VIDEO - Ukatili wa Wapishi wa China

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,293
33,078
VIDEO - Ukatili wa Wapishi wa China
3572586.jpg

Samaki Akaangwa akiwa hai, Aliwa akiwa hai Thursday, November 19, 2009 2:06 AM
Samaki siku zote hukaangwa kwa kutumia mafuta yaliyochemka sana na haiingii akilini kuwa samaki anaweza kukaangwa kwenye mafuta ya moto na akaendelea kuwa hai, lakini wataalamu wa mapishi wa China wanaweza kufanya hivyo, amini usiamini. Wataalamu wa mapishi wa China wamevumbua staili ya kukaanga samaki walio hai na kuwatenga mezani wakiwa wameiva tayari kwa kuliwa lakini bado wakiwa hai.

Hata hivyo staili hiyo ya mapishi imeonekana kuwa ya kikatili sana kwani samaki huwekwa kwenye mafuta ya moto nusu ya mwili wake lakini kichwa chake hakiingizwi kwenye mafuta na huachwa kwenye unyevu unyevu ili aweze kuendelea kuishi.

Samaki anapoiva hutengwa kwenye sahani tayari kuliwa lakini hadi wakati huo huwa bado yupo hai na huweza kuchezesha mapezi yake na mdomo wake.

Video ya tukio hilo ambalo ni gumu kuamini imewekwa kwenye YouTube ikimuonyesha samaki aliyekaangwa nusu ya mwili wake akiwa bado yupo hai. Video hiyo imetazamwa na maelfu ya watu tangia ilipowekwa kwenye YouTube siku chache zilizopita.

Video hiyo imesababisha malalamiko ya watu wengi kwa ukatili wa wapishi wa China wanaoufanya kwa samaki kwa kuwaakaanga wakiwa hai na kuwala wakiwa hai.

Ni watu wachache wenye mioyo migumu ndio walioweza kuonja ladha ya minofu ya samaki huyo aliyekaangwa akiwa hai.

Chini ni Video hiyo ya samaki aliyekaangwa akiwa hai na kuliwa akiwa hai.


VIDEO - Samaki Akaangwa akiwa hai, Aliwa akiwa hai Bonyeza hapa chini kuiona video http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3572586&&Cat=2
 
Back
Top Bottom