VIDEO: Siri zaidi za kambi ya Singida zajulikana

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
Shuhudia mwenyewe video hii



MORE UPDATES

Mwita Waitara azungumzia mpango ulikuwaje



Slaa azungumzia tukio la tindikali



Mwigulu akiri kuna kambi

KATIKA hali inayoonyesha Chama cha Mapinduzi (CCM) kinafanya kampeni za kijasusi katika uchaguzi mdogo wa Igunga, kimekiri kuwa kimewaweka kambini vijana 386 kwa ajili ya kupata “mafunzo maalumu.”

“Wanadai tumeandaa kambi zaidi ya moja, si kweli, tunayo kambi moja kule Ulemo. Mbona wao CHADEMA wameamua kuwaleta mawakala wa kuhesabu kura kutoka vyuo vikuu? Sisi tukasema hapana, tutawatumia vijana wa Igunga, tukapita kwenye vijiji vyote 96 tukawachukua vijana wanne kila kijiji".

Alisema vijana hao wamekusanywa kutoka vijiji 96 vya jimbo hilo. Kambi hiyo ya vijana imewekwa katika eneo la Ulemo, wilayani Iramba. CHADEMA inadai lengo la CCM ni kuwapa mafunzo ya kigaidi kwa ajili ya kuiba kura na kuanzisha vurugu siku ya uchaguzi.
Gazeti hili limepata habari kwamba kambi hiyo ya wiki moja, ilifungwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana CCM (UVCCM), Martin Shigella, wiki iliyopita, Septemba 9, mwaka huu, na itafanyika tena wiki moja kabla ya uchaguzi.

(Tanzania Daima)
 
Last edited by a moderator:
Hali ni mbaya sana. Mungu atunusuru. Lakini hili wimbi la wahindi, waarabu kujificha ccm tunalichukuliaje?
 
Kijana anaonekana kuguswa sana na umafia unaoendelea ndani ya CCM. Mimi nakubaliana naye kabisa: Bora kufia imani na nchi yako kuliko kuisaliti kama Akina Nape wanavyoendelea kufanya.

Ole wake CCM kama watathubutu kumfanyia ubaya wowote huyu kijana. Watanzania wote tuko mashahidi wa aliyoyasema huyu kijana. Endapo lolote litakupata, Tanzania haitatawalika !
 

Hakuna kitu kinachodai na kinachomtesa mtu mpenda amani au asiependa kuonea mtu kama dhamira. Huyu kijana kaona anachokifanya anakwenda kumfanyia nani na ni kwa nini na ni kwa sababu gani? Hongera kijana kama unayosema ni kweli mungu atakulinda.

Maoni yangu: Hawa vijana wanaojifunza haya mafunzo ni vizuri wakajulikana kwa sababu inawezekana wanawadhuru watu lakini hatuna taarifa. Kila mkoa na wilaya wawe makini na wanapopata hizo taarifa ni kuwashambulia.

Kama ni ruksa kila chama cha upinzani kiazishe kikundi chake. Si wameanza wao.
 
Ni vizuri Ocampo ajulishwe kabla mambo hayajawa mabaya zaidi. Hii tabia ya kutumia vijana kuleta vurugu kwa maslahi ya kisiasa ni sugu kwa Africa, cha ajabu ccm pamoja na kuwa na viongozi vijana bado wanatumia hizi mbinu chafu za kizee kuendesha siasa. Ocampo Ocampo.
 
...sijui kwa nini akili yangu ya nane inaniambia kwamba huu ni mtego ambao CDM wanasubiriwa wanase.

Hapa lazima kuenenda kwa akili sana... Jiulize dogo katoa wapi ujasiri huo wa kusema lolote kama hajatumwa?? Imeandikwa siyo ajabu shetani akaja kama malaika wa nuru na watumishi wake wakaja kama watumishi wa haki.... Kuweni werevu someni kati ya mistari anayoghani dogo mtagundua kuna msukumo wa hila ndani yake... Bora wampokee awe member wa kawaida ila itakuwa KOSA kubwa kumpa kitengo.....

Dogo amejikanganya kiaina kwa namna alivyojieleza....

Kambi ilikuwepo na wamewahi ahed of time wasije wakaumbuka...
 
Taratibu watakuja kuumbuka mmoja baada ya mwingine hongera Chadema Television jitahidini tunataka haya yawafikie wananchi walio wengi.
 
kama yasemwayo na huyo kijana ni kweli, sina budi kuamini kuwa watakaovuruga amani ya Tanzania ni ccm, hatuwezi kukubaliana na ubaradhuli wa namna hii, na kwa hisia zangu iwapo huyu kijana atafanyiwa jambo lolote baya na CCM au mawakala wake, CCM wajue kuwa huyu ndie atakaekuwa Bouaziz wa Tanzania i.e (bouaziz ni yule kijana wa Tunisia aliyejichoma moto kwa kukerwa na manyanyaso ya serikali na hatimaye wimbi la mapinduzi likaanzia tunisia na kusambaa katika mataifa mengine ya kiarabu.)

CCM ni watu wazima lakini sasa akili zao zinawatuma kukalia poti la mtoto kwa kujisaidia.
 
4n yangu haiplay ni nini kipo hebe njulishe
Huyu kijana anadai na yeye alikuwa mmoja wa wana kambi wa Singida ameamua kutubu waliyokuwa wanayafanya huko ambayo ni pamoja na mpango wa vijana wa UWT waliotumwa Arusha kuandaa kura fake wazilete Igunga siku kama mbili kabla ya uchaguzi.
 
Huyu kijana anadai na yeye alikuwa mmoja wa wana kambi wa Singida ameamua kutubu waliyokuwa wanayafanya huko ambayo ni pamoja na mpango wa vijana wa UWT waliotumwa Arusha kuandaa kura fake wazilete Igunga siku kama mbili kabla ya uchaguzi.

C'mon, mpango kuiba kura unapanga na watu zaidi 300. Hivi ninyi mnaichulia poa sana CCM.
 
kama yasemwayo na huyo kijana ni kweli, sina budi kuamini kuwa watakaovuruga amani ya Tanzania ni ccm, hatuwezi kukubaliana na ubaradhuli wa namna hii, na kwa hisia zangu iwapo huyu kijana atafanyiwa jambo lolote baya na ccm au mawakala wake, ccm wajue kuwa huyu ndie atakaekuwa Bouaziz wa Tanzania i.e (bouaziz ni yule kijana wa Tunisia aliyejichoma moto kwa kukerwa na manyanyaso ya serikali na hatimaye wimbi la mapinduzi likaanzia tunisia na kusambaa katika mataifa mengine ya kiarabu.) ccm ni watu wazima lakini sasa akili zao zinawatuma kukalia poti la mtoto kwa kujisaidia!


Akili ya kuambiawa changanya na ya kwako-By JK
MwanaCCM amkosoa Mwigulu kuihusisha CHADEMA na tindikali - YouTube
 
Back
Top Bottom