VIDEO: Tundu Lissu ataka Rais Magufuli asusiwe kila mahali na mataifa mengine duniani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

VIDEO: Tundu Lissu ataka Rais Magufuli asusiwe kila mahali na mataifa mengine duniani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by DEMBA, Jul 17, 2017.

 1. DEMBA

  DEMBA JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2017
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 8,022
  Likes Received: 4,217
  Trophy Points: 280
  Mbunge wa Singida Mashariki amefanya mkutano na waandishi wa habari akimtuhumu Magufuli kwa mambo mengi na kutaka asusiwe kila mahali.

  Amesema mataifa ya nje yanayompa hela Magufuli yamsusie Magufuli na kutompa pesa za kuikandamiza Tanzania. Kujenga uwanja wa ndege Chato ni kama Mobutu Seseseko alivyojenga kijijini kwao.

  Amesema Mwinyi na wengine wanaotaka Magufuli aongoze miaka zaidi ya 10 wanataka Magufuli awe kama rafiki zake Nkurunziza, Kagame na Joseph Kabila na kuita huo ni ujinga. Wanaoshangilia Bombardier hawajui zimenunuliwaje na Magufuli anaendesha nchi kwa misingi ya kikabila na Kifamilia, akimtolea mfano Dotto James Katibu Mkuu wizara ya fedha na Naibu wake ni watoto wa dada alikuwa afisa ngazi za chini wa TANROADS miaka 2 iliyopita na wanaambiana mjomba tununue ndege, tujenge uwanja wa ndege nyumbani na hela zinatoka.

  Mmoja wa wanasheria wa wizara mmoja Medad Kalemani na Naibu Waziri nishati na madini hakufukuzwa kwenye skendo ya madini iliyomuondoa Muhongo. Kuingilia uhuru wa mahakama. Anawaambia majaji kwenye mikutano ya hadhara namna ya kutoa hukumu.

  Sasa ni mwezi wa 8 mahakama ya Tanzania haina Jaji mkuu ina Kaimu jaji mkuu na hii haijawahi kutokea Magufuli anajiona yeye ndio dola kwenye karne ya 21. Majaji wa mahakama kuu 4 kujiuzulu ndani ya miezi 3 haijawahi kutokea na sababu wala maelezo hayatolewi japo kuna baadhi yao walihusika na Escrow ila haijatolewa sababu

  Kama majaji wanalazimishwa kujiuzulu bila maelezo nani yupo salama?
  Vyombo vya habari vinavamiwa kwa bunduki na hakuna hatua inayochukuliwa
  Tunaposema udikteta ndio huu. Kazi ya kupinga udikteta sio ya CHADEMA tu, ni vyombo vya habari, wafanyakazi wa serikali viongozi wa dini. Kutumia vibaya fedha na rasilimali za taifa.  Kwa Mwendelezo wa habari soma=Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu akamatwa akiwa uwanja wa ndege wa Dar akielekea Kigali
   
 2. U

  UCD JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2017
  Joined: Aug 17, 2012
  Messages: 3,045
  Likes Received: 2,034
  Trophy Points: 280
  Vuvuzela huyu tumemzoea. Hata kwenye makinikia alisema tutanyolewa bila wembe na wenye makinikia badala yake wakapanda ndege kuja kuomba tuongee!! Sasa anatafuta kick nyingine kama anataka tususiwe na mataifa si angewafuata hukohuko hao mabwana zake??
   
 3. Akasankara

  Akasankara JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2017
  Joined: Feb 28, 2015
  Messages: 1,784
  Likes Received: 1,828
  Trophy Points: 280
  Nchi inaendeshwa bila weledi, masikini wanapata tabu na hawajuwi wamlilie nani
   
 4. Akasankara

  Akasankara JF-Expert Member

  #4
  Jul 17, 2017
  Joined: Feb 28, 2015
  Messages: 1,784
  Likes Received: 1,828
  Trophy Points: 280
  Watumishi wa umma wamebaki mayatima
   
 5. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #5
  Jul 17, 2017
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 22,486
  Likes Received: 13,700
  Trophy Points: 280
  Hajaongelea kuhusu MIGA?

  Tanzania ni nchi huru...hata ikisusiwa na dunia nzima bado tutasimama kama nchi.

