Video: Shujaa Mbowe alionya lakini akapuuzwa

Kwa hiyo tunamuita nabii au

blast from the past
IMG-20141102-WA0010.jpg
 
Jionee mwenyewe , maana tukiandika tunaonekana tumeongeza chumvi
Erythro, sisi tunaotazama toka nje, tunaona hii ni 'chachu' 'tu kazi yenyewe hasa bado.

Hii ni fursa nzuri sana, ya mahali pa kuanzia kwenda mbele.

Msipochukua tahadhari, hii inaweza ikageuzwa na mahasimu wenu na kuwa kiboko cha kuwatandikia nyinyi.

Kwa hiyo kunahitajiwa pawe na tahadhari kubwa isije ikaonekana nyinyi mnawategemea hao watu wengine wawafanyie kazi mnayotakiwa kuifanya nyinyi.
Ni lazima waTanzania waone mnafanya kazi kwelikweli, na sio kuwategemea hao watu wa nje. H

Hawa shirikianeni nao kwa tahadhari kubwa, hasa katika mambo ambayo nyinyi hamna uwezo nayo, kwa mfano uwepo wa tume huru kabla ya uchaguzi na wakati wa kupiga kura pawepo na utaratibu wa uwazi, ili kura zote zihesabike.

Haya mambo mengine yoote yanayotuhusu sisi wenyewe, fungeni mikanda muyafanye kwa ufanisi.

Kwa mfano: huku kijijini kwetu tunasikiasikia tu fununu zinazomhusu Makonda; lakini kiuhakika sio Makonda anayesemwa ndani ya ujumbe waliotoa Marekani.

Sisi wananchi huku kijijini hatujui lolote juu ya jambo hili. Sana sana tumesikia tu toka kwa Mwenyekiti wetu wa mtaa, ambaye ni ccm, anaeleza jinsi mabeberu waliokataliwa na Baba wa Taifa hili wanavyotafuta njia za kujipenyeza tena ili wanyone mali zetu za madini na utajiri mwingine.
Haya ndio tunayoyasikia, hatusikii chochote toka kwenu. Vipi?

Mfano wa pili. Kama kweli mnataka kushiriki kwenye uchaguzi unaofuata, wakati wa kuwaandaa wagombea ni sasa. Tafuteni watu wengi, kila jimbo liwe na mgombea na hao mnaowasimamisha wawe wameandaliwa barabara.

Hapa ndipo ninapokuwa na matumaini ya uwepo wa John Mnyika. Kazi yake itapimwa baada ya uchaguzi. Hii ni nafasi yake nzuri sana ya kujijengea sifa nzuri ya uongozi katika maisha yake.

Sihitaji kuchukua Kadi, ili mkipewa uongozi niwashikie bango ipasavyo.
 

Makonda, Magufuli, Ndugai na Mataga wote ni waoga, wavivu wa kufikiri, wabaguzi na wajinga!
Wao ukiwashinda kwa hoja wana chukulia personal...!
Kuanzia kitambo sana, Magufuli ana historia ya kuumiza ama kudhuru kwa namna mbali mbali wote waliokuwa wanabishana au kuchuana naye kwenye maamuzi au kwenye uchaguzi! Fika pale Geita mjini utapewa mifano kama yote!
Makonda kwa uvivu, woga na ujinga wake tulishuhudia akimshambulia bila aibu senior wake na mwanachama mwenzake (Judge Warioba) kisa tu wametofautiana mawazo!
Tumeshuhudia Ndugai akiwacharaza bakora wanaomshinda kwa hoja... Na tumeshuhudia akiwadhalilisha wabunge na wote wenye mawazo tofauti na yeye (Halima Mdee, Zitto, Tundu, CAG n.k)!
Wengine tuliwaza mbali sana... Tukajiuliza hivi hawa ndani ya chama tu wakishindwa kwa hoja wanapiganat itakuwajewakipewa madaraka makubwa??

Yaliyoendelea baada ya hapo sote tunahisi kuna ushiriki wao wa moja kwa moja!
Fast forward... Mmarekani sasa anawa search mmoja baada ya mwingine!
Yajayo yanafikirisha!
 
Back
Top Bottom