Video: Mwanamke abakwa na kuzikwa akiwa mzima...polisi wamfukua na kukuta amekwishafariki

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,082






Matukio ya kikatili yameendelea kutikisa nchini Nigeria baada ya mwanamke mmoja kubakwa na kuzikwa akiwa mzima....


Taarifa toka katika mitandao ya kinigeria zinadai kuwa mwanamke huyo alibakwa na kisha wabakaji wakamfunga miguu na mikono.....

Zoezi la kumfukua likiendelea.....

Mwili wa dada huyo ukifukuliwa

Mwili umekwisha fukuliwa, bahati mbaya dada huyo amekwisha fariki....
Baada ya kumfunga,Mashetani hao walichimba shimbo porini walikotekeleza unyama huo na kisha kumzika akiwa hai ili kuficha ushahidi.....

Jeshi la polisi nchini humo lilifanikiwa kuipata habari hiyo masaa 12 baada ya mwanamke huyo kuzikwa akiwa hai....

Zoezi la kumfukua dada huyo lilianza, lakini bahati mbaya dada huyo alikuwa amekwisha fariki

.KAMA HUNA MOYO WA KIJASIRI USIANGALIE


Ifuatayo ni video ya tukio hilo Bonyeza hapa

http://www.mpekuzihuru.com/2013/06/video-mwanamke-abakwa-na-kuzikwa-akiwa.html


 
Yaani huu ukatili mkubwa. Upumzike kwa Amani dada.
 
yaani hadi machozi yananitoka jamani, adhabu ya Mungu kali inakuja juu yao, tena pole pole na wanadamu wakiona na kushuhudia
 
Watu kama hao adhabu yao,unawafunga kwenye mti halafu watu maarufu kwa kulenga mishale wanaletwa,anaangukiwa na mvua ya mishale anakuwa kama kale ka-mnyama "porcupine" .Hii midude inaudhi sana.Pumzika kwa amani Dada yetu.
 
Inasikitisha sana ila damu ya huyu dada itafuata mmoja baada ya mwingine tena muda si mrefu.
 
Jamani... Hivi binaadam inakuaje Unakua na roho mbaya kwa binadam mwenzako. Looh Mungu awashinde na wao waonje uchungu kuliko walompa mwenzao
 
Back
Top Bottom