Video: Mh Mansour Waziri asikuwa na wizara maalum Akitoa Maoni ya katiba mpya Muungano wa mkataba

GHIBUU

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
4,323
2,000
[video]http://blip.tv/mzalendonet/tunaoutaka-ni-muungano-wa-maslahi-kiuchumi-sio-vitunguu-na-mbatata-mansour-6454456[/video]
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
20,903
2,000
..Mansour hana nia njema.

..kupitia muungano huu ZNZ inapewa umeme bure toka Tanganyika halafu watu kama Mansour wanabeza kwamba huduma na misaada kama hiyo is just "vitunguu" na "mbatata."

..lakini hata kama ni "vitunguu" na "mbatata," hivi Mansour haioni kwamba ZNZ inafaidika kwa kuagiza vyakula hivyo ndani ya muungano, kuliko nje ya muungano??

..Nje ya muungano, na ZNZ ikiwa na sarafu yake yenyewe, basi italazimika kuagiza "vitunguu" na "mbatata" kwa kutumia FEDHA ZA KIGENI.
 
Magogoni

New Member
Jan 7, 2011
2
0
Ndugu yangu bora nyamaza usizungumze usichokijua.Hakuna umeme ambao Zanzibar inapata bure kutoka Bara,na bei ambayo Zanzibar inauziwa umeme ni kubwa kuliko ule umeme unaouzwa kwa wananchi wa Tanganyika.Pili sisi kununua vitunguu kwa pesa za kigeni tushazowea tulikuwa tunaagiza vitunguu kutoka India kwa hizo pesa za kigeni siyo vitunguu vibovu kutoka Bara.Wewe jibu hoja za Mansour kuliko ukawa unaandika utumbo wa jambo usilolijua.
 
Kadogoo

JF-Expert Member
Feb 26, 2007
2,072
1,195
..Mansour hana nia njema.

..kupitia muungano huu ZNZ inapewa umeme bure toka Tanganyika halafu watu kama Mansour wanabeza kwamba huduma na misaada kama hiyo is just "vitunguu" na "mbatata."

..lakini hata kama ni "vitunguu" na "mbatata," hivi Mansour haioni kwamba ZNZ inafaidika kwa kuagiza vyakula hivyo ndani ya muungano, kuliko nje ya muungano??

..Nje ya muungano, na ZNZ ikiwa na sarafu yake yenyewe, basi italazimika kuagiza "vitunguu" na "mbatata" kwa kutumia FEDHA ZA KIGENI.

yaani wewe bado una fikra zile za kidumu enzi za nyerere kuhusu fedha za kigeni! we unathamini sana fedha za kigeni kuliko zetu sio!
 
Mlengo wa Kati

JF-Expert Member
Feb 16, 2011
2,731
0
Tuta endelea kuitawala zanzibar,nia tunayo na uwezo tunao,wakibaki wao peke yao watachinjana kwanza hawapendani kati ya unguja na pemba! zanzibar ni koloni letu la kudumu!
 
Kadogoo

JF-Expert Member
Feb 26, 2007
2,072
1,195
Tuta endelea kuitawala zanzibar,nia tunayo na uwezo tunao,wakibaki wao peke yao watachinjana kwanza hawapendani kati ya unguja na pemba! zanzibar ni koloni letu la kudumu!

Rorya na Musoma watu wanachinjana kila siku tumeweza kumaliza tatizo? jee, albino wanao chunwa ngozi kila siku huku Tanganyika tumeweza kuwaokoa?
 
GHIBUU

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
4,323
2,000
..Mansour hana nia njema.

..kupitia muungano huu ZNZ inapewa umeme bure toka Tanganyika halafu watu kama Mansour wanabeza kwamba huduma na misaada kama hiyo is just "vitunguu" na "mbatata."

..lakini hata kama ni "vitunguu" na "mbatata," hivi Mansour haioni kwamba ZNZ inafaidika kwa kuagiza vyakula hivyo ndani ya muungano, kuliko nje ya muungano??

..Nje ya muungano, na ZNZ ikiwa na sarafu yake yenyewe, basi italazimika kuagiza "vitunguu" na "mbatata" kwa kutumia FEDHA ZA KIGENI.

