Tundu Lissu ataka Rais Magufuli asusiwe kila mahali na mataifa mengine duniani

Siasa za Tanzania haziendi bila unafiki bibie! Magufuli huyuhuyu alizisifia safari za nje za Kikwete. Nakumbuka Magufuli alisimama Bungeni na kushupaza misuri kuzitetea safari hizo na kumwomba Kikwete asafiri zaidi ili ailetee nchi mapesa! Nafikiri sina haja ya kukuambia nini alisema baada ya kuwa Rais.

Pia CCM hawa hawa walishupaza misuri ya shingo kusema Lowassa siyo fisadi. Hadi Kikwete alikwenda kumfanyia kampeni ya Ubunge kule Monduli! Nape akaanzisha kampeni ya kuvua magamba, huku mwanzoni akisema Lowassa ni moja ya magamba hayo! Mwishowe wake unaufahamu.

Na mwisho, Magufuli anajipambanunua kama anapiga vita ufisadi! Sasa ni nini kinamzuia kumfungulia mashtaka fisadi Lowassa? Si hadi ilianzishwa Mahakama ya mafisadi? Mbona Mahakama inakosa wateja wakati kila kukicha Magufuli analalamika juu ya nchi hii kuliwa na kuchezewa sana (yeye mwenyewe alishiriki katika kuila na kuichezea); yaani analalamika kama mwananchi wa kawaida!!

Lowassa, Sumaye, Mkapa na Kikwete na viongozi waandamizi wengi waliopo na waliopita wa serikali ya CCM wanapaswa kuwa wamefikishwa Mahakama ya mafisadi!
Naheshimu maoni yako, ila hainiondolei ukweli kua Lisu si mzalendo kama wengi wanavyomsifia na kumpamba tena anayetaka inchi yangu itengwe hapana kwakweli amenitoka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wafia wa Katundu kalissu awatakuelewa mkuu, yeye mwenyewe kasahau alivyomsajiri marehemu dada yake ubunge wa viti maalum pale Chadema. Au anajua watanzania wasahulifu?

Uyu ana moral na ujasiri wa kusema ukabila na ukanda wakati chama chake ndio magwiji ya haya mambo, angeanza kukisafisha chama chake kwanza ndio angeeleweka. Ama kweli nyani haoni kundule.

Mwisho naomba kumuuliza Katundu kalissu kama kajisahulisha ili Lucy Awenya ni mtoto wa marehemu mzee Ndesamburo, Mukya ni Hawara wa mwenyekiti wake,Komu na Yule mama Komu na Salim Mwalimu ni ndugu anabisha? Kubenea kaingiza usajiri wake, na Ally Bananga diwani sombetini mkewe yupo viti maalum pale mjengoni.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ata mimi nimejiuliza haya maswali hadi nimechoka yaani mtu anapataje ujasiri wa kumnyooshea kidole mwenziwe wakati huko kwao kuanzia yule DJ wake hadi mtu wa mwisho wanamakando ata hayawezi kuzungumzwa hapa jamvini. TL asijione ana akili kuliko waTanzania wote anaweza kuwa anaakili kuliko CDM wote but sio wa Tz wote.
 
Uza huo ubongo ww unakaa nao kwa hasara. Akina Masamaki tuliambiwa ni majizi, mbona wote wameachiwa tena kwa serekali kusema haina haja ya kuendelea na kesi?

Unajuaje pengine kuna mkono wa mtu mkubwa kushinda Magufuli. . Huwezi kuwa na nyumba 75 mtumishi wa serikali, HUYU lazima alikuwa na connection.. kesi ya contsiner 200 iliishia wapi? Hujui kama kuna vitisho gani kwa Rais Magufuli kusema atawalinda MARAIS wa zamani ambao kila mala wanamkumbusha walimteuwa. Turudi nyuma, Watanzania hatuna choice, kwenye upinzani kuna watu wachache sana wenye nguvu za kuleta mabadiliko. Unaamini Lowassa anaweza kuleta mabadiliko kwenye Nchi hii? Alivyo dhaifu na historia ya ufisadi aliyonayo. Ni tajiri mkubwa, hana kiwanda, alijipatiaje Utajiri? Kuna mambo mengi yanawaudhi Watanzania wengi anayoyafanya Rais Magufuli, kutokufuata sheria, na mawazo yake ya kutokuona mbali, lakini what alternative do we have?
 
Mbunge wa Singida Mashariki amefanya mkutano na waandishi wa habari akimtuhumu Magufuli kwa mambo mengi na kutaka asusiwe kila mahali.

Amesema mataifa ya nje yanayompa hela Magufuli yamsusie Magufuli na kutompa pesa za kuikandamiza Tanzania. Kujenga uwanja wa ndege Chato ni kama Mobutu Seseseko alivyojenga kijijini kwao.

