Video: Mgombea wa CCM akiwatoka PCCB wakati akigawa rushwa

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
55,180
85,339
Tangu kura sijui za maoni sijui za nini huko zitangazwe, matukio ya rushwa yalishamiri mno, mchakato huu ulifanywa na Chadema pia ila hatukusikia haya mambo.

Video hii ni mtu anayesikika akitajwa kwa jina la Ngeleja akiwakimbia PCCB wakati wakijaribu kumkamata. Wabunge wa style hii kamwe hawawezi kuleta changamoto zozote Bungeni zaidi ya kupiga makofi, kushangilia, kukejeli na kupitisha miswada mibovu kama ile ya Madini.
 
Attachments

  • VID-20200723-WA0088.mp4
    9.3 MB

Attachments

  • IMG-20200723-WA0076.jpg
    IMG-20200723-WA0076.jpg
    57.3 KB · Views: 1
Infantry Soldier nimeipigia kura Tanzania. Wewe mzalendo mwenzangu unasubiri nini mpaka sasa?????

ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. IPIGIE KURA YA NDIO NCHI YAKO PLEASE PLEASE PLEASE.

Tanzania has been nominated for the 27th World Travel Awards 2020. To WIN in the nominated categories your SUPPORT and VOTE is much NEEDED. The voting ends on 22

August 2020.

To vote use the following link Vote Vote – World Travel Awards then log in or register for new account.

Vote for Tanzania to win the categories of:

(1) Africa's leading airport

(2) Africa's leading tourist attraction

(3) Africa's leading beach destination

(4) Africa's leading destination

(5) Africa's leading national park

(6) Africa's leading tourist board

YOUR VOTE COUNTS!
 
Umasikini tulionao Leo hii Ni matokeo ya rushwa, ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka, vyote hivi vimeasisiwa na kulelewa na fisiem kuanzia Uhuru mpaka Leo hii!

Nikiona mtu kavaa kijani najisikia kutapika!

Aibu! Aibu! Aibu Hawa nguruwe!
"Kuanzia Uhuru?"

Bila shaka yoyote, rushwa ya aina fulani haiwezi kukosekana kabisa katika taifa lolote.

Kinachotazamwa ni dhamira na juhudi zinazofanyika kuizima rushwa hiyo isiwe kubwa kiasi cha kuwaondolea haki raia.

TANU na CCM za mwanzo, rushwa ilikuwepo, lakini kilichofahamika nia kuheshimika ni dhamira ya dhati iliyokuwepo ya kupambana nayo.

Na raia wa kawaida alijua na kuthamini dhamira na juhudi za mapambano hayo.

Siku hizi imebaki kudanganyana tu kwamba kuna kupambana na rushwa huku vitendo vikionyesha tofauti kabisa na maneno yanayosemwa.

Kama kuna vioja kama vinavyofanywa na TAKUKURU, basi inabaki wananchi wenyewe watafsiri wanavyoona wenyewe.
 
Nilikuwepo hapo hiyo siku. Sijui ilikuwaje sikurekodi. Kuna jamaa alipigwa na wananzengo mwanzo kabla ya tukio hili na pesa alizokuwa nazo ziligombaniwa.
 
Mijadala yote hii inayohusu rushwa katika mchakato huu wa kuchuja wagombea inapoteza lengo kwa kuangalia upande mmoja tu wa sarafu na kutotilia mkazo upande wa pili.

Tatizo lipo kwa wajumbe; hao wawakilishi wa chama wanaokwenda kuwachuja watia nia