VIDEO - Paka na Mamba Nani Zaidi? Paka

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,315
33,111
<table border="0" cellpadding="0" cellspacing="0"><tbody><tr><td colspan="3" style="padding-left: 10px; padding-top: 5px; width: 491px;"></td> </tr> <tr style="background-color: rgb(225, 225, 225); padding-top: 10px;"> <td style="width: 250px; padding-left: 5px; padding-bottom: 5px; padding-top: 5px;" valign="top">
5136194.jpg

Mtanange wa paka na mamba, mshindi alikuwa ni paka</td> <td style="padding-left: 10px; width: 316px;" valign="top"> Tuesday, November 16, 2010 2:15 AM
Kwa kuambiwa huwezi kuamini na hata kwa walioshuhudia kwa macho yao hawakuweza kuyaamini macho yao, paka ameweza vipi kusimama kidete mbele ya mamba mkubwa kama huyu na kufanikiwa kumfanya mamba akimbilie majini.</td> </tr> <tr> <td colspan="3" style="vertical-align: top; width: 491px;"> VIDEO ya tukio hilo lililotokea mjini New Orleans nchini Marekani imekuwa gumzo la siku kwenye televisheni za Marekani.

Paka mwenye umbile la kawaida alisimama kidete mbele ya mamba ambaye binadamu mwenye akili zake asingeweza kumsogelea karibu.

Katika tukio hilo ambalo ni nadra sana kulishuhudia duniani, paka alishinda gemu kwa kufanikiwa kumtisha mamba kwa mikwara yake na kumfanya mamba akimbilie majini.

Hata baada ya mamba huyo kurudi tena na mwenzake, paka huyo aliendeleza mikwara yake na kuwatiririsha mamba wote wawili majini.


</td></tr></tbody></table>
 
Last edited by a moderator:
Si sawa kabisa kulinganisha mamba na paka. Nafikiri hao mamba wote wameshiba, ndiyo maana hata binadamu wapo hapo karibu na hawaogopi. Usiniambie kwamba mamba mwenye njaa atapoteza muda wa kutishiana na paka.
 
Paka kumchimba mkwara mamba inawezekana kabisa kwani mamba ni kiumbe anayetegemea ku-attack windo lake kwa kuvizia. Ni nadra sana mamba kukamata windo kwa mapambano ya ana kwa ana. Pili mamba anapokuwa nchi kavu uwezo wake wa kupambana unapunguwa kwa karibu 60%, laiti mpambano huu ungekuwa ndani ya maji ni wazi huyo paka angekuwa ni mshikaki mtamu sana kuwa huyo mamba kwani nina uhakika kama walivyo wanyama wengine wengi, paka huyo asingekuwa na jeuri kwa mamba wakiwa majini... Hata hivyo thanks kwa kuleta kiburudisho!!
 
Mi nadhani huyo paka ana ujomba na mzee Chui miraba (Tiger). So kampiga mkwara mamba kuwa akileta za kuleta atamwita mjomba wake.

Tiger_panthera_tigris_tigris_Bengal.jpg
 
Back
Top Bottom