SI KWELI Video: Polisi Uganda wamekamata gauni la kifahari aliyekuwa spika wa nchi hiyo kufuaia tuhuma za rushwa zinazomkabili

SI KWELI Video: Polisi Uganda wamekamata gauni la kifahari aliyekuwa spika wa nchi hiyo kufuaia tuhuma za rushwa zinazomkabili

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Police in Uganda have arrested a dress belonging to Parliament Speaker Anita Among. The designer outfit, which she wore during President Museveni's recent swearing-in, was reportedly purchased for Ksh. 1.1 million. Among is facing corruption allegations.

Screenshot 2026-05-21 080215.png
 
Tunachokijua
Madai

Kupitia mitandao ya kijamii ikiwemo Faceboo na Instagram kumekuwana kipande cha video kinachosambaa kikionesha gari linalodaiwa ni la polisi likisafirirsha nguo ambayo inadiawa kuwa ni nguo ya gharama ya aliyekuwa Spika wa bunge la Uganda kuanzia mwaka 2022, Anita Among.

Uhalisa wa madai hayo

Video pamoja na taarifa hii inajiri kipindi ambacho Anita anakabiliwa na shutuma za rushwa pamoja na ubadhiifu wa mali za umma ambapo baadhi ya mali zake zinashikilia na jeshi la polisi.

Vyanzo mbalimbali nchini Uganda viliripoti matukio ya kukamatwa kwa mali za Anita ikiwemo Daily Monitor ambao walichapisha video pamoja taarifa kuwa Polisi wameanza kubeba magari ya aliyekuwa Spika wa nchi hiyo kutoka katika makazi yake huko Nakasero kufutia tuhuma zinazomkabili.

Hakuna taarifa za ziada zilizochapishwa na vyanzo vya kuaminika kuonesha kuwa kuna gari lililobeba nguo za kiongozi huyo kwa kuwa ni za gharama sana kufuatia kwa tuhuma zinazomkabili.

Ufuatiliaji zaidi umebaini kuwa video hiyo imehaririwa ama kutengenezwa kwa Teknolojia ya Akili Unde huku ikonesha baadhi y dosari ikiwemo nembo ya jeshi la polisi kuwa na baadhi ya mapungufu, gari kukosa namba ya usajili ya polisi (UP) na watu kutokuonekana vizuri.
Back
Top Bottom