Kweli shule muhimu, na bahati mbaya waziri wa elimu Mugulo hana elimu ya kuwaongoa wasiokuwa na elimu kwa vile elimu yake ni duni, watanzania/watanganyika mutaendelea kuwa samaki au vifuu.

Rudi shule
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
20,903
2,000
GHIBUU, Kadogoo,

..jamani jaribuni kuwa na UTU na SHUKURANI.

..majuzi Bilali amepewa bil 32 na serikali ya Tanganyika kwa ajili ya maendeleo ya ZNZ.

..kabla ya hapo tuliwafutieni deni mlilolimbikiza Tanesco.

..mara kadha wa kadha tumekuwa tukilipa mishahara ya SMZ.

..pia huku Tanganyika kuna waZNZ 350,000++ wanaishi na kufanya shughuli za kiuchumi.

..Tanganyika ndiyo nchi pekee dunia iliyohifadhi wakimbizi wengi zaidi wa kiuchumi toka ZNZ.

..ni ukosefu wa shukurani, na uongo wa waziwazi, kudai yote hayo ni "vitunguu" na "mbatata."

NB:

..majuzi hospitali ya serikali ZNZ imeshindwa kulisha chakula wagonjwa.

..hivyo vihela vyenu kidogo vya kigeni tumieni kwa mambo ya maana kama uwekezaji kwenye viwanda, na siyo kuagiza chakula. masuala ya importation ya chakula ur more advantaged kama mkiagiza toka Tanganyika kwa kutumia LOCAL CURRENCY.

cc: Nguruvi3
 
Last edited by a moderator:

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,919
2,000
Joka kuu umesahau kitu, hata Rais Shein amekiri kuwa wanasoma bure!
Hawana bajeti ya elimu ya juu au ulinzi
Mafao ya uzeeni ni kutoka Dar
Ajira za bure na wote wamehamia Mikocheni hadi wabunge wao ambao wanapaswa kuishi Zanzibar wapo Dar wanakula raha.

Unajua hawa watu ni viumbe wa ajabu sana. Endapo wanadhani wanaonewa tumewapa kila mbinu, hawataki
Bado tu wanang'ang'ana na muungano wa mkataba. Hatutaki sisi na wala hatuihitaji Zanzibar

Tumewapa data za Benki kuu. Revenue yao kwa mwezi ni bilioni 10 pungufu ya wilaya ya Ilala.
Tanganyika Revenue ni Bilioni 790 kwa mwezi, zaidi ya bajeti ya Zanzibar ya mwaka. In other words revenue ya Tanganyika ya mwezi November 2012 ni bajeti ya miaka 10 ya Zanzibar, nani aende kuiba kule? Nani awatake hawa na kwa lipi.

Wakitaka mkataba kwanza wawe na adabu wafunge midomo maana hawana chochote cha kumsaidia mtanganyika halafu tutawapakata kama tulivyowapakata miaka nenda miaka rudi.

Nani amewapa ZNZ haki ya kuamua aina ya ushirikiano? Kwa sababu zipi?
 
Mkwaruzo

JF-Expert Member
Feb 21, 2011
566
195

Kwanini lakini?
Mnatusaidia ili tuwape shukurani? Au ndiyo ulimbukeni huo?
Hakuna msaada wa lazima, hizo pesa mnazotoa mnawapa wahafidhina kwa maslahi yenu wenyewe. Kama mna hamu ya kusaidia mbona mnawaondosha wakimbizi kwa nguvu? Hebu tuachieni basi
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
20,903
2,000
Mkwaruzo,

..hivi UMEME tunaowapa bure unatumiwa na wahafidhina peke yao, wananchi wa kawaida hawapati huduma hiyo?

..je, waZNZ zaidi ya 350,000 wanaoishi Tanganyika na kufaidika kwa fursa za ajira na biashara wote hao ni wahafidhina??

..mimi naunga mkono muungano uvunjwe, lakini ingependeza kama tungetumia ustaarabu na hoja za ukweli, kuliko uzushi na hoja za jumla-jumla alizokuwa akijenga Mansour Yusuf Himid.
 
Last edited by a moderator:

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,919
2,000
Kwanini lakini?
Mnatusaidia ili tuwape shukurani? Au ndiyo ulimbukeni huo?
Hakuna msaada wa lazima, hizo pesa mnazotoa mnawapa wahafidhina kwa maslahi yenu wenyewe. Kama mna hamu ya kusaidia mbona mnawaondosha wakimbizi kwa nguvu? Hebu tuachieni basi
Ndugu yangu, Tanzania ni nchi pekee iliyowahi kutoa Uraia kwa wakimbizi 160,000 katika historia ya dunia kwa wakati mmoja tu.
Achilia hayo Tanzania imetoa msaada kwa nchi zote ikiwa ni pamoja na kuwahifadhi wakimbizi.
Hatufukuzi wakimibizi kwasababu tunao wakimbizi wa zanzibar wapatao 350,000, itakuwa ni uonevu kuwafukuza Wanyarwanda 80,000 tena wasiotumia rasilimali yoyote kama wale 350,000.

Kuhusu kuachiwa, nadhani wewe ni mgeni katika ukumbi huu. JF wametoakila aina ya msaada ili 'muachiwe''.
Wazanzibar wamebaki na muungano wa mkataba hawataki kusikia neno vunja muungano. Nani king'ang'anizi?

Umemsikia Mansour akikiri kwa ulimi wake kuwa wanataka muungano, sasa mtu anayetaka muungano aachiwe kivipi tena wakati yeye anautaka muungano!

Umemsikia Mansour anasema anataka mkataba, sasa mkataba wa nini nanyi mnataka kuachiwa. Utaachiwaje ukiwa katika mkataba.

Mansour amesema anataka ushirikiano katika ulinzi. Hii maana yake ni kuwa wanataka wapewe ulinzi wa bure kama wanavyopewa elimu, nishati na mishahara.

Mansour amejichanganya aliposema mkataba wa mzee Karume ndio wanaoutaka. Sasa mkataba wa muungano ni wa nini tena wakati wa mzee Karume upo bado?

Anasema ZNZ inataka self determination, endapo wanataka hivyo kwanini anaomba mkataba wa muungano tena.

Katika kuonyesha kuwa ZNZ ina viongozi wa ajabu na ambao hatujui uwaziri wanaupataje, Mansour anasema hataki kusikia faida za muungano wa mbatata na vitunguu. Hapo hapo analalamika kuwa watu wa jimboni kwake hawawezi kuingiza TV bara aua Magari. Mansour anafahamu kuwa katika makontena 800 yanayopakuliwa ZNZ 750 yanabeba bidhaa kwa soko kubwa la Tanganyika. Kiongozi huyu asiye na maono halioni hilo kama faida ya muungano.

Sijui amesoma wapi, ninachojua ni kuwa asilimia 98 ya WZNZ viongozi na wafanyakazi wamesoma kwa kodi za Mtanganyika tena bure na nafasi za upendeleo hata kama alikuwa kilaza. No wonder ndio maana tuna majuha kama Mansour

Mnasour amesema anataka muungano kama wa EU. Sijui ZNZ inasomesha nini huko skuli maana EU ni jumuiya na si muungano. Kwa mantiki hiyo anachokiataka ni kuwa na EAC au SADC. Lakini kwa kuhofia neno vunja muungano bado Wazanzibar wameng'ang'ana na muungano wa mkataba ambao sisi tunasema mwisho ni Chumbe.

Upuuzi huo hautavuka bahari, na ukivuka uvushwe na Wazanzibar kwa sharti kuwa Adabu na heshima mbele, kidomo domo mwisho chumbe.

Anasema EU kuna wanachama wenye nchi zenye watu 20,000. Huu kama ndio uzanzibar na usomi wa ZNZ basi kuna tatizo zaidi ya muungano. Hivi huyu juha anajua EU kweli.

Halafu anasema anataka muungano wa haki na usawa, sasa nani anayetakiwa adai haki, yule anayening'inia mgongoni au yule aliyembeba? Halafu Mansour na elimu yake hajiulizi bajeti yake ya miaka 10 ni sawa na kusanyao la mwezi la Tanganyika, usawa utatoka wapi?

Kama alivyo Ahmed na Maalim Seif, Mansour ameshindwa kutaja hayo mambo ya mkataba ni yapi. Ameishia kutueleza kuhusu Hong Kong na Makao, sijui kama huyu Waziri wa Kizanzibar aliwahi kukaa darasani na kusoma historia, jiografia na elimu ya uraia. Huwezi kufananisha chungwa na matembele waziri Mansour! Too low kwa waziri.

Mwisho, Wazanzibar wakae wakielewa kuwa muda wa kuwaendekeza na mdomo juu sasa basi.
Zanzibar inaihitaji Tanganyika kwa namna yoyote ile ndio maana wamepewa panga hakuna anayethubutu kulitumia.
Hakuna anayesimama na kusema vunja muungano, wamebaki kuitisha makongamano ya kudanganyana.

Tanganyika tunasema ZNZ hamna haki ya kuchagua aina ya muungano kwasababu muungano wowote ule ninyi kama ZNZ hamuwezi kuweka kitu cha maana mezani. Kwa bilioni 10 kwa mwezi mna kitu gani. Si afadhali tufanye muungano wa mkataba na Bakhresa!

Muungano mnaoutaka ni kuhemea na hapo ndipo tunajeuri ya kuwaambia bila kificho Tulieni mapakatwe! Mumeshindwa kutamka neno vunja muungano hamna lolote la maana la kusema zaidi ya hadithi. Hadithi mwisho chumbe! ukivuka bahari kama wale 350,000 adabu mbele, heshima kwanza.

LET ZNZ GO!
 
GHIBUU

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
4,323
2,000
Mkwaruzo,

..hivi UMEME tunaowapa bure unatumiwa na wahafidhina peke yao, wananchi wa kawaida hawapati huduma hiyo?

..je, waZNZ zaidi ya 350,000 wanaoishi Tanganyika na kufaidika kwa fursa za ajira na biashara wote hao ni wahafidhina??

..mimi naunga mkono muungano uvunjwe, lakini ingependeza kama tungetumia ustaarabu na hoja za ukweli, kuliko uzushi na hoja za jumla-jumla alizokuwa akijenga Mansour Yusuf Himid.

Kuridhisha watawala na watawaliwa. Hujui wewe kula na kipofu ? Kwa taarifa yako ukiangalia wanaongoza serikali wote wanatoka chama kimoja,sasa unafikiri serikali itaendeshwa vipi ? Sisi umeme tunalipia sasa unaposema sisi tunatumia bure sikuelewi, mahafidhuna wanaongoza serikali na hao hao ccm, pengine deni wanalipana mlangowa nyuma ili watawaliwa waendelee kutawaliwa na watawala nao waendelee kutawala.
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
20,903
2,000
GHIBUU,

..kwa taarifa yako umeme mnaulipia kwa bei ya chini kuliko wa-Tanganyika.

..pia serikali yenu huwa hailipi chochote kwa Tanesco, na serikali ya muungano kwa kutumia kodi ya wa-Tanganyika hulipa madeni yenu.
 
Last edited by a moderator:

Nurdin moh'd

JF-Expert Member
Nov 1, 2012
367
0
Ndugu yangu, Tanzania ni nchi pekee iliyowahi kutoa Uraia kwa wakimbizi 160,000 katika historia ya dunia kwa wakati mmoja tu.
Achilia hayo Tanzania imetoa msaada kwa nchi zote ikiwa ni pamoja na kuwahifadhi wakimbizi.
Hatufukuzi wakimibizi kwasababu tunao wakimbizi wa zanzibar wapatao 350,000, itakuwa ni uonevu kuwafukuza Wanyarwanda 80,000 tena wasiotumia rasilimali yoyote kama wale 350,000.

Kuhusu kuachiwa, nadhani wewe ni mgeni katika ukumbi huu. JF wametoakila aina ya msaada ili 'muachiwe''.
Wazanzibar wamebaki na muungano wa mkataba hawataki kusikia neno vunja muungano. Nani king'ang'anizi?

Umemsikia Mansour akikiri kwa ulimi wake kuwa wanataka muungano, sasa mtu anayetaka muungano aachiwe kivipi tena wakati yeye anautaka muungano!

Umemsikia Mansour anasema anataka mkataba, sasa mkataba wa nini nanyi mnataka kuachiwa. Utaachiwaje ukiwa katika mkataba.

Mansour amesema anataka ushirikiano katika ulinzi. Hii maana yake ni kuwa wanataka wapewe ulinzi wa bure kama wanavyopewa elimu, nishati na mishahara.

