VIDEO: Rais Kikwete awajibu wanaoponda safari za nje ya nchi

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Mheshimiwa Rais kawajibu wale wote wanaoponda safari zake za nje... enyi watanzania mwenye masikio na asikie...

[video=youtube_share;KZ1FVYyGxio]http://youtu.be/KZ1FVYyGxio[/video]
 
Kumsikiliza huyu Kiumbe ni sawa na kupoteza muda. Hana mpya yoyote atakayoisema zaidi ya ujeuri ua ufedhuli wake
 
Da eti sisi ni masikini nani atufuate.... Mataifa yaliyoendelea yanatafuta natural resources kwa hiyo lazima watawatembelea, lakini je hata usipotembelewa una shida gani? Aaangalie wenzake wamefanya safari ngapi na je wamewakilishwa na viongozi wengine safari ngapi. Hapa kweli tulichemsha sana watanzania
 
Mheshimiwa Rais kawajibu wale wote wanaoponda safari zake za nje... enyi watanzania mwenye masikio na asikie...

[video=youtube_share;KZ1FVYyGxio]http://youtu.be/KZ1FVYyGxio[/video]

Sawa bwana Vasco dagama
 
Mheshimiwa Rais kawajibu wale wote wanaoponda safari zake za nje... enyi watanzania mwenye masikio na asikie...

[video=youtube_share;KZ1FVYyGxio]http://youtu.be/KZ1FVYyGxio[/video]

Je lini atawajibu watanzania kuhusu Maisha bora kwa kila mtanzania?
 
Tatizo siyo kwamba tanzania isisafiri nje, bali rais asifanye kazi ya waziri wa mambo ya nje. Safari hizo ni kazi ya waziri wa mambo ya nje. Safari zingine anakwenda kuhudhuria semina ambazo ni jukumu la maafisa wa serikali wala siyo mawaziri
 
Kwa mlio msikiliza anasemaje kwa ufupi maana kheri niambiwe kuliko kumsikiliza.
 
Da eti sisi ni masikini nani atufuate.... Mataifa yaliyoendelea yanatafuta natural resources kwa hiyo lazima watawatembelea, lakini je hata usipotembelewa una shida gani? Aaangalie wenzake wamefanya safari ngapi na je wamewakilishwa na viongozi wengine safari ngapi. Hapa kweli tulichemsha sana watanzania
Anafikiri kwa kutumia makario. Dr. Masaburi.
 
Hatulalamiki kwanini anaenda nje, tunacholalamika safari zimezidi kama vile yeye ni waziri wa mambo ya nje. Na kitu kingine kinashangaza kwenda nje kuwaalika watu waje kutuibia natural resources zetu. Kama sisi hatuna uwezo bora tuziache ardhini mpaka tutakapo pata uwezo. Ndio maana mikataba inakuwa mibovu kwa sababu tunawabembeleza waje kuwekeza. Wawekezaji wa ndani ni wa muhimu kuliko wa nje, serikali ijaribu kuelimisha watu wake kuwekeza, kuliko kupoteza muda kuzunguka nje kutafuta wawekezaji. Elimu bora na uzalendo ndio imewafikisha wenzetu walipo huko mnakoenda kushangaa na si wala safari za kutembelea nchi zilizoendelea. Safari za mara kwa mara si uzalendo kwa nchi yetu hata kidogo.

Kwanini wenyewe hawaji kutuambia tukawekeze kwao
 
Tatizo siyo kwamba tanzania isisafiri nje, bali rais asifanye kazi ya waziri wa mambo ya nje. Safari hizo ni kazi ya waziri wa mambo ya nje. Safari zingine anakwenda kuhudhuria semina ambazo ni jukumu la maafisa wa serikali wala siyo mawaziri

Hakuna safari iliyonikera na kunifedhehesha kama hii "aliyodandia" kwa Ngeleja......Rais wa nchi yangu kuvishwa name tag ilikuwa fedheha sana!....na hakukuwa na Rais mwingine hata wa Burundi hakuwepo!

ngeleja1.jpg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom