Naona mnajiropokea tu kwa chuki zenu dhidi ya Uislam, Zanzibar watu hawajakatazwa kula mchana wala kulazimishwa kufunga. Hata baadhi ya Waislam huwa hawafungi kama vile wanawake walio kwenye siku zao, wagonjwa, vikongwe nk kilichokatazwa ni kula hadharani ambapo jamii vya Zanzibar kwa zaidi ya 95% ni Waislamu, hivyo ni suala la kuheshimu na kutowafanyia karaha waliofunga. Watalii ni wengi sana Zanzibar na wanalizingatia hili kwa unyenyekevu tu, wanakula vizuri tu wakiwa mahotelini mwao. Tatizo ni mabaradhuli wachache, hasa wa kutoka Tanganyika, wanawafanyia dharau na kejeli wenzao waliofunga, hao lazima wachezee mbati tu, na nyie mabaradhuli mnaojiropokea tu mitandaoni nendeni kule halafu mkiuke taratibu zao walizojiwekea kisha muone mtakavyofanywa, mtaishia kuroroma tu mitandaoni!
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.