Video:Nyerere alipokutana na Keneth Kaunda gerezani na kushinikiza atoke

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,634
29,997
Habari,

Hii video imechukuliwa wakati Mwl Nyerere alipoenda Zambia na kukutana na rais wa wakati huo CHILUBA, ambaye alikuwa kamfunga Kaunda, Mwalimu Nyerere akaomba dakika 40 za mazungumzo na rais Chiluba, baada ya hapo akaomba kwenda kumuona rafiki yake Kaunda katika gereza alilofungwa.

Akafika akaonana naye, akakuta Kaunda yuko kwenye mgomo wa kula, muda wa kumuona ukaisha akaambiwa atoke akasema hebu tufunge sote hapa mi na bwana Kaunda, kama naondoka basi naye muachieni atoke, kama hatoki nitabaki naye hapa, ikabidi uongozi wa gereza uwasiliane na Rais Chiluba akasema anaomba mazungumzo na Mwl Nyerere wakayazungumza Kaunda akaachiwa.

KENETH KAUNDA KWA KAULI YAKE ALISEMA KILA LINAPOTAJWA JINA LA NYERERE NALIA NATOA MACHOZI SANA NA NINALIA.

Nasikia alimwambia kama umachi hii leo mizigo yenu pamoja na mafuta yenu kwenye bomba la TAZAMA utafute pa kuvipitisha. Na wakati huo huo Chiliba alikuwa na bifu na Dos Santos wa Angola, basi akawa hana pa kutokea.
Nyerere naye aliingilia mamlaka ya nchi nyingi mno
 
Nyerere naye aliingilia mamlaka ya nchi nyingi mno

Mkuu britanicca kumbuka Mwl Nyerere na Kaunda walikuwa mstari wa mbele kupinga ukoloni hasa kusini mwa Afrika wakati huo nchi nyingi zilikuwa bado chini ya utawala wa wazungu.Aliposikia rafiki yake,kiongozi mwenzake,mzee mwenzake..... katiwa ndani kwasababu za kijinga lazima angechukua hatua.

Ifahamike wazi wakati huo Mwl Nyerere alishaachia ngazi hakuwa Rais wala mamlaka yoyote ya kiutawala.Unaposema aliingilia mamlaka ya nchi nyingine nadhani unakosea sana.
 
Nasikia alimwambia kama umuaachi hii leo mizigo yenu pamoja na mafuta yenu kwenye bomba la TAZAMA utafute pa kuvipitisha. Na wakati huo huo Chiluba alikuwa na bifu na Dos Santos wa Angola, basi akawa hana pa kutokea.
Hebu weka vizuri hapa. Kwani kipindi Kaunda anawekwa ndani na Chiluba rais wa Tanzania alikuwa nyerere mpaka awe na uwezo wa kutishia kuzuia bidhaa za Zambia toka Dsm!!?
 
Hebu weka vizuri hapa. Kwani kipindi Kaunda anawekwa ndani na Chiluba rais wa Tanzania alikuwa nyerere mpaka awe na uwezo wa kutishia kuzuia bidhaa za Zambia toka Dsm!!?

Hizi ni tetesi za wakati ule. Rais alikuwa Mh. Benjamin Mkapa hivyo kuna uwezekano wa kuwa walishauriana na ndipo akaenda, na umbeya huu nilipewa na rafiki yangu Mzambia ambaye alikuwa mpinzani wa Chiluba.
 
Kumbukumbu zangu zinaniambia Chiluba ameingia madarakani wakati Tz rais ni Mwinyi
 
huku kwetu ukizungumiza ufisadi wa Kikwete mbele ya Magufuli anaweza akakukata makofi ukazimia ukajikuta umelazwa hospital ya taifa.
Mtu yeyote aliye Pata kibali kutoka kwa MAULANA kuongoza mamilioni ya watu anakuwa sio mtu wa kawaida . ..inatakiwa hekima kushuhulika naye . ..kumbuka Daudi na Sauli . ...Daudi alimwachia Mwenye Enzi Mungu ashuhulike na Sauli kwani Sauli alikuwa ni mpakwa mafuta wa Mwenye Enzi Mungu . ..tuwe na hekima katika mienendo yetu . .
 
Dah! Hata mm imenigusa sana, Ila pongezi kwa Mwl. Baba wa Taifa la Tanganyika! I real Love the Man Mr. Teacher for whatever what happens!
 
Nimeangalia chumba alichokua anaishi Kaunda nikapata huruma kimtindo.. Yaani Rais kuishi katika kile kichumba.. Sipati picha huko Rumande aliko Lema kukoje
 
Nyerere naye aliingilia mamlaka ya nchi nyingi mno
Kubwa kuliko yote ni hoja alizojenga UN kushinikiza CHINA ipewe hadhi ya KURA YA VETO ambayo initially walipewa zile nchi zilizokuwa kwenye kundi la washindi wakati wa WW2.

Wakati huo no nation could foresee that one day CHINA would endanger US position as World's Superpower. Jambo hilo ni bahati ya mtende kwa taifa la China hasa wakati huu ambapo foreign policy ya CHINA inavyokinzana na ile ya Marekani. Kwahiyo, CHINA ana nguvu ya ku-veto maamuzi yoyote kule UN(na mabaraza yake) ambayo yako kinyume na maslahi yake.

Jambo hili ni chungu mno kwa Marekani.
 
Mtu yeyote aliye Pata kibali kutoka kwa MAULANA kuongoza mamilioni ya watu anakuwa sio mtu wa kawaida . ..inatakiwa hekima kushuhulika naye . ..kumbuka Daudi na Sauli . ...Daudi alimwachia Mwenye Enzi Mungu ashuhulike na Sauli kwani Sauli alikuwa ni mpakwa mafuta wa Mwenye Enzi Mungu . ..tuwe na hekima katika mienendo yetu . .
Na sisi tutapata kibali kutoka kwa mungu kufuta hati ya shamba la Mkapa.
 
Back
Top Bottom