VIDEO - Vimombo Vya Wasanii Wabongo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

VIDEO - Vimombo Vya Wasanii Wabongo

Discussion in 'Entertainment' started by Ng'wanza Madaso, Sep 23, 2009.

 1. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #1
  Sep 23, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  VIDEO - Vimombo Vya Wasanii Wabongo
  [​IMG]
  Nyota wa filamu za Bongo, Steven KanumbaTuesday, September 22, 2009 4:04 PM
  Libeneke la uwezo wa wasanii wa Bongo kutema ngeli limeendelea tena na mwanadada Sporah, Mtanzania anayeendesha shoo yake kwenye televisheni moja ya Uingereza ametoa video za wasanii wa kibongo kama vile Kanumba, AY, Mwana FA wakitema ngeli walipokuwa kwenye ziara zao za kisanii nchini Uingereza. Baada ya watu na baadhi ya vyombo vya habari vya Bongo kukiongelea na wengine kukiponda sana kimombo alichotema nyota mashuhuri wa Filamu za Bongo, Steven Kanumba wakati alipoalikwa kwenye Big Brother nchini Afrika Kusini, mwanadada Sporah Njau, mbongo anayeendesha shoo yake inayojulikana Sporah Show nchini Uingereza ametoa video hizi kuonyesha kwamba Kanumba hajachooka kiiivyo kwenye kutema ngeli kama alivyoongelewa na wabongo.

  Sporah ametoa video za wasanii wa Bongo kama vile Ay, Mwana FA, Ali Kiba pamoja na Kanumba mwenyewe ambao aliwaalika kwenye shoo yake jijini London wakati walipofanya ziara zao za kisanii nchini Uingereza.

  Ali Kiba hakutaka tabu aliamua kuongea kiswahili kuepusha wadau msimnange sana na kiinglish chake.

  Angalia video hizo chini.

  Baada ya kuangalia video usikose kukipigia kura kipindi cha Sporah Show ambacho muandaaji wake Sporah Njau amechaguliwa kuwa mmoja wa watakaowania tuzo ya Best TV Presenter katika tuzo za BEFFTA Awards za nchini Uingereza ambazo hutolewa kwa watu weusi wanaotamba kwenye fani mbali mbali za muziki, filamu na fani nyinginezo kibao.

  Kumpigia kura Sporah click link hii chini, baada ya kuandika jina na email yako nenda kwenye kijumba cha Category chagua Best TV Presenter halafu nenda kwenye kijumba cha chini cha Nominee mchague Sporah Njau. GONGA HAPA KUMPIGIA KURA SPORAH

  VIDEO - Kanumba akilalamika jinsi wabongo wanavyomsema vibaya kwa sababu ya kimombo chake


  VIDEO - Kanumba akitema ngeli nchini Uingereza Part I


  VIDEO - Kanumba akitema ngeli nchini Uingereza PART II


  VIDEO - Kanumba akitema ngeli nchini Uingereza Part III


  VIDEO - Mwana FA na AY wakitema ngeli nchini Uingereza


  VIDEO - Ali Kiba hakutaka tabu aliamua kutema kiswahili nchini Uingereza


  Video zake ziko chini
   
  Last edited: Sep 23, 2009
 2. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #2
  Sep 23, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Mmhm.. Mbona hakuna links yoyote ya video hapo?
   
 3. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #3
  Sep 23, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #4
  Sep 23, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  [video=youtube;4p2QYLlpdP4]http://www.youtube.com/watch?v=4p2QYLlpdP4[/video]
   
 5. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #5
  Sep 23, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  [ame="http://www.youtube.com/watch?v=kgSqhBi-DLc"]Sporah Show - AY & Mwana FA[/ame]
   
 6. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #6
  Sep 23, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #7
  Sep 23, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #8
  Sep 23, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Nimekuwekea hapo juu kaka umeziona?
   
 9. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #9
  Sep 23, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Tusiwakatishe tamaa wasanii wetu. Tuwapeni moyo hata kama wanafanya vibaya,hata kama hawaongei vizuri kimombo tusiwakatishe tamaa.
   
 10. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #10
  Sep 23, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Samahani Moderator, nimezichanganya parts za Sporah na Kanumba kama kuna uwezekano naomba unipangie vizuri ukianzia na Part 1,2,3 ili ziwe na mpangilio mzuri,kwani huwezi anzia part 3 ukamalizia na part 1. Natanguliza shukurani. Nimeziweka hapa kwa makusudi makubwa ili tuendelee kuwapa moyo wasanii wetu si kuwakatisha tamaa.
   
 11. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #11
  Sep 23, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  !!!!!????
   
 12. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #12
  Sep 23, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Ndio nini, sema usikike.
   
 13. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #13
  Sep 23, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Naam Kamanda! Naendelea kuziangalia...:D
   
 14. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #14
  Sep 23, 2009
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Enzi hizo tulipo kuwa form 3 walikuwapo mabingwa wa Kiswahili cha kuongea na kuandika. Cha ajabu sikuona mtu akichekwa kwa vile kiswahili chake ni nyanya.
  Ni ajabu sana kuona watu na shule zetu tunacheka wasanii wanaojieeleza kwa kiingereza cha kusuasua.
  Kiingereza siyo lugha rasmi ya mawasiliano Tanzania, Kiingereza ni lugha tunayo lazimika kuongea pale tutakapo pata elimu ya juu au katika biashara.
  Kwa wastani wasanii hawa wanaongea kiingereza average kwa watanzania wa kawaida na hata wale walo kaa UK na US kwa muda mrefu na kuishia kujifunza kiingereza cha matusi na kile cha mitaani.
   
