- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Wakuu katika pitapita zangu huko mitandaoni leo nimekutana na hii video ambayo inasemekana kuwa ni ya Uganda na mwanamke mmoja anaonekana kumpiga kofi polisi, je kuna uhalia upi hapa wakuu?
- Tunachokijua
- Jeshi la polisi ni moja kati ya vyombo vya usalama ambavyo vimekabidhiwa jukumu la kulinda usalama wa raia na mali zao. Majukumu ya Jeshi la Polisi nchini Uganda yameainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Uganda na Sheria ya Jeshi la Polisi la Uganda, majukumu hayo ni pamoja na kulinda maisha ya watu na mali, kuzuia na kubaini uhalifu, kudumisha sheria na utulivu, pamoja na kuhakikisha usalama wa jumla na usalama wa umma nchini Uganda.
Kumekuwapo na video ambayo imesambaa sana mtandaoni ikiwaonesha wanawake wawili mmoja kati ya hao anaonekana akimpiga kofi afisa wa jeshi la Polisi aliyevalia sare za jeshi la polisi la Uganda. Wasiwasi ju ya video hiyo ni kuwa imerekodiwa nchini Uganda na ni halisi siyo maigizo?
Ni upi uhalisia wa video hiyo?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia Google Reverse image search umebaini kuwa video hiyo ilichapishwa kwa mara ya kwanza mtandaoni tarehe 18 Oktoba 2024, rejea hapa na hapa. Aidha video hiyo ni ya kweli na ilirekodiwa nchini Uganda ambapo mwanamke mmoja alidaiwa kumshambulia Afisa wa jeshi la polisi kwa kumpiga makofi.
Aidha Kupitia ukurasa rasmi wa mtandao wa X jeshi la polisi nchini Uganda lilichapisha taarifa kutokana na tukio hilo ambapo ilibainisha kuwa afisa wa jeshi hilo kutoka kituo cha polisi barabara ya Jinja alijaribu kulisimamisha gari jeupe aina ya Toyota Land Cruiser lenye usajili wa namba UBM 439T lilokuwa likiendeshwa na mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Mercy Timbitwire Bashisha aliyetuhumiwa kusababisha ajali akidaiwa kugoma kusimama baada ya kusimamishwa.
Taarifa hiyo iliongeza kuwa Baada ya kufika katika eneo la kuongozea magari Lugogo jijini humo aliegesha gari hilo katika eneo la Uganda Manufacturers Association na kulifunga huku afisa huyo wa polisi akimtaka kuonesha kibali cha kuendesha gari lakini badala yake mwanamke huyu alionekana kumshambulia afisa huyo.
Hata hivyo Bashisha, ambaye alikuwa pamoja na mwanamke mwingine wakati wa tukio hilo aliyejulikana kwa jina la Bernardine Abangira, walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Nakawa na kusomewa mashtaka sita dhidi yao ambayo ni wizi, kushambulia, kuendesha gari kizembe, kushindwa kutii agizo la afisa wa jeshi la polisi na kutumia gari bila Bima
Mwendesha mashtaka, Mariam Kuluthum aliiambia mahakama kuwa Timbitwire Mercy na Abangira Bernadine walitenda makosa hayo Oktoba 18, 2024 katika Uwanja wa Maonyesho wa UMA, Kitengo cha Nakawa; Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Makerere kando ya barabara ya Port Bell mjini Kampala na huko Lugogo kando ya barabara kuu ya Kampala- Jinja katika Wilaya ya Kampala.
Kesi hiyo ilihairishwa tena mpaka Novemba 04, 2024 ambapo Mahakama ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Nakawa ilimuachilia kwa dhamana Bashisha. Mshitakiwa huyo alipandishwa tena kizimbani mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Elias Kakooza katika eneo la Nakawa lakini bado alikana shtaka na kuachiwa kwa dhamana ya fedha taslimu shilingi milioni 7.5 baada ya kupata wadhamini wake ni wa kutosha.
Aidha upande wa mashtaka ulikamilisha kuwasilisha ushahidi mbele ya mahakama lakini kesi hiyo ilihairishwa tena mpaka Disemba 04, 2024.