VIDEO: Mzee Kingunge atoa tathmini kuhusu Miaka 55 ya Uhuru wa Tanganyika

Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,433
7,055

==========

Mwanasiasa mkongwe nchini Kingunge Ngombale Mwilu atoa tathmini ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanganyika.

Akichambua masuala mbalimbali Mzee Kingunge ameelezea mambo yaliyofanywa na serikali ya awamu ya kwanza na kuzungumzia mambo kadhaa ya tawala zilizofuata.

Katika nyanja ya maendeleo ya kijamii Mzee Kingunge amesema kuwa kwa awamu ya kwnza ilinaanzia kwenye elimu na afya

Uchumi na kwa upande wa uchumi basi kwa wakati huo ilijumuisha wananchi woote kwa kazi kwa bidii.

Aidha Mzee Kingunge ameelezea kuwa kwa sasa taifa linaongozwa bila ya kufuata mipango ya maendeleo, wanachi wanataka maendeleo na viongozi wanataka maendeleo lakini kikwazo ni katika upangaji wa maendeleo.
 
Safi sana Mzee Kingunge Ngombale Mwiru. nadhani viongozi wanasiasa na wale wa maofisini/wizarani wasidhanikujifungia ndani ndiyo inawafanya wanajua sana mambo yote na hivyo kutoshirikisha wananchi ktk ngazi zote ili nchi ipate maendeleo kwa kasi kubwa zaidi.
 
Alifanya nini wakati ni waziri na mkuu wa mkoa. Watu wanataka waone wenzie wanafanye juu ya matarajio wakati wao walifanya chini ya kiwango.

Anaweza akaeleza kitu achoacha hapa Tanzania hatatukamkumbuka?
 
More than 30 years yupo serikalini na hakuna lolote la maana alilofanya. Wazee kama yeye huwa wananishangaza sana.
 
Mzee Kingunge ni aina ya wale wazazi waliokuwa wanaongoza shuleni kila somo lakini cha kushangaza hawakupata elimu na kuishia madarasa ya awali kabisa, kila akizungumzia shule utamsikia enzi zangu mimi.

Yeye atakumbukwa kwa lipi kama waziri na mkuu wa zamani, na kiongozi mwandamizi wa chama chao kilichoasisi ufisadi Tanzania?

Mzee Kingunge hajawahi kuwa mshauri mzuri kuanzia kwa serikali aliyoitumikia tangu akiwa kijana na mpaka leo na chama chake cha zamani.

Katika watu wanaotakiwa kuomba radhi kwa Watanzania Mzee Kingunge yupo na CCM wote.

Taratibu za chama zimekiukwa 2015 je 1995 na 2005 hazijakiukwa? Au kwasababu kulikuwa na ujinga wao wa kuachiana ndio ikambidi avute subira?

Nchi hii ina uongozi mbovu ila Kingunge alikuwa mbovu zaidi kama kina Msukuma tu, kama ni ujasiri alikuwa wapi kina Mbowe, Maalim, Mbatia, Lipumba walipokuwa wanaichachafya ccm na kujiweka mstari wa mbele kwenye mapambano?
 
Shikamoo Mzee, unanikumbusha Vita ya maji maji hivi mdachi alishindwa vile eeh!au ni babu zetu waliambulia kitanzi?
 
Mzee yuko vizuri. Kwa upande mwingine hope mambo yake ameyaweka vizuri kimaandishi otherwise kwa heshima kubwa aliyo nayo ccm hawakawii kufanya fujo wakidai ni mtu wao.
 
Hii Kweli Nitokee Vipi, Mzee Mbona Enzi Zile Ukiwa Kiongozi Mkubwa Hukuweza Hivi Vitu
 
Mzee Kingunge ni aina ya wale wazazi waliokuwa wanaongoza shuleni kila somo lakini cha kushangaza hawakupata elimu na kuishia madarasa ya awali kabisa, kila akizungumzia shule utamsikia enzi zangu mimi.

Yeye atakumbukwa kwa lipi kama waziri na mkuu wa zamani, na kiongozi mwandamizi wa chama chao kilichoasisi ufisadi Tanzania?

Mzee Kingunge hajawahi kuwa mshauri mzuri kuanzia kwa serikali aliyoitumikia tangu akiwa kijana na mpaka leo na chama chake cha zamani.

Katika watu wanaotakiwa kuomba radhi kwa Watanzania Mzee Kingunge yupo na CCM wote.

Taratibu za chama zimekiukwa 2015 je 1995 na 2005 hazijakiukwa? Au kwasababu kulikuwa na ujinga wao wa kuachiana ndio ikambidi avute subira?

Nchi hii ina uongozi mbovu ila Kingunge alikuwa mbovu zaidi kama kina Msukuma tu, kama ni ujasiri alikuwa wapi kina Mbowe, Maalim, Mbatia, Lipumba walipokuwa wanaichachafya ccm na kujiweka mstari wa mbele kwenye mapambano?
Mbona unatuchanganya. Mzee si yupo Chadema au amesharudi ccm
 
Mzee amekula maisha yake yote yupo karibu na uongozi wa juu wa nchi kama kiongozi lakini hatujui yeye kama yeye aliifanyia nini nchi hii. Kama ni kufeli kwa nchi na yeye ni mmojawapo aliechangia. Sasa ilikuaje akasema ccm imeishiwa pumzi wakati yeye alikua kada wake.Hana lolote na ndio maana hata Nyerere hakuweza kumtumia sana kwa sababu ya uwezo wake mdogo
 
Alifanya nini wakati ni waziri na mkuu wa mkoa. Watu wanataka waone wenzie wanafanye juu ya matarajio wakati wao walifanya chini ya kiwango.

Anaweza akaeleza kitu achoacha hapa Tanzania hatatukamkumbuka?
Kama umemsikiliza, kasema Elimu haikuwepo, asilimia 82% ya Watanganyia walikuwa hawajui kusoma na kuandika, waliwapa elimu asilimia 93% wakajua kusoma na kuandika.

Unahoji walifanya nini, kwasababu wewe ni CCM mnajua mnavyo Fanya madudu ndio unapinga hadi ukweli!

Ujuaji wenu wa kutokutaka kushilikisha watu mnatuchelewesha,
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom