Video: Mh Mansour Waziri asikuwa na wizara maalum Akitoa Maoni ya katiba mpya Muungano wa mkataba

Baraghash,

..Mh.Ismail Jussa katika maandishi yake alisema kwamba EAC na EU ni mifano ya muungano wa mkataba.

..mapendekezo yangu kwamba tunataka Tanganyika huru na Zanzibar huru itakayofuatiwa na muungano wa mkataba kupitia EAC ni katika kumuunga mkono Mh.Ismail Jussa.

..kuhusu kuhamasishana kuipata Tanganyika huru sisi tuko nyuma kidogo kulinganisha na wenzetu wa Zanzibar. Pamoja na hayo tutaendelea kuhamasishana kupitia njia mbalimbali kama mitandao, magazeti, mpaka kufikia hatua mliyofikia nyinyi. Kumbuka hata nyinyi zanzinet, mzalendo, wamekuwa na mchango mkubwa ktk harakati zenu.

..hata huku Tanganyika muungano umesababisha wakimbizi wa ki-Tanganyika ktk nchi mbalimbali. Wakimbizi hao ni makini na wasomi wakubwa ktk nchi kama Namibia, Botswana, Zimbabwe, Canada, Australia, na kwingineko.

..mwisho, na sisi pia hatutaki kutawaliwa. kuna wa-ZNZ wamepewa madaraka ktk wizara zisizohusiana na muungano. Kodi za wa-Tanganyika ndizo zinazotumika kuendesha serikali ya muungano wakati Zanzibar haichangii chochote. wa-Tanganyika pia wamekuwa wakibebeshwa mzigo wa kulipa madeni ya Zanzibar kwa Tanesco, pamoja na kulipa mishahara ya watumishi wa SMZ. Kwa kifupi tunataka Tanganyika iachwe ipumue.

Joka Kuu,
Nadhani tunazungumza lugha moja. Ukiona Mke anakufanyia vitimbi, hakuheshimu,anainda, utukutu,hkusaidii, ndio HAKUTAKI HUYO Lakini nyie Watanganyika maudhi yote hayo bado nyimbo ileile MUUNGANNO UDUMU . mbona sisi hatutafuni meno tunasema HATUTAKI MUUNGANO WAZIWAZI. Tena mnakasirika na kutumia vyombo vyenu vya dola kutupiga na kutunynyasa? JAMANI HATUTAKI MUUNGANO HAMSIKIII? Chukueni kila kitu chenu pamoja na wakimbizi wa uchumi kutoka Tanganyika (Makahaba) na sisi TUPUMUE
 
Baraghash,

..kuna taratibu zinazotakiwa kufuata ktk kuuvunja muungano.

..vyombo sahihi vya kushughulikia tatizo hili ni BARAZA LA WAWAKILISHI na BUNGE LA MUUNGANO.

..tatizo ni kwamba kwa upande wa ZNZ mmeamua kutumia UAMSHO kuupinga muungano, na sote tunaelewa kwamba chombo hicho siyo rasmi.

..vurugu unazoziona ni matokeo ya kutumia njia sizizo rasmi kujaribu kuvunja muungano. kama una kumbukumbu mwaka 1993/94 wa-Tanganyika, kupitia wabunge wetu, tulidai serikali ya muungano na hakuna mtu yeyote yule aliyeumizwa kwasababu tulifuata taratibu na sheria.

..kitendo chenu cha kutumia taratibu zisizo rasmi ndiyo kinatoa nafasi kwa mambo ya kihuni-huni kufanyika dhidi ya wananchi. upande unaopinga muungano unajenga chuki, wakati ule unaounga mkono ukitumia vyombo vya dola kuumiza wananchi.

..wabunge na wawakilishi, haswa wa chama cha CUF, wangekuwa na UJASIRI pamoja na BUSARA wangepeleka hoja na malalamiko yao ktk baraza la wawakilishi au bunge la muungano.

..tatizo lingine ni kwamba wa-Tanganyika wakisema hawataki muungano, au muungano hauwatendei haki, wamekuwa wakipokea MATUSI mazito-mazito toka kwa wa-ZNZ. sijui kama unakumbuka matusi yaliyoelekezwa kwa Mh.TUNDU LISSU pale alipoelezea kasoro zilizopo ktk muungano wetu, na kupendekeza kurejeshwa kwa serikali ya Tanganyika.
 
Last edited by a moderator:

Kwanini tundu asihoji sheria iliyotumika kuifuta tanganyika?huoni kuwa hilo ni ttzo kuona bungeni tanganyika haimo?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom