Video: Peter Msigwa amkosoa Vikali Spika Ndugai, Ampa Ushauri huu - Sakata la Halima Mdee na Wenzake

Huyu mchungaji ganja kweli kweli, hivi wangekuwa site mirrow si gari ingekuwa ilishapata ajali na kupinduka na kuua watu???? Yaani wanasahau kabisa walishawahi omba ndege na uwajibikaji na kumtegemea Mungu na ndiyo hao hao waliogomea bunge na kulaumu serikali kwa kununua ndege pamoja na kulaumu serikali kwa nini imeleta uwajibikaji???
 
Swali la mwisho limemkamata Mchungaji 'off guard".
Yes, hili swali la mwisho kashindwa kulijibu inavyotakiwa...

Nina hakika hata mtangazaji ameuliza hili swali akiwa hajui anataka jibu la namna gani kutoka kwa mteja wake na kwake jibu lolote ni sawa...

KWA MAONI yangu, nadhani Mch. Peter Msigwa angeweza kujibu swali hilo kwa kuzingatia maelezo yafuatayo;

å Ni hivi ndugu mtangazaji, duniani kote hakuna nchi isiyokuwa na serikali. Kila nchi ina serikali...

å Tofauti ni aina ya serikali inayoongoza/tawala nchi husika...

# Angeendelea kusema;

å Kuna serikali zilichoguliwa kidemokrasia na kutawala kwa ridhaa ya wananchi..

å Na kuna serikali zinatawala kwa mabavu. Zimejiweka zenyewe. Hazina ridhaa ya wananchi na mfano ni kama serikali hii ya Tanzania chini ya CCM na huyu anayeitwa "Rais" Magufuli...

å Wanadai wamechaguliwa kihalali katika uchaguzi wa kidemokrasia uliofanyika tarehe 28/10/2020...

å Ukweli ni kuwa huo haukuwa UCHAGUZI bali UCHAFUZI ama maigizo ya UCHAGUZI. Waliandaa uchaguzi kama hadaa na geresha tu huku wakiwa tayari wana matokeo ya mfukoni, nani ni Rais, diwani na mbunge. Kauli na matendo yanathibitisha..!!

å Serikali kwa kutumia vyombo vya dola na Tume ya uchaguzi (NEC), zilipora maamuzi halali ya wananchi kuchagua viongozi kupitia sanduku la kura na badala yake wakawaweka viongozi wasiotokana na ridhaa ya wananchi, wasiochaguliwa na wananchi akiwemo Magufuli na Hussein Mwinyi kule Zanzibar...

å Sasa wananchi wanajua kuwa waliporwa haki ya kuchagua. Wanalalamika na kuwapigia kelele hawa wanajiita "viongozi waliochaguliwa"...

å Nafsi zao zinawahukumu. Na wao wanaujua ukweli kuwa hawakuchaguliwa, hawakushinda na hawana uhalali wa kuunda serikali lakini kwa mabavu wameunda. Wanawatawala watu kwa lazima, kwa mabavu. Na mfano ni haya yanayofanyika sasa yaani kina Halima Mdee na wenzake...

å Ili kutafuta uhalali wanajaribu kutumia hadaa na ghiriba kuzitumia baadhi ya taasisi ikiwemo vyama vya siasa ikiwemo CHADEMA ili kupata uhalali wa kuitwa " serikali yenye ridhaa ya wananchi "...

å Kwa hiyo, baada ya maelezo hayo Mch.Peter Msigwa angemalizia tu kwa kusema;

".... Tunachokipinga sisi ni serikali hii isiyokuwa halali kujaribu kututumia sisi CHADEMA kama taasisi kujipa uhalali wa kutawala na ndiyo maana wanachama wwnzetu katika taasisi yetu wanaoshiriki uharamu huu, tunafanya kila tunaloweza kwa kuzingatia sheria, miongozo na katiba ya chama kujitenga nao ikiwemo kutokuwa na ushirika nao ili wakipenda wajiunge na wezi wenzao..."

