Video: Padri Pascal Luhengo wa jimbo la Mahenge Morogoro amuomba msaada Rais Samia Suluhu baada ya kukimbia nchi na kwenda mafichoni

Narubongo

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
2,717
2,000
Bahati mbaya hulifahamu Kanisa Katoliki na ndiyo maana unaongea tu kwa mazoea! Ngoja nikufahamishe kidogo! Ishu iliyopo ni kwamba, kwa miaka nenda!

Mapadre wa Kanisa Katoliki wamekuwa na utaratibu wa kutafuta marafiki na wafadhili nje ya nchi wakati wanapokuwa Seminari kuu (Mafrateli) wakiwa katika hatua ya ushemasi, lakini pia wakiwa Mapadre!

Marafiki/Wafadhili hao huwasaidia katika masuala mbalimbali, kama kuwatumia fedha, magari kwa ajili ya kwenda kutolea huduma kwenye Vigango, nguo kwa ajili ya kuwagawia wenye mahitaji maalum, nk.

Hivyo kilichotokea kwa huyo Padre ni wizi wa kimtandao ambao ulifanywa na matapeli kwa msaada wa siri kutoka kwa baadhi ya watu walio mzunguka huyo Father, na wanao tambua fika ya kwamba ana marafiki/wafadhili wanao msaidia mara kwa mara.

Padre anataka haki itendeke! Hofu iko wapi? Kama ameshirikiana na hao matapeli, si vyombo husika vitakuja kutoa majibu baada ya kufanya huo upelelezi kwa kina na kuwatia nguvuni wahusika wote!
Yes padre ametoa ushahidi wote na namna fedha zilivyoingia na kutolewa bank, ametoa ushuhuda wa majina na nakala za vitambulisho vya waliotoa fedha wu na bank, mfano huyo mwenye account boa ni mtu anayefahamika na aliitwa akathibitisha kupokea fedha sasa unahitaji ushahidi gani tena au upelelezi gani hapo kama si mchezo mchafu
 

idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
24,261
2,000
Hii aya imenifikirisha Sana.

“Ni padri wa kwanza kutulalamikia, lakini na sisi tupo kama yeye, ambavyo kuna waumini ambao wanatenda dhambi kila siku, wanatubu mbele yake na kwenye madhabahu, lakini hajaweza kuwafanya wasiendelee kutubu. Kwa mantiki hiyo na sisi tunaendelea kumtafuta huyu mtu."
 

Isanga family

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
8,738
2,000
Aisee walifika sehemu mbaya sana yaani ujambazi kila sehemu daah Nchi ilikokua inakwenda kubaya mno Mungu katuepusha na mengi...
 

Malaika Mkuu

JF-Expert Member
Nov 5, 2014
868
1,000
Its very pissible wakafanya hivyo.
Niliibiwa simu nikarepirt kwao, wakaomba imei number nikawapa wakaomba fedha nikawapa laki nne.
Baadaye wakamkamata mhalifu, akawalipa millions, wakamwachia na hadi sasa wananichenga.
Nikaenda TCRA baada ya kuunganishwa na boss wangu bado wakadai mchezo uko kwa wazee wa kazi.
Hawafai hawafai hata kidogo.

Sent from my LG-F800S using JamiiForums mobile app
 

Bayyo

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,778
2,000
Unaongea utumbo,Yesu na Muhamad kwa nyakati tofauti na kwa maeneo tofauti waliwahi kukimbilia uhamishoni kuepuka kuuwawa.sembuse PadPadri
Duh, Yesu angekimbia asingesulubiwa msalabani.. labda huyo Muhamad alikimbia
 

T11

JF-Expert Member
Oct 11, 2017
4,967
2,000
Kuna mambo ya ajabu nchi hii na hii yote ni jiwe na tiss, polisi aliowapa mamlaka ya kuua kudhulumu
Duhjiwe alikutenda nini? Kwanza hayupo halafu mambo ya kutekana na wizi wa kimtandao umekujaje hapo
 

MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,562
2,000
Its very pissible wakafanya hivyo.
Niliibiwa simu nikarepirt kwao, wakaomba imei number nikawapa wakaomba fedha nikawapa laki nne.
Baadaye wakamkamata mhalifu, akawalipa millions, wakamwachia na hadi sasa wananichenga.
Nikaenda TCRA baada ya kuunganishwa na boss wangu bado wakadai mchezo uko kwa wazee wa kazi.
Hawafai hawafai hata kidogo.

Sent from my LG-F800S using JamiiForums mobile app
Pole sana Rushwa bado ipo Tanzania.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom