Video: Ukienda Zanzibar lazima unyooke, sio kula kula ovyo, jamaa achezea kichapo...hehehe

Hizi imani zakulamishana sasa, hivi kwani kutokula ndio inaleta maana ya kufunga au kufunga ni kuacha dhambi na maombi kufanyika kwa sana?

Na hao walio mpiga funga yao itafika kwa mungu? Au wao hawaja funga ? na kama hawaja funga mbona hawaja pigwa?
 
sina hakika kama uislamu ni dini ya kweli?
dini gani ya kulazimishana eti wewe ukifunga unataka wote uwalazimishe wafunge.
 
Ukiona umefunga halafu ukiona mtu anapita akila chakula unawake hasira na kumjeruhi kwa kipigo basi jua umeshinda njaa tu hakuna mfungo wa kweli hapo.
Hehehe nimecheka sana.
 
Naona mnajiropokea tu kwa chuki zenu dhidi ya Uislam, Zanzibar watu hawajakatazwa kula mchana wala kulazimishwa kufunga. Hata baadhi ya Waislam huwa hawafungi kama vile wanawake walio kwenye siku zao, wagonjwa, vikongwe nk kilichokatazwa ni kula hadharani ambapo jamii vya Zanzibar kwa zaidi ya 95% ni Waislamu, hivyo ni suala la kuheshimu na kutowafanyia karaha waliofunga. Watalii ni wengi sana Zanzibar na wanalizingatia hili kwa unyenyekevu tu, wanakula vizuri tu wakiwa mahotelini mwao. Tatizo ni mabaradhuli wachache, hasa wa kutoka Tanganyika, wanawafanyia dharau na kejeli wenzao waliofunga, hao lazima wachezee mbati tu, na nyie mabaradhuli mnaojiropokea tu mitandaoni nendeni kule halafu mkiuke taratibu zao walizojiwekea kisha muone mtakavyofanywa, mtaishia kuroroma tu mitandaoni!
 
Back
Top Bottom