VIDEO: Prof. Lipumba akiri kumsaidia Rais Kikwete katika Uchaguzi 2010

Lipumba ni wa ovyo sana.Na nadhani hata wale mateja aliowarubuni wakavunje mlango wa ofisi aliwahadaa kwa kutumia udini.
 
Mmmh, nimeisikiliza hii video hadi Mwisho. Naweza kusema Lipumba amepoteza uhalali wa kuwa mwenyekiti wa CUF. Maana ameonyesha dhahiri kwamba yeye ni kiongozi wa waislam na si watanzania. Kwa msingi huo CUF ni chama cha waislamu.
Akawe imamu maana hata wale anaowatumia leo hii ni kupitia dini.Yametimia.
Lipumba hafai hata kuwa Imamu wa msikiti, akiwa Imamu atataka awe Imamu wa Maisha kama alivyokuwa Mwenyekiti wa Maisha huko CUF

Waislam for 50 yrs bado tunalalamika na kuendelea kuichagua CCM badala ya kuangalia maendeleo ya nchi, sisi tunakadhania Uislam na Ukiristo huku Rasilimali zetu zinaibiwa na Wawekezaji walioletwa na Kikwete na CCM yake

Rais
Jaji Mkuu
Mkubwa wa Usalama wa Taifa
IGP
Hao wote ni waislam na bado tunalalamika kuwa tunaonewa, ni nani hasa anayetuonea kama sio sisi wenyewe tunaoneana? Tusitafute mchawi wakati mchawi wetu tunamchua kuwa ni CCM.

Badala ya kufikiria Maendeleo ya Taifa letu bado tumegubigwa udini na kunyooshea wenyewe kwa wenyewe vidole, sisi wote ni Watanzania na tuna haki ya kuishi katika Taifa letu bila ya kujali dini. Adui wa Muislan ni CCM hakuna mwengine.

Kikwete nchi imemshinda asitafute mchawi, aondoke kabla halijaangamia hili Taifa.

Sisi Waislam tujue kuwa Ukiristo, Uislam, Ubaniani, Ugalatia na dini nyingine zitakuwepo Tanzania na zitaendele kuwepo, as long the world still exist na hizo dini zitakuwepo.

Kwa hiyo wahubiri wa dini, Get lost

Adui wa Waislam ni CCM, tukifanikiwa kumtoa hii nchi itatulia na maendeleo ya nchi yatapatikana

Bado Nina Mashaka na Elimu ya Prof Lipumba naona haiimsaidi kujua lipi ni zuri na lipi ni baya kulisema kwenye jamii, hafai hata kuwa Kiongozi wa Mtaa. Shame on him.

Huyu Lipumba hana lolote anajitia anatatea haki za dini kumbe uchu wa madaraka kama alivyo Kikwete, Lipumba hafai hata kuongoza kwao urambo hatoweza.
 
Eti unajiita mpinzani wa kweli, wewe ni mpinzani wa nani wakati mpinzani wako unamgawia kura zako!
Hapo ufahamu kua hapa ndipo maalim Seif alipokosa imani na wewe! Kwa tabia hiyo unafikiri maslim Seif angekuamini? Maalim Seif ana akili alijua kua wewe ndiye ulieiua CUF. Maalim Seif alijua wewe sio mpinzani wa kweli ndio maana ulilalamika unatengwa.


Usipimane ubavu na Maalim Seif, type yake ilikua Nyerere na sio wewe! Kumbuka kua Maalim Seif alimsumbua sana Nyerere kwahiyo poteza tu muda wako yeye anakuchora tu.


Wanaokutaka kwa sasa walikua wapi wakati inaondoka? Mbona hawakukushikia mabango usiondoke kipindi hicho?


Kwakweli wapinzani wa kweli walionekana mwaka 2015 wakati wa uchaguzi.

Hebu tuwekeni na ile ya LOWASA ya kule TABORA ya akina lutherani
 
Hebu tuwekeni na ile ya LOWASA ya kule TABORA ya akina lutherani
Na yeye alisema atamsaidia Magu? Maana mada hapa ni kiongozi wa upinzani kusema kamsaidia mgombea wa chama tawala.
Lipumba anastahili adhabu ya bakora hamsa wa ishirini ili kumrudisha akili ikae sawa
 
Wakuu,

Katika zunguka zangu nikitafuta video ya kinachodaiwa kunaswa na Tanzania Daima (Ref Lipumba akiri kumsaidia Kikwete Uchaguzi 2010), nimefanikiwa kuipata video hii katika YouTube. Nimetafuta Part 2 ya Video hii sijaipata, nawashirikisha Part 1 yake ili tunapojadili mambo kama haya tusiuziwe mbuzi katika gunia.

Kinachoshangaza, tumefikia hatua hii kama nchi? Ndizo siasa zilizo nyuma ya pazia na wananchi tumefumbwa macho?

Video yenyewe hii hapa:

Screenshot_2023-08-20-17-05-45-1.jpg
 
Back
Top Bottom