Tundu Lissu ataka Rais Magufuli asusiwe kila mahali na mataifa mengine duniani

Tukisubiri mh Magufuli awagaragaze kwa mara nyingine Chadema mwaka 2020 kumekuwa na vita vya chini kwa chini kati ya wagombea watarajiwa wa Chadema yaani Tundu lissu na Edward lowassa.

Vita hii inaendeshwa kwa mwendo wa matamko kati ya hawa wagombea wawili.

Bado hakuna mgombea aliyetoa tamko la kumkandia au kumpinga mwenzake lakini kwa maoni yangu matamko ya namna hiyo yatakuja kadri muda unavyojiri.

Kwa upande wa lowassa matamko yake yanakuwa ni ya kujihakikishia nafasi ndani ya Chadema...huku Tundu lissu akija na matamko yasiyotaka kuvunja katiba na vigezo vya chama chake.

Inaelekea kamanda lissu pamoja na visa vyake akawa muwakilishi wa Chadema asili huku Lowasa akiiwakilisha timu katwa a.k.a timu ya Ulipo tupo inayotaka kuiteka chadema.

Tuendelee kushuhuduia mpambano huu wa KUNGURU MWOGA!
 
CHADEMA wasipokuwa makini wataishiwa kususiwa wao na Watanzania.

Tanzania haijafikia kabisa viwango vya kususiwa na jumuia ya kimataifa.
Ili ifikie kususiwa inatakiwa iweje na inafikaje huko. Huwa inaanza ghafla ama hatua kwa hatua. Halafu unamaanisha watanzania wanataka vyama vingine vizuiwe kufanya siasa na CCM pekee ndiyo iwe inafanya siasa?

Unadhani ni sahihi kwa rais kutumia fedha bila ya kuidhinishwa na bunge na ni sahihi pia kujenga miundo mbinu kwa kutumia fedha za umma atakavyo? Umenikumbusha ule waraka wa serikali "unaozuia" wafanyakazi wa umma kufanya siasa lakini ni kwa wale wanaoipinga serikali. Maana yake wanaoiunga mkono serikali ni ruksa kufanya siasa.
 
Nakushauri lisu chagua maneno ya kuongea vinginevyo jamii nzima itakuona bwege. Kumbuka ukikosona na kanisa katoloki unajiua mwenyewe kisiasa na kijamii. Lowasa alikosa kula hasa baada ya kumshambulia pengo. Lile kanisa achana nalo kabisa lina misingi mathubuti linaweza kujiendesha lenyewe bila hata uwepo Wa serikali.

Unaona jk alivyowekwa kati hasa baadae ya kuoneaha upendeleo wake kwa waislam. Alimaliza utawala wake kwa shida sana na angeendelea angejiudhuru tu
Kama halina ukweli hilo swala, atakuwa amekosea lakini kama lina ukweli sioni tatizo.
 
T
Lengo hasa la huyu mtu kuongea na media lilikuwa ni nini hasa ?

- Kujenga uwanja chato ?
- Uwepo wa ndugu wa Magufuli serikalini ?
- Ukabila ?
- Demokrasia ?
- Kuhamasisha jumuiya za kimataifa zimsusie Magu ?
- Kaimu Jaji Mkuu ?

Binafsi naona mkanyanyiko na mrundikano wa mada kibao sehemu moja
Kuwaonyesha watanzania udikteta na ukabila na undugunaizesheni wa awamu ya 5
 
CHADEMA wasipokuwa makini wataishiwa kususiwa wao na Watanzania.

Tanzania haijafikia kabisa viwango vya kususiwa na jumuia ya kimataifa.

Sasa huyu so called 'msomi' ndo anataka nchi isusiwe?

Kwa minajili gani hasa?

Mtu yupo Tanzania na ana uhuru wa kumzungumzia hivyo rais aliyepo madarakani halafu anataka nchi isusiwe?

Hata hiyo jumuia ya kimataifa ikimsikia itamcheka kwa dharau nyingi sana.

Huyu jamaa mdomo wake hauna breki!

He is a demagogue on steroids!
Hana maana hajui kuwa heshima yake inashuka kila uchao. Sijajua matamko ya Lissu ni yake mwenyewe au ni ya CHADEMA. Kama ni ya CHADEMA basi watafakari sana kila tamko wanalolitoa mwisho chama kitabaki na mwenyekiti na huyo so called mwanasheria msomi.
 
