote wakuu ni wateule wa rais na wanakula kiapo cha uaminifu kwake na ndio maana kwenye uchaguzi wa Tanzania kwa kiwango kikubwa rais anatembea na matokeo kwenye kampeni tofauti na Kenya.

Baada tu ya uchaguzi huu kumalizika inatakiwa kinachofuata kiwe kupigania katiba mpya kwa gharama yoyote ili kuondoa hii hali inayoitia nchi aibu na ambayo siku si nyingi itapelekea watu watinge The Hague, Uholanzi.
 
Mdharau kwao mtumwa kwa nini ukashabikie Kenya wakati Zbar kuna Tume Huru baadhi ya wajumbe ni wa vyama vya upinzani
 
Kama ni matatizo yetu tuyajadili wenyewe, siyo mtu anatuletea mambo ya Kenya kama rejea ya mafanikio na majivuno yao bandia. Nayaita bandia kwa sababu wakenya kila wakati wanajiona eti wako bora kuliko sisi wakati kisiasa wako hovyo kabisa. Baada ya Rwanda, ndo pekee waliouwana ktk ukanda huu kwa sababu za uchaguzi. Bahati mbaya sana sisi, kama unavyoona akina dikteta2020 anamwita mtu ni mchambuzi wakati hana lolote! Mafanikio ni mfumo siyo kuandikwa tu ktk katiba. Z'bar tume ilipalaganyika pamoja na kwamba ilikuwa na uwakilishi wa vyama vyote vikuu!

Hapa kwetu mambo yako hovyo kabisa na tunaostahili kulalama ni sisi wananchi. Hawa wanasiasa wetu wa upinzani wako hovyo maana ndo wamekuwa Bungeni miaka yote wakifanya show off. Wanalalama ili sisi wananchi tuwasaidie kurudi Bungeni, wakifika hatuwasikii wakitia presha juu ya mambo ya msingi. Leo hii tusingekuwa na mkuu wa mkoa au wilaya anayejihusisha na siasa za CCM. Wako kimya wakihangaikia kusikika Bungeni kwa matusi nk. ili uchaguzi ukifika warudishwe.

Mtu kama Lissu nilitegemea apambane na mambo kama hayo na jumuiya ya kimataifa, badala yake yeye ana mwanasheria anayemlinda, yeye akiwa nje ya nchi; zoezi la kijinga kuliko yeye mwenyewe anavyoamini. Yaani ashinde wakati majimbo yako chini ya wakurugenzi, usalama uko chini ya mkuu wa wilaya, na mkuu wa wilaya ni mkuu wa usalama wilayani? Halafu unategemea vitisho na kujivuna eti tutawapeleka mahakamani! Trash!
 
Siasa za Kenya ni za ubaguzi wa kikabila.

Kenya wapambane kwanza waondoe hili kabla ya wao kukosoa wengine.
Kwa hyo rais akiteua yeye mwenyekiti wa tume ndio ameondoa ukabila? Ni kwel Kenya wanaukabila lakn n haki rais ambaye n mgombea kuchagua mwenyekit wa tume?
 
Kuna wendawazimu unawakuta kwenye thread za dar v nairobi. Hovyo kabisa, Kenya imetuacha mbali ktk mambo mengi.

Ili utoke usonge mbele ni lazima ukubali hali yako kwanza kisha uchukue hatua.
 
Kwenye kura za udiwani na ubunge nchini Kenya hakuna kabisa figisu na anayeshinda au kushindwa ni kwa uhalali 100%.
Katika mazingira anayoyazungumzia Mohamed Ali wa Jicho Pevu( tazama clip hapa chini) unaweza kujiridhisha kabisa kuwa uchaguzi wa wabunge na udiwani unaenda sawia na murua huko Kenya? Tusidanganyane!!!

Hao jamaa wana demokrasia sana, Tanzania hii nani anaweza kuongea hivyo tofauti na Lissu.

Hayo maswala anayoongelea huyo mbunge mbona ni yale yale ya ufisadi na hata huku tunayo, mtu anatwaa pesa za umma kwenda kujengea uwanja wa ndege kwao na ukiuliza unaletewa wasiojulikana.

Kama Kenya ni sawa na Colombia je Tanzania ina tofauti gani huku kuna watu hadi leo haijulikani walipo.

Yanayofanyika katika mashirika kama Air Tanzania hakuna anayejua na hata kwenye ujenzi wa bwawa la Stieglar Gorge na hata reli ya Standard Gauge, tunaambiwa ni siri ya Magufuli na mpwa wake. Hamna kitu hapo.
 
Back
Top Bottom