  So let him shut up and live!
   
 6. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #6
  Jul 17, 2017
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,672
  Likes Received: 1,617
  Trophy Points: 280
  Kwa namna ipi ?
   
 7. Freeland

  Freeland JF-Expert Member

  #7
  Jul 17, 2017
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 14,464
  Likes Received: 6,765
  Trophy Points: 280
  safi sana Lissu

  Singida safi sana
   
 8. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #8
  Jul 17, 2017
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,859
  Likes Received: 3,116
  Trophy Points: 280
  Hivi Mkuu bado yuko likizo ........ naona Lisu anamhalibia mapumziko wake!!
   
 9. M

  Meela JF-Expert Member

  #9
  Jul 17, 2017
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,017
  Likes Received: 512
  Trophy Points: 280
  Sasa huyu mzee wa Singida kachanganyikiwa. Yaani ameshindwa kuwashawishi waTZ wamchukie rais wao sasa anataka wananchi wa mataifa mengine wamsusie!

  Post sent using JamiiForums mobile app
   
 10. MoseKing

  MoseKing JF-Expert Member

  #10
  Jul 17, 2017
  Joined: Jul 5, 2017
  Messages: 646
  Likes Received: 650
  Trophy Points: 180
  Vipi kuhusu kumpeleka MAGU Mahakamani kumteua Jaji Mkuu na Makonda?
   
 11. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #11
  Jul 17, 2017
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 22,486
  Likes Received: 13,700
  Trophy Points: 280
  Mzee wa MIGA anatafuta kiki ya msimu ili kucounter tamko la lowassa!
   
 12. swissme

  swissme JF-Expert Member

  #12
  Jul 17, 2017
  Joined: Aug 15, 2013
  Messages: 13,040
  Likes Received: 16,595
  Trophy Points: 280
  Lissu my next president.


  Swissme
   
 13. KING DUBU

  KING DUBU JF-Expert Member

  #13
  Jul 17, 2017
  Joined: Mar 7, 2017
  Messages: 817
  Likes Received: 1,040
  Trophy Points: 180
  Wananchi Hali ngumu mazezeta wa chama kile wanabwabwaja wakati uhalisia wanauona. Huyu mzee huyu..... Nje anacheka ila ndani bonge la snichi.
   
 14. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #14
  Jul 17, 2017
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,672
  Likes Received: 1,617
  Trophy Points: 280
  Mkuu ungejibu hoja zake walau ningekuelewa ,kama ni debe tupu basi utusaidie huo u'debe tupu wake tuujue na sisi tusio ufaham
   
 15. KikulachoChako

  KikulachoChako JF-Expert Member

  #15
  Jul 17, 2017
  Joined: Jul 21, 2013
  Messages: 14,432
  Likes Received: 12,462
  Trophy Points: 280
  Wakati mwingine huwa nashindwa kumuelewa Tundu Lissu mantiki za hoja zake.....lakini naheshimu maoni yake kama ambavyo katiba inamruhusu......
   
 16. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #16
  Jul 17, 2017
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 44,428
  Likes Received: 14,078
  Trophy Points: 280
  hahahahah vipi atwambie kwanza walifikia wapi kutomtambua Magufuli?
   
 17. tindo

  tindo JF-Expert Member

  #17
  Jul 17, 2017
  Joined: Sep 28, 2011
  Messages: 11,237
  Likes Received: 12,161
  Trophy Points: 280
  Mkuu kwani anapendwa?
   
 18. Allen Kilewella

  Allen Kilewella Verified User

  #18
  Jul 17, 2017
  Joined: Sep 30, 2011
  Messages: 7,686
  Likes Received: 10,980
  Trophy Points: 280
  Mlevi anamuuliza mlevi mwenzie. Ule mwezi ama jua? Mwenzake akamjibu, hata mimi mgeni mtaa huu!!
   
 19. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #19
  Jul 17, 2017
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 33,221
  Likes Received: 40,229
  Trophy Points: 280
  Safi sana Tundu Lissu

  Post sent using JamiiForums mobile app
   
 20. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #20
  Jul 17, 2017
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 22,486
  Likes Received: 13,700
  Trophy Points: 280
  Unaielewa kawaida ya awamu ya tano?
   
Loading...