Nakushauri lisu chagua maneno ya kuongea vinginevyo jamii nzima itakuona bwege. Kumbuka ukikosona na kanisa katoloki unajiua mwenyewe kisiasa na kijamii. Lowasa alikosa kula hasa baada ya kumshambulia pengo. Lile kanisa achana nalo kabisa lina misingi mathubuti linaweza kujiendesha lenyewe bila hata uwepo Wa serikali.

Unaona jk alivyowekwa kati hasa baadae ya kuoneaha upendeleo wake kwa waislam. Alimaliza utawala wake kwa shida sana na angeendelea angejiudhuru tu
Hakuna anaemaliza Ikulu kwa shida wewe, mbona hicho kikundi chenu cha kula nguruwe hakikumtoa mpaka amemaliza kwa mujibu wa katiba.
Na bwana wenu sasahivi anatibiwa na waarabu Dubai.
 
Yanamsusia Magufuli au anataka watanzanua wasusiwe? Ana roho mbaya huyu anafikiri Rais ana shida au ni wananchi halafu jimbo lake huyu ni Magogoni anapambana na ikulu hatari Singida mara chache sana

Lissu kaongea ukweli, watu watz wanaumizwa hakuna wa kuwasemea. Safi sana lisu mpe za kweli.
 
Mbunge wa Singida Mashariki amefanya mkutano na waandishi wa habari akimtuhumu Magufuli kwa mambo mengi na kutaka asusiwe kila mahali.

Amesema mataifa ya nje yanayompa hela Magufuli yamsusie Magufuli na kutompa pesa za kuikandamiza Tanzania. Kujenga uwanja wa ndege Chato ni kama Mobutu Seseseko alivyojenga kijijini kwao.

Amesema Mwinyi na wengine wanaotaka Magufuli aongoze miaka zaidi ya 10 wanataka Magufuli awe kama rafiki zake Nkurunziza, Kagame na Joseph Kabila na kuita huo ni ujinga. Wanaoshangilia Bombardier hawajui zimenunuliwaje na Magufuli anaendesha nchi kwa misingi ya kikabila na Kifamilia, akimtolea mfano Dotto James Katibu Mkuu wizara ya fedha na Naibu wake ni watoto wa dada alikuwa afisa ngazi za chini wa TANROADS miaka 2 iliyopita na wanaambiana mjomba tununue ndege, tujenge uwanja wa ndege nyumbani na hela zinatoka.

Mmoja wa wanasheria wa wizara mmoja Medad Kalemani na Naibu Waziri nishati na madini hakufukuzwa kwenye skendo ya madini iliyomuondoa Muhongo. Kuingilia uhuru wa mahakama. Anawaambia majaji kwenye mikutano ya hadhara namna ya kutoa hukumu.

Sasa ni mwezi wa 8 mahakama ya Tanzania haina Jaji mkuu ina Kaimu jaji mkuu na hii haijawahi kutokea Magufuli anajiona yeye ndio dola kwenye karne ya 21. Majaji wa mahakama kuu 4 kujiuzulu ndani ya miezi 3 haijawahi kutokea na sababu wala maelezo hayatolewi japo kuna baadhi yao walihusika na Escrow ila haijatolewa sababu

Kama majaji wanalazimishwa kujiuzulu bila maelezo nani yupo salama?
Vyombo vya habari vinavamiwa kwa bunduki na hakuna hatua inayochukuliwa
Tunaposema udikteta ndio huu. Kazi ya kupinga udikteta sio ya CHADEMA tu, ni vyombo vya habari, wafanyakazi wa serikali viongozi wa dini. Kutumia vibaya fedha na rasilimali za taifa.

Nimeisikiliza clip mwanzo mpaka mwisho na binafsi sioni jipya zaidi ya kuwa malalamiko haya ni kama yamerasimishwa kuliko ilivyokuwa mwanzoni ambapo yalikuwa yakiongelewa chinichini.
Naamini Mheshimiwa Rais ana sababu za kufanya yote aliyoyafanya pia serikali ina majibu kwa hoja za Lissu kwa hivyo ni bora tusubiri response ya serikali kwa haya aliyoyataamka TL.

Jambo moja ni dhahiri, Lissu kajilipua. Amejiamini kitu gani, SIJUI!!
 
Back
Top Bottom