Ningehadithiwa bila kuona video ningesema magazeti uchwara yamem quote vibaya, kwa sababu kutokuwepo kwa open space jijini Dar es Salaam ni crisis kubwa sana ya mipango jiji
Natambua Rais amesema eneo alilolitoa kwa taasisi hii ya Kiislam linaenda kujengwa hospitali ambayo itatumika kwa Watanzania wote, wa dini zote na wasio na dini.
Lakini pamoja na kwamba sote tutatibiwa hapo, Rais unaposema open space haina maslahi kwa hiyo naigawa ijengwe kitu chenye maslahi, huyu Kiongozi wetu anafikiria vitu kwa umakini gani?
Hivi Open Space maana yake ni kwamba ni kwamba hakuna kitu cha maana cha kujenga hapo? Hivi ndivyo Rais wetu anavyochambua mambo anapokaa Ikulu?
Na kwamba sehemu nyingine zooooote zimejaa Tanzania nzima za kujenga dispensary akashindwa kuwapa kiwanja huko?
And that is assuming kwamba wanajenga hospitali, manake msemaji wa Waislam kaomba eneo la "kupanua shule yetu ili tuweke form 5 na 6 na mabweni ya Wasichana..."
Rais anakuja dakika tano baadae kusema mmeomba eneo ambalo "mnaenda kujenga nadhani hospitali..." UNADHANI HOSPITALI? Huna hakika?
Seriously hukumsikia Shehe? Kwenye siku ya Qurani tunaweza kujisahaulisha na kupindisha kauli namna hii mbele ya hadhara?