Video: Sabaya azomewa "mwiziiiii mwiziiiii!" Hakika cheo ni dhamana

View attachment 1822689

Hakika cheo ni dhamana. Tumia cheo kutenda haki, tenda kazi ya Mungu.

Hili ni funzo kubwa sana kwa wenzetu mnaoteuliwa na kuchaguliwa. Oneni mwenzenu anavyodhalilika. Hamjachelewa sana,huu ni wakati wa kulia na kutubu hadharani
Hiyo ndiyo nafasi pekee waliokuwa wakiitafuta wananchi ili waonyeshe hisia na chuki zao dhidi ya kiongozi katili.
 
kilicho fanywa na kundi hilo la watu walio kuwa nje ya mahakama ni kuikosea heshima mahakama au kuidharau mahakama, huwezi kutoa maneno ya kashfa kwa mtuhumiwa mbele ya mahakama!!.

kitendo cha wazomeaji hao kinaweza kuzua vurugu na uvunjifu wa amani miongoni mwa watu amabo wana chuki na sabaya na wengine ambao bado ni wafuasi wa sabaya.

kitendo kama hicho kisijirudie tena, Jeshi letu la polisi lisiruhusu utovu kama huo kutendeka mbele ya jengo la kutolea haki.
 
Hivi anajitetea mwenyewe au anatumia wakili, huyo wakili atakuwa na kibarua kigumu sana kwa ushahidi ule wa video!!
Tena kwa video hii,kesi yake ndio inakuwa rahisi kabisa, maana hakimu atakuwa na wakati mgumu,akipatikana na hatia itaonekana hakutendewa haki, kwani alihukumiwa na umma kabla ya kesi kusikilizwa na hakimu alishawishiwa na kelele za wananchi na vyombo vya habari havikumlinda kabisa.
 
Pole yake sana , huu msiba uliisha pale pale chato siku ile ile
Sabaya anavuna alichokipalilia kwenye shamba la mwendazake
 
Back
Top Bottom