VIDEO - Msiba Kenya, Moto Waua Watu 120

jamadari

JF-Expert Member
Feb 13, 2010
295
92
5945954.jpg

Zaidi ya watu 120 wameteketea kwa moto Kenya
Monday, September 12, 2011 8:12 PM
Mtu aliyewasha sigara wakati watu wakiiba mafuta toka kwenye bomba la mafuta lililopasuka alisababisha moto mkubwa uliopelekea vifo vya zaidi ya watu 120 leo asubuhi jumatatu jijini Nairobi, Kenya.
Miili ya watu zaidi ya 120 ilitapakaa kwenye maeneo ya kitongoji cha Sinai jijini Nairobi baada bomba la mafuta kulipuka na kusababisha moto mkubwa uliua watu na kuziteketeza nyumba nyingi za kitongoji hicho cha watu mafukara.

Msemaji wa polisi, Kenya bwana Thomas Atuti alisema kuwa idadi ya waliofariki kutokana na moto huo ni zaidi ya watu 100.

Watu wengine wapatao 112 waliwahishwa kwenye hospitali ya taifa ya Kenyatta miili yao ikiwa imeungua vibaya sana.

Chanzo cha moto huo ni sigara iliyowashwa na mmoja wa watu waliojitokeza kuiba mafuta toka kwenye bomba la mafuta lililokuwa likikatiza kitongoji cha Sinai kuelekea uwanja wa ndege.

Bomba hilo lilikuwa likivuja mafuta hali iliyowafanya baadhi ya watu wamiminike na ndoo zao kuja kukinga mafuta.

Mlipuko mkubwa ulioambatana na moto mkubwa uliosambaa kwenye kitongoji hicho ulipelekea watu wengi kuungua na moto. Watoto wengi ndio waliofariki kwenye moto huo.

Baadhi watu walijitosa kwenye mto ili kunusuru maisha yao lakini wengi wao walisombwa na maji.

Angalia VIDEO ya tukio hilo chini.








<tbody>
</tbody>



huu wizi wa Mafuta bado watu hajajifunza mambo yaliyotokea Jamhuri ya Congo?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom