VIDEO: Polisi Marekani wameingia chaka kumkamata undercover FBI Agent Raia mweusi mwenye asili ya Sudan Kusini

Status
Not open for further replies.

black sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
18,240
2,000
ila mitandao ina nguvu sana aisee.

huyo anyeitwa afisa wa FBI,ni nigga mmoja alifananishwa na polis wakagundua waliingia cha kike kumshika hakuwa wanayemtafuta,wakurungwa wameunga n story iliyopo.

afisa wa FBI akatae kukamatwa,halafu atoe kitambulisho,kazi si ndo imeishia hapo!!!

hii story ya mwaka jana imebadilishwa na kuwa mpya na kibaya zaidi imekuwa kama picha la kihindi

Fake news

Kweli mitandao ina nguvu
Siku hizi kuna watu walikuwa kila wakipata clip mbio kunitumia nikiwaambia sio kila kitu mnaamini wamenichoka sasa
 

denis fourplux

JF-Expert Member
Aug 17, 2017
962
1,000
This is a fake story. Hii ni habari ya mwaka jana na haihusiani na maandamano ya sasa.

Lakini pia huyo jamaa sio FBI agent. Ni kwamba walimfananisha na mtuhumiwa waliyekua wanamtafta alipotoa kitambulisho ikaonekana sio yeye.

Sasa mataahira wa mitandaoni chochote wanachokipokea wanakichukua kama kilivyo.

Alichukua ID zao za nini kama hana cheo pahala popote?
 

Consigliere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
12,004
2,000
Mkuu weww ni muha nini? Umesema mwenyewe *hakuna alipochukua vitambulisho vyao* kucomment hii unasema uliyemkatia kaongea Id na sio card(bussiness). Huoni kauli zako zinautata. Maana video inaonyesha wakimpa vitu hakuna ajuaye kama ni Id au business card.
Pia, kinachofanya watu waamini ni FBI ni hili tukio la mkamatwaji kupewa Id/bussiness card na polisi. Embu imagine polisi akukamate kisha akuachie na utambulisho wake akuachie. Hili si jambo jepesi kwa viburi walivyonavyo mapolisi. Kumbuka pia aliyekamatwa ni black hawawezi muogopa kiasi cha kumpatia Id/bussiness card kama sio mtu fulani
Kwa hiyo unakiri kwamba ni imani ya watu kuwa huyo ni FBI lakini hakuna popote alipojitambulisha hivyo. Wanaamini hivyo kwasababu ya kuona na kumsikia jamaa akiwaomba kadi ya inayotambulisha shughuli zao.

Huyo hakuomba IDs zao bali busines cards, na Polisi walikuwa wapole baada kujiridhisha kwamba waliyekuwa wanamfikiria siye, na jamaa alianza kuja juu baada ya kuina Polisi wamejiridhisha kwamba siye.

Elewa kwamba baada ya tukio hilo huyo jamaa na yeye kwa upande wake ana haki zote za ku open charges, na Polisi kutoa business cards zao ni lazima ili akienda kufungua malalamikoawe na taarifa zao ndiyo maana walimpatia business cards zao sababu wanajua huyo jamaa ni haki yake kisheria.

Sasa hapo sijui habari sijui za Muha zinatoka wapi? Mnawashutumu wazungu kuwa ni wabaguzi wakati ninyi ubaguzi umetamalaki kuanzia kwenye sura, ngozi, maneno tabia hadi uboho.
 

The Underboss

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
3,953
2,000
Kwa hiyo unakiri kwamba ni imani ya watu kuwa huyo ni FBI lakini hakuna popote alipojitambulisha hivyo. Wanaamini hivyo kwasababu ya kuona na kumsikia jamaa akiwaomba kadi ya inayotambulisha shughuli zao.

Huyo hakuomba IDs zao bali busines cards, na Polisi walikuwa wapole baada kujiridhisha kwamba waliyekuwa wanamfikiria siye, na jamaa alianza kuja juu baada ya kuina Polisi wamejiridhisha kwamba siye.

Elewa kwamba baada ya tukio hilo huyo jamaa na yeye kwa upande wake ana haki zote za ku open charges, na Polisi kutoa business cards zao ni lazima ili akienda kufungua malalamikoawe na taarifa zao ndiyo maana walimpatia business cards zao sababu wanajua huyo jamaa ni haki yake kisheria.

Sasa hapo sijui habati sijui ni Muha zinatoka wapi. Mnawashutumu wazungu kuwa ni wabaguzi wakati ninyi ubaguzi umetamalaki kuanzia kwenye sura, ngozi, maneno tabia hadi uboho.
Mkuu tatizo la watu wengi hua kila kitu wanakichukua kama kilivyo. Yaani chochote wakiona mtandaoni basi wanakiamini kama kilivyo, hawajiulizi hata kidogo.

Hii mitandao ya kijamii itaharibu sana hiki kizazi. Ni rahisi sana kulisha uongo na uzushi hiki kizazi kupitia mitandao na wao wakaumeza huo uongo kama ulivyo.

Hii video ni ya mwaka jana, haihusiani kabisa na maandamano ya kifo cha Floyd ila wahuni wameitungia uongo na kuitupia mitandaoni watumiaji wa mitandao wameimeza kama ilivyo.
 

Vi rendra

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
3,051
2,000
watu weusi jamboo dogo utaskia tumebaguliwa
tupunguze na mentality ya ubaguzi japo ubaguzi upo kweli
Mbongo mpe picha story atakupa.

Hii video imekuwepo kitambo.

Askar wamemfananisha huyu jamaa. Na walipoangalia id yake ndyo kugundua sio wanayemtafta.
 

Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
25,013
2,000
Undercover unatembea na kitambulisho? Inakuingia akilini?

Hata ukicheki muvi ambazo kunakua na undercover agent utagundua hata wakikamatwa hawabishi, wanaenda mpaka kituoni na in some cases wanakua processed kabisa.

Kureveal kama wewe ni undercover kisa kukamatwa imagine ndiyo unatishiwa bunduki si utatoa siri zote?

Pia hii video nimetafuta credible source nimekosa. Website 2 tu zina hii habari. Youtube na moja inaitwa eyegambia na hiyo eyegambia siyo original owner badala yake na yenyewe inasema 'according to reports'
 

Blood of Jesus

JF-Expert Member
Sep 19, 2016
1,477
2,000
Mkuu walikosea lazima wangeomba ID ya jamaa,jamaa anawaambia siyo mimi wao wanaforce,wangemwomba ID wahakikishe ndo wanayemtafuta
Kwa kawaida sio rahisi mhalifu ajitaje. Pia unaweza ukamwomba kitambulisho akajidai anakitafuta mfukoni, akachomoa silaha akawadhuru.
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom