Video shows Minneapolis cop with knee on neck of motionless, moaning man who later died

Amani kwako.

Kuna video inatrend sana mitandaoni (nimekuwekea chini) ikionyesha askali wa kibeberu akimkaba mmarekani mweusi pembeni ya gari kwa takribani dakika 10 ambapo jamaa alikuwa akilalamika, ila baadaye jamaa alikata kauli na kufariki dunia.

Kutokana na tukio hilo askali muhusika na wenzake watatu wamesimamishwa kazi, ila watu mbalimbali duniani wanasema adhabu hiyo haitoshi kukingana na matukio wanayotendewa watu weusi nchini humo na adhabu zitolewazo kwa waliohusika na kisa.

Panoja na hilo, jamii ya wamarekani weusi katika majimbo mbalimbali wamefanya maandamano kushinikiza hatua mbalimbali zichukuliwe, raia wengine wamevamia vituo vya polisi na kuanza kufanya fujo, huku wakivunja magari na kuwapiga mawe polisi ikiwa ni gadhabu kutokana na tukio hilo.

Vile vile raia, jamii ya kizungu wameonekana kukerwa na tukio hilo huku wakionyesha hasira kwa kupasua vioo vya magari nk.

Angalia sinema hapa👇ya kwanza ni wakati wa tukio la kikatili na ya pili wananchi wakifanya yao.



 
Tuwe wakweli.

US askari akishafanya hivi atashtakiwa, kisha kutokana na ushahidi uliopo na sheria zao atahukumiwa mfano kesi ya Rodney King.

Nchi za Afrika askari akiua tarajia atakingiwa kifua na hata mahakamani asifike.

So in Us hakuna aliye juu ya sheria (ingredient muhimu ya demokrasia) kwa bara letu ni kinyume chake. Hivyo ni sawa tu kusema wapo mbele kutuzidi kidemokrasia.
Umeongea point ya maana sana! Watu wanaleta ushabiki as if wametumwa na serikali au wanatekeleza sheria! Ni wapuuzi hao askari na kitanzi watakula. Ingekuwa China na shitholes nyingine wala hata hizo habari zisinge-leak.

Bwana Utam na STRUGGLE MAN mnakumbuka yaliyotokea ubalozi wa Saudia binadamu kukatwakatwa vipande vya nyama? Kuna ukatili zaidi ya ule uliofanyika ndani ya afisi rasmi ya serikali?
 
Hii video imeniuma sana.

Hicho kimbilikimo hapo ndio angepaswa hata amzuie mwenzake, unamwambia mtu get in the car na kati unaona kagandamizwa hapo?

Na ukiangalia unaona kabisa huyo muuaji pamoja na kumwekea goti shingoni, lakini kagandamiza mkono kwenye paja ili aongeze pressure.

Huyu alidhamiria kuua, na jamaa alifia pale pale hata jamaa alivyokuja kumtest alikuta ashakufa, wasidanganye watu

Yule Wa team ya msaada naye kaja kampima mapigo kaondoka bila hata kumzuia police na kaenda kutumia dk kama tatu ndio kurudi.
 
Kuna mtu humu anaitwa Erythrocyte hawa wamarekani wakitoa kauli zao kwa serikali yetu utamsikia eti mungu wabariki wamarekani. Huwa namsoma huyu mtu anavyowapapatikia wamarekani najua siasa zinamtoa akili. Haya ndio mambo ya kawaida wamarekani weupe wanafanyia watu weusi huko kwao halafu unajidanganya wanakupenda wewe mwafrika!
 
Moderator Mhariri na wengineo, unapounganisha uzi hebu angalia inside content ipi inaeleweka kwa wasomaji, siyo kuunganisha tu uzi huu na picha ambayo haina maelezo aseee😬siyo sahihi.

Kama mmenielewa nadhani kuna kitu mtafanya.
 
Waafrica sisi wanafiki sana, hapa Bongo albino wanauawa na Watanzania wenzao ila huoni hizi comments.
 
Kuna mtu humu anaitwa Erythrocyte hawa wamarekani wakitoa kauli zao kwa serikali yetu utamsikia eti mungu wabariki Wamarekani. Huwa namsoma huyu mtu anavyowapapatikia wamarekani najua siasa zinamtoa akili. Haya ndio mambo ya kawaida wamarekani weupe wanafanyia watu weusi huko kwao halafu unajidanganya wanakupenda wewe mwafrika!
Acha ujinga wewe kwani hilo tukio limefanywa na Serikali ya Marekani? Unashindwa kutofautisha Jambo linalofanywa na Serikali ya Marekani na Jambo kufanywa na mmarekani.

Hilo Jambo limefanywa na Askari wa kimarekani na ameshafukuzwa kazi for further steps. Bongo mangapi yanafanywa na watu wapo kitaa.


Acha kulinganisha United States na takataka utakuwa kichwani hauko sawa.
 
Back
Top Bottom