Mansour amejichanganya aliposema mkataba wa mzee Karume ndio wanaoutaka. Sasa mkataba wa muungano ni wa nini tena wakati wa mzee Karume upo bado?

Anasema ZNZ inataka self determination, endapo wanataka hivyo kwanini anaomba mkataba wa muungano tena.

Katika kuonyesha kuwa ZNZ ina viongozi wa ajabu na ambao hatujui uwaziri wanaupataje, Mansour anasema hataki kusikia faida za muungano wa mbatata na vitunguu. Hapo hapo analalamika kuwa watu wa jimboni kwake hawawezi kuingiza TV bara aua Magari. Mansour anafahamu kuwa katika makontena 800 yanayopakuliwa ZNZ 750 yanabeba bidhaa kwa soko kubwa la Tanganyika. Kiongozi huyu asiye na maono halioni hilo kama faida ya muungano.

Sijui amesoma wapi, ninachojua ni kuwa asilimia 98 ya WZNZ viongozi na wafanyakazi wamesoma kwa kodi za Mtanganyika tena bure na nafasi za upendeleo hata kama alikuwa kilaza. No wonder ndio maana tuna majuha kama Mansour

Mnasour amesema anataka muungano kama wa EU. Sijui ZNZ inasomesha nini huko skuli maana EU ni jumuiya na si muungano. Kwa mantiki hiyo anachokiataka ni kuwa na EAC au SADC. Lakini kwa kuhofia neno vunja muungano bado Wazanzibar wameng'ang'ana na muungano wa mkataba ambao sisi tunasema mwisho ni Chumbe.

Upuuzi huo hautavuka bahari, na ukivuka uvushwe na Wazanzibar kwa sharti kuwa Adabu na heshima mbele, kidomo domo mwisho chumbe.

Anasema EU kuna wanachama wenye nchi zenye watu 20,000. Huu kama ndio uzanzibar na usomi wa ZNZ basi kuna tatizo zaidi ya muungano. Hivi huyu juha anajua EU kweli.

Halafu anasema anataka muungano wa haki na usawa, sasa nani anayetakiwa adai haki, yule anayening'inia mgongoni au yule aliyembeba? Halafu Mansour na elimu yake hajiulizi bajeti yake ya miaka 10 ni sawa na kusanyao la mwezi la Tanganyika, usawa utatoka wapi?

Kama alivyo Ahmed na Maalim Seif, Mansour ameshindwa kutaja hayo mambo ya mkataba ni yapi. Ameishia kutueleza kuhusu Hong Kong na Makao, sijui kama huyu Waziri wa Kizanzibar aliwahi kukaa darasani na kusoma historia, jiografia na elimu ya uraia. Huwezi kufananisha chungwa na matembele waziri Mansour! Too low kwa waziri.

Mwisho, Wazanzibar wakae wakielewa kuwa muda wa kuwaendekeza na mdomo juu sasa basi.
Zanzibar inaihitaji Tanganyika kwa namna yoyote ile ndio maana wamepewa panga hakuna anayethubutu kulitumia.
Hakuna anayesimama na kusema vunja muungano, wamebaki kuitisha makongamano ya kudanganyana.

Tanganyika tunasema ZNZ hamna haki ya kuchagua aina ya muungano kwasababu muungano wowote ule ninyi kama ZNZ hamuwezi kuweka kitu cha maana mezani. Kwa bilioni 10 kwa mwezi mna kitu gani. Si afadhali tufanye muungano wa mkataba na Bakhresa!

Muungano mnaoutaka ni kuhemea na hapo ndipo tunajeuri ya kuwaambia bila kificho Tulieni mapakatwe! Mumeshindwa kutamka neno vunja muungano hamna lolote la maana la kusema zaidi ya hadithi. Hadithi mwisho chumbe! ukivuka bahari kama wale 350,000 adabu mbele, heshima kwanza.

LET ZNZ GO!

Kabla jazba zako hazijapanda zaidi jiulize ikowapi tanganyika unayoitetea ww?
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
20,903
2,000
Nurdin moh'd,

..tumewasikia wa-ZNZ mkija na hoja ya muungano wa mkataba.