".....kwa hiyo, ni lazima kila wanapohadaa umma kwa kuwatumia baadhi ya wanachama wetu na kwa jina la chama chetu (CHADEMA), kutafuta uhalali, tuwataarifu kuwa sisi hatuwatambui na wala hatuna ushirika nanyi katika hayo mnayofanya. Kwa hiyo siyo swala la kuitambua ama kutoitambua..."
 
Yes, hili swali la mwisho kashindwa kulijibu inavyotakiwa...

Nina hakika hata mtangazaji ameuliza hili swali akiwa hajui anataka jibu la namna gani kutoka kwa mteja wake na kwake jibu lolote ni sawa...

KWA MAONI yangu, nadhani Mch. Peter Msigwa angeweza kujibu swali hilo kwa kuzingatia maelezo yafuatayo;

Ukweli ni kuwa, dunia kote hakuna nchi isiyokuwa na serikali. Kila nchi ina serikali...

Tofauti ni aina ya serikali inayoongoza/tawala nchi husika...

Angeendelea kusema;

å Kuna serikali zilichoguliwa kidemokrasia na kutawala kwa ridhaa ya wananchi..

å Na kuna serikali zinatawala kwa mabavu. Zimejiweka zenyewe. Hazina ridhaa ya wananchi na mfano ni kama serikali hii ya Tanzania chini ya CCM na huyu anayeitwa "Rais" Magufuli...

å Wanadai wamechaguliwa kihalali katika uchaguzi wa kidemokrasia uliofanyika tarehe 28/10/2020...

å Ukweli ni kuwa huo haukuwa UCHAGUZI bali UCHAFUZI ama maigizo ya UCHAGUZI..

å Serikali kwa kutumia vyombo vya dola na Tume ya uchaguzi (NEC), zilipora maamuzi halali ya wananchi kuchagua viongozi kupitia sanduku la kura na badala yake wakawaweka viongozi wasiotokana na ridhaa ya wananchi, wasiochaguliwa na wananchi akiwemo Magufuli na Hussein Mwinyi kule Zanzibar...

å Sasa wananchi wanajua kuwa waliporwa haki ya kuchagua. Wanalalamika na kuwapigia kelele hawa wanajiita "viongozi waliochaguliwa"...

å Nafsi zao zinawahukumu. Na wao wanaujua ukweli kuwa hawakuchaguliwa, hawakushinda na hawana uhalali wa kuunda serikali lakini kwa mabavu wameunda. Wanawatawala watu kwa lazima, kwa mabavu. Na mfano ni haya yanayofanyika sasa yaani kina Halima Mdee na wenzake...

å Ili kutafuta uhalali wanajaribu kutumia hadaa na ghiriba kuzitumia baadhi ya taasisi ikiwemo vyama vya siasa ikiwemo CHADEMA ili kupata uhalali wa kuitwa " serikali yenye ridhaa ya wananchi "...

å Kwa hiyo, baada ya maelezo hayo Mch.Peter Msigwa angemalizia tu kwa kusema;

".... Tunachokipinga sisi ni serikali hii isiyokuwa halali kujaribu kututumia sisi CHADEMA kama taasisi kujipa uhalali wa kutawala na ndiyo maana wanachama wwnzetu katika taasisi yetu wanaoshiriki uharamu huu, tunafanya kila tunaloweza kwa kuzingatia sheria, miongozo na katiba ya chama kujitenga nao ikiwemo kutokuwa na ushirika nao ili wakipenda wajiunge na wezi wenzao..."

".....kwa hiyo, ni lazima kila wanapohadaa umma kujipa uhalali kwa kuwatumia baadhi ya wanachama kwa jina la chama chetu (CHADEMA), tuwataarifu kuwa sisi hatuwatambui na wala hatuna uahirika nanyi katika hayo mnayofanya...."
Naamini ulichoandika kitawasaidia sana CDM
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom