CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kimeibua mkanganyiko mkubwa kwa wanachama na wananchi baada ya kubadili msimamo wake kuhusu kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.Awali, chama kilieleza nia ya kushiriki uchaguzi lakini Freeman Mbowe alinukuliwa akisema hawatashiriki.
Baadaye, chama kilikanusha kauli hiyo kikisisitiza hakijajitoa. Kwa mshangao mkubwa, Oktoba 27, Chadema kimetoa taarifa rasmi ya kutoshiriki uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Novemba 27.Akitoa tamko hilo, Suzan Limo Spika wa kinachoitwa Bunge la Chadema alisema: "Leo tumewaita kwa hoja mahususi kuhusu mchakato wa kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa... Chadema imejiondoa rasmi kutoka uchaguzi wa vitongoji, vijiji na mitaa."
Hatua hii imeshtua wengi hasa wakati ambapo maandalizi na kampeni za uchaguzi zinaendelea.Wachambuzi wa siasa wameonya kuwa uamuzi huo unaweza kuzorotesha matarajio ya wanachama wa chadema waliokiona kama mbadala wa CCM.
Baadaye, chama kilikanusha kauli hiyo kikisisitiza hakijajitoa. Kwa mshangao mkubwa, Oktoba 27, Chadema kimetoa taarifa rasmi ya kutoshiriki uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Novemba 27.Akitoa tamko hilo, Suzan Limo Spika wa kinachoitwa Bunge la Chadema alisema: "Leo tumewaita kwa hoja mahususi kuhusu mchakato wa kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa... Chadema imejiondoa rasmi kutoka uchaguzi wa vitongoji, vijiji na mitaa."
Hatua hii imeshtua wengi hasa wakati ambapo maandalizi na kampeni za uchaguzi zinaendelea.Wachambuzi wa siasa wameonya kuwa uamuzi huo unaweza kuzorotesha matarajio ya wanachama wa chadema waliokiona kama mbadala wa CCM.
- Tunachokijua
- Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni chama cha upinzani nchini Tanzania, kilichoanzishwa mwaka 1992. Kinajulikana kwa kusimamia demokrasia, haki za binadamu, na utawala bora. Kimekuwa mpinzani mkubwa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika chaguzi mbalimbali.
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni mchakato wa kidemokrasia ambapo wananchi hupiga kura kila baada ya miaka mitano kuwachagua viongozi wa ngazi za mitaa kama vile Wenyeviti wa Vijiji, Wenyeviti wa Vitongoji, na Wajumbe wa Serikali za Mitaa. Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Tanzania kwa Mwaka huu unatarajiwa kufanyika November 27, 2024 (Soma hapa).
Mnamo 27 Octoba 2024 CHADEMA kupitia Bunge la Wananchi ndani ya chama hicho waliita wanahabari ili kuzungumzia mchakato wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 ambao kwa sasa zoezi la uandikishaji wapiga kuwa limekwishafanyika na kukamilika na sasa ni zoezi la uchukuaji fomu za wagombea na urudishaji ukiwa unaendelea ambapo moja ya waliozungumza kwenye mkutano huo ni Suzan Lyimo.
Baada ya mkutano huo na wanahabari kumeibuka kipande cha Video kikionesha kuwa na Logo za Millad Ayo huku kikimuonesha Suzan Limo akitangaza kuwa CHADEMA imejitoa kushiriki kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024.
Je, Ukweli wa kipande hicho cha Video upoje?
JamiiCheck imebaini kuwa kipande hicho cha video kinapotosha, kwani Suzani Lyimo hakusema kuwa CHADEMA imejitoa kwenye mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za mitaa bali alikuwa anatoa ufafanunuzi wa taarifa potofu zilizokuwa zikisambaa mtandaoni kuhusu CHADEMA kujitoa kwenye uchaguzi, ambapo alisema tayari CHADEMA ilitoa taarifa ya kanusho juu ya upotoshaji huo na kwamba wao CHADEMA hawana mpango wa kujitoa kwenye uchaguzi huo.
Aidha, tumebaini kuwa kipande hicho cha video kimehaririwa kutoka kwenye video halisi aliyozungumza Suzan Lyimo kwa kukata vipande vya Video aliyozungumza kwa kuunganisha na kipande kingine cha mbele huku baadhi ya vipande kwenye video vikiondolewa kwenye mtiririko wa video hiyo. Suzan Lyimo ambaye ni Spika wa Bunge hilo la Wananchi kwenye chama cha Demokrasia na Maendeleo alikuwa akitoa ufafanuzi juu ya Mwenendo wa mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa huku akigusia kuwapo kwa upotoshaji wa Taarifa unaodai kuwa CHADEMA wamejitoa kwenye uchaguzi jambo ambalo chama hicho kimekanusha na yeye kusisitiza kuwa hawana mpango wa kujitoa.
-Kwenye video iliyopotoshwa ukitazama kwa makini utaona kucheza(kuruka) kwa video mara Suzan anamaliza kutamka kuwa ''uchaguzi utafanyika tarehe 27 mwaka huu'' kisha kipande kilichoungwa kinaingia kikisema anaomba kuwatangazia umma wa watanzania, na baada ya hapo akitamka neno CHADEMA video inacheza tena na kufuata kipande kilichoungwa kuwa imejitoa kushiriki uchaguzi hali inayothibitisha kuungwa kwa video
Vilevile, Wapotoshaji wamehariri ionekane kama imechapishwa na ukurasa wa MillardAyo wa Instagram ambapo JamiiCheck imefatilia na kubaini kuwa haikuchapishwa na kurasa za MillardAyo bali wapotoshaji wamehariri kwa lengo la kuwapotosha wananchi.