..sasa na sisi tunawajibu tunataka Tanganyika huru, na Zanzibar huru, zitakazofuatiwa na muungano wa mkataba kupitia EAST AFRICAN COMMUNITY.
 
Last edited by a moderator:

Baraghash

JF-Expert Member
Dec 18, 2012
2,713
2,000
Nurdin moh'd,

..tumewasikia wa-ZNZ mkija na hoja ya muungano wa mkataba.

..sasa na sisi tunawajibu tunataka Tanganyika huru, na Zanzibar huru, zitakazofuatiwa na muungano wa mkataba kupitia EAST AFRICAN COMMUNITY.
Ndugu yangu Nurdin kama watanganyika wataidai nchi yao ( Sijui kutoka kwa nani?) ni jambo safi sana, lakini sio kupitia Jamii forum. Hamasisha kma vile UAMSHO watoe maoni haya kwenye kamati zinzokusanya maoni.
2 Nnanyie hamtosheki tu, mna nchi kubwa tu lakini mate yanakutokeni kuitaka Zanznzibar. Sasa mnaona kijiba cha roho kinakusakameni mnalilia mpaka na Lake Malawi. Ikisha mtakwenda Lake Victoria, baadae Lake Tanganyika. ILi mradi kufakamia ambachi si chenu na bado ndio kwanza nchi tori kwa umasikini duniani. Hebu king'ang'anieni chenu ndio mtake vya wenzenu.

3 Inaoneshapia hji tofauti ya Muungano wa Mkataba n jumuiya za mashirikiano

4. Kutokana na Ufsadi wa Tanganyika Zanzibar imezalisha wakimbizi lakini ni makini si kwa Tanganyika tu lakini wameenea Ulimwengu mzima. Nasema wakimbizi makini kwa vile kote walikosambaa wanamiliki uchumi vizuri, mfano hai ni kama walivyoudhibiti uchumi wa Tanganyika kwenye nyanja zote mkibaki watanganyika kulia wivu tu. Dar inaendelea kujengeka katoka wa wawekezaji mahiri kutoka Zanzibar. Watanganyika waliokimbilia Zanziba kazi yao kujenga makanisa tu na vilabi vya pombe na wenyewe wamwshashituka.
5 Kwa ufupi Zanzibar wanarejea tu usemi wao wa asili toka zama za Rais Aboud Jumbe kuwa hawataki kutawaliwa, Basi, ka lugha ya kISWAHILI SANIFU WANASE WANATAKA MUUNGANO WA MKATABA. Wahafidhina wa ZANZIBAR WANAJUA KUWA lENGO NI KUUZIKA MUUUNGANO
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
20,903
2,000
Baraghash,

..Mh.Ismail Jussa katika maandishi yake alisema kwamba EAC na EU ni mifano ya muungano wa mkataba.

..mapendekezo yangu kwamba tunataka Tanganyika huru na Zanzibar huru itakayofuatiwa na muungano wa mkataba kupitia EAC ni katika kumuunga mkono Mh.Ismail Jussa.

..kuhusu kuhamasishana kuipata Tanganyika huru sisi tuko nyuma kidogo kulinganisha na wenzetu wa Zanzibar. Pamoja na hayo tutaendelea kuhamasishana kupitia njia mbalimbali kama mitandao, magazeti, mpaka kufikia hatua mliyofikia nyinyi. Kumbuka hata nyinyi zanzinet, mzalendo, wamekuwa na mchango mkubwa ktk harakati zenu.

..hata huku Tanganyika muungano umesababisha wakimbizi wa ki-Tanganyika ktk nchi mbalimbali. Wakimbizi hao ni makini na wasomi wakubwa ktk nchi kama Namibia, Botswana, Zimbabwe, Canada, Australia, na kwingineko.

..mwisho, na sisi pia hatutaki kutawaliwa. kuna wa-ZNZ wamepewa madaraka ktk wizara zisizohusiana na muungano. Kodi za wa-Tanganyika ndizo zinazotumika kuendesha serikali ya muungano wakati Zanzibar haichangii chochote. wa-Tanganyika pia wamekuwa wakibebeshwa mzigo wa kulipa madeni ya Zanzibar kwa Tanesco, pamoja na kulipa mishahara ya watumishi wa SMZ. Kwa kifupi tunataka Tanganyika iachwe ipumue.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom