Video: Mwalimu anayetuhumiwa Kulawiti, Kubaka Watoto wa Shule ya Msingi asomewa MASHITAKA 6 MAHAKAMANI

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,455

Mwalimu wa Shule ya Msingi Global International School iliyopo Mtaa wa Vijana, Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chacha Magere (26), amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni kwa tuhuma za kubaka, kuwalawiti na kuwashambulia kwa aibu baadhi ya wanafunzi wake anaowafundisha.

Jumla amesomewa mashtaka sita.

Mwendesha Mashtaka wa Wakili wa Serikali, Hilda Kato ameeleza mbele ya Hakimu Mkazi Frankoo Kiswaga kuwa mtuhumiwa kwa nyakati tofauti Januari na Mei 2022 akiwa shuleni kwake aliwabaka na kulawiti wanafunzi wake wa kike (majina yamehifadhiwa) kinyume na sheria.

Aidha, Mwendesha Mashtaka Wakili wa Serikali Daisy Makalala amedai mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Aron Lyamuya kuwa mtuhumiwa akiwa kazini kwake alimlazimisha mwanafunzi wake wa kike kumnyonya sehemu zake za siri kwa lengo kujiridhisha kingono.

Shtaka lingine ni kumdhalilisha kingono mwanafunzi wake ambapo Mwendesha Mashtaka Daisy Makalala amedai katika tarehe hizo Mwalimu huyo mkazi wa Mwananyamala A akiwa shuleni kwake aliviingiza vidole vyake sehemu za siri za mwanafunzi wake wa kike (Jina linahifadhiwa) kwa lengo la kujiridhisha kingono.

Mtuhumiwa amekana tuhuma zinazomkabili na amepelekwa rumande baada ya upande wa mashitaka kuweka kiapo cha kupinga dhamana.

Upelelezi wa kesi hizo umekamilika na kuahirishwa mpaka Juni 13, 2022 ambapo yataanza kusomwa maelezo ya awali.

Pia soma hapa: Kinondoni: Tuhuma za Mwalimu kulawiti na kubaka watoto wa Shule ya Msingi, Waziri atoa siku 7 za uchunguzi
 
Alipata Wakili Kama Majura Magafu, Huyo Ticha anachomoka, Facts Za Hyo Kesi Zinachanganya Sana

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Walawiti utawajua tu! Ombea lisikukute hili kwa mwanao! utatamani ukate panga kichwa cha mtu!

Watoto ni malaika! unamharibia future yake tokea udogo wake!

Ukute mwalimu ni mwathirika! mie wala asingefika mahakamani!

Mngeokota vipande kila kukicha mpaka wiki mbili zinapita mnakamilisha mwili mzima ndio mkazike.
 
Na yeye abakwe na njemba zenye miili kama tano iwe fundisho.
 
walawiti utawajua tu! Ombea lisikukute hili kwa mwanao! utatamani ukate panga kichwa cha mtu!

watoto ni malaika! unamharibia future yake tokea udogo wake!

ukute mwalimu ni mwathirika! mie wala asingefika mahakamani!

mngeokota vipande kila kukicha mpaka wiki mbili zinapita mnakamilisha mwili mzima ndio mkazike
Acha vitisho wakati hata kivuli chako unakiogopa, yaani nakuona ni muumini wa kangaroo courts maana umeshahukumu! Hii ni kesi ambayo tunategemea kuwa kutakuwa na witness na DNA results na report za wataalamu mbalimbali including Doctors na psychology one, huyu ni suspect sio convicted ana haki zote kama mimi na wewe.
 
Acha vitisho wakati hata kivuli chako unakiogopa, yaani nakuona ni muumini wa kangaroo courts maana umeshahukumu!,hii ni kesi ambayo tunategemea kuwa kutakuwa na witness na DNA results na report za wataalamu mbalimbali including Doctors na psychology one, huyu ni suspect sio convicted ana haki zote kama mimi na wewe
Kesi kama hizi asilimia ya kusingiziwa ni 0.
 
Back
Top Bottom