 15. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #15
  Sep 23, 2009
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,164
  Trophy Points: 280
  ni kweli,halafu mbona poa tu wameeleweka kabisa,naona kanumba kule south alichachawa tu lakini kingereza chake wala si kibaya kiivyo
   
 16. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #16
  Sep 23, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Madela Wa- Madilu,
  Kaka nimekusikia na kukuelewa na kukusoma vizuri sana, hicho ndicho watu wanatakiwa kuelewa na sio kuwakatisha tamaa hawa wasanii wachanga ambao bado wanahitaji malezi yetu na msaada wetu ili waweze kufikia malengo waliojiwekea kwa faida yao na Taifa kwa ujumla.
   
 17. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #17
  Sep 23, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Kwa kweli amejitahidi sana,kaeleweka na kaongea kwa kujiamini. Iddi Amini alikuwa na kiinglish cha ajabu lakini alieleweka mbele ya madaktari, mikutano ya kimataifa na wananchi wake.
   
 18. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #18
  Sep 23, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Acheni kumdekeza Kanumba.

  Kanumba wee Ngosha acha kulialia uonewe huruma.

  Nenda kafanye hizo KOZI hasa kuongea na amini nakuambia kila sehemu utakayofika, hutahitaji kujichekeshachekesha na kusema YOU KNOW nyingi. Unafahamu Kiingereza siyo siri ila hujafanya maongezi mengi ya Kuongea. Tafuta shule na zipo kibao au hata waalimu wa kukufundisha watakufuata hata kwako so longer you pay them.

  Muone huyu dada, tena alikuwa binti mdogo saana wakati anafanya maajabu haya. Kilikuwa hakifahamu kabisa Kiingereza maana kinatoka Canada ya Wafaransa. Alijifungia ndani miaka miwili na alipotoka, huwezi amini alikuwa hafahamu KABISAA English. Kanumba na wenzako, tafuteni shule mpate mazoezi ya kuongea. Wengine nao watafaidika kupata kazi na nyinyi mtaweza kuimba, kuongea kwa Kiingereza kama Waingereza wenyewe. Kila kitu chawezekana dunia ya leo kama mna nia.

  [ame]http://www.youtube.com/watch?v=Nk6LV5pC13Q[/ame]
   
 19. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #19
  Sep 24, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Kaka hapo pekundu hahitaji kuwa kama mwingereza wakati yeye ni Mtanzania,hapo umekosea. Marais wa Ufaransa,Libya,Russia,China na wengineo wametumia Lugha zao ku address U.N GENERAL ASSEMBLY kwa lugha zao na nahisi kuna wengine hata kiingereza hakipandi lakini hakuna aliyewazomea au kuwaambia kwa nini wasiwe kama Waingereza?. Jivunie Lugha yako mengine ya baadae
   
 20. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #20
  Sep 24, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Ng'wanza, hebu acha kuchemsha Ngwana Madaso. Ufaransa ni lugha inayojitegemea kama Kiingereza (International). Russian ni lugha mashuhuri sana duniani hata Tanzania utapata watu wengi tu wanaongea. Kichina inatosha kufahamu kuwa Wachina ni wengi sana duniani na Rais wa China alisoma Urusi na anaongea Kirusi. Rais wa Urusi mwenyewe anaongea Kiingereza. Putin ndiyo wacha maana Shushushu lile linatema Kijeruman, Kifaransa na English. Ghadaffi alimwaga Kiarabu na hii nayo ni lugha yakimataifa. Hata Kiswahili ni lugha ya Kimataifa maana ndiyo lugha ya Africa Union kama kilivyo Kiingereza kwa EU.

  Haya mambo ya kulinganisha Kanumba na Marais ntakuelezea kisa kimoja. Nilishawahi kukutana na mkurugenzi wa Citibank nikiwa nchi za watu miaka ya 90. Huyu jamaa kutoka Congo Kinshasa, alikuwa akiongea English kwa sababu alisomea USA, France, Lingala, Swahili na kwa sababu alienda kufanya kazi Brazil kwa miaka 7 na kazi za chini, ilibidi ajifunze ki-Portugal. Baadaye akaja Spain kwa miaka kibaa na Kispnish kikaiba kiPortugal chote. Ila baada ya kuwa kafanya kazi kwa miaka mingi akawa amepanda sana hadi kuwa Mkurugenzi wakati mie nimekutana naye. Huwezi amini kuwa jamaa alikuwa akiongea Kiingereza tu pale kazini na kama wewe humuelewi basi acha kazi CitiBank. Na hiyo nchi haikuwa ya Kiingereza.
  Kanumba na hawa wengine, kama wanataka kujipanua KIKAZI basi lazima walau wafahamu Kiingereza. Itakuwa vema wakiongeza na Kifaransa. Wakija kuwa na majina basi wanaweza hata kudeka wakati wakipokea OSCAR kuwa "Mie ntaongea Kisukuma/Kiswahili maana huwa nafikiri Kiswahili".
   
Loading...