Amesema Mwinyi na wengine wanaotaka Magufuli aongoze miaka zaidi ya 10 wanataka Magufuli awe kama rafiki zake Nkurunziza, Kagame na Joseph Kabila na kuita huo ni ujinga. Wanaoshangilia Bombardier hawajui zimenunuliwaje na Magufuli anaendesha nchi kwa misingi ya kikabila na Kifamilia, akimtolea mfano Dotto James Katibu Mkuu wizara ya fedha na Naibu wake ni watoto wa dada alikuwa afisa ngazi za chini wa TANROADS miaka 2 iliyopita na wanaambiana mjomba tununue ndege, tujenge uwanja wa ndege nyumbani na hela zinatoka.

Mmoja wa wanasheria wa wizara mmoja Medad Kalemani na Naibu Waziri nishati na madini hakufukuzwa kwenye skendo ya madini iliyomuondoa Muhongo. Kuingilia uhuru wa mahakama. Anawaambia majaji kwenye mikutano ya hadhara namna ya kutoa hukumu.

Sasa ni mwezi wa 8 mahakama ya Tanzania haina Jaji mkuu ina Kaimu jaji mkuu na hii haijawahi kutokea Magufuli anajiona yeye ndio dola kwenye karne ya 21. Majaji wa mahakama kuu 4 kujiuzulu ndani ya miezi 3 haijawahi kutokea na sababu wala maelezo hayatolewi japo kuna baadhi yao walihusika na Escrow ila haijatolewa sababu

Kama majaji wanalazimishwa kujiuzulu bila maelezo nani yupo salama?
Vyombo vya habari vinavamiwa kwa bunduki na hakuna hatua inayochukuliwa
Tunaposema udikteta ndio huu. Kazi ya kupinga udikteta sio ya CHADEMA tu, ni vyombo vya habari, wafanyakazi wa serikali viongozi wa dini. Kutumia vibaya fedha na rasilimali za taifa.



Edit kichwa cha habari andika wanaCCM wamjia juu Lissu,kwani watanzania tunampongeza Lissu kwa kusema ukweli bila kuficha
 
Katika mijitu isiyo na akili ya maisha ni Tundu Lissu,ulitaka uwanja wa ndege ujengwe Dar? Kwani Chato hakuna watanzania wanaishi? Tundu Lissu unaishi kwa mastress ya kujitafutia kila siku. Kwani wewe nani hadi mataifa ya kigeni yakutii? Vipi kwani ile kesi yenu kule ICC iliishia wapi? Tupe kwanza majibu ya hiyo kesi ndo uteleze mambo mengine vinginevyo inabidi ukapimwe akili wewe si mzima...!!
 
Sasa huyu mzee wa Singida kachanganyikiwa. Yaani ameshindwa kuwashawishi waTZ wamchukie rais wao sasa anataka wananchi wa mataifa mengine wamsusie!

Post sent using JamiiForums mobile app
LAZIMA KUWE NA SPIDI GAVANA PAHALA, TUNDU ANASAIDIA KUIWEKA. SAFI
 
Kuna vitu vichache mzee akibadili video hii itakosa pakushikia, ila sauti hii ikidharauliwa ni hatari.
 
Katiba ishasema ni mihula miwili tu
Naona kuna watu wanalipwa pesa na ccm chini kwa chini ili kutoa matamko ya kidkiteta. ya kumwambia mtawala atawale milele
Kuna kampeni imeanzishwa inaitwa baki ******** ambayo inafadhiliwa na chama cha mapinduzi chini ya bwana yule
Hatutaruhusu nchi kuingia kwenye udikteta kama huu wa sasa hivi
Si walisema mikutano ya hadhara ni marufuku? Sasa imekuaje tena?
Operesheni yoyote itakayotangazwa na upinzani nitaunga mkono kwa nguvu zote
Ni mpumbavu tu ndo atakubali kutawaliwa kidkteta na kimabavu
Mpaka sasa hivi ni lipi limefanyika maendeleo yapi? Labda chato
Nawaomba sana viongozi wa upinzani awamu hii tusilogwe wala kukubali huyu mtu aachwe tena naomba itangazwe operesheni ya kumn'goa madarakani kisheria
Hatugopi chochote alimradi tusivunje sheria tu
[HASHTAG]#Hatutaki[/HASHTAG] [HASHTAG]#udikteta[/HASHTAG] [HASHTAG]#wako[/HASHTAG]
 
Shida wa Tz Tuna Piga Sana Kelele Katika Mitandao Ila Linapo Kuja Swala La Kupinga Kitu Kwa Maandamano Hakuna Hata Mmoja Wa Kusubutu
 
Kweli hili ni VUVUZELA alichokiongea hapo hafananii na uwezo wa elimu aliyonayo. Nenda jimboni kwako ukashughulikie shida za wananchi wa jimboni kwako. Sasa muda wa kuropoka ulishapita.
 
69 Reactions
Reply
Back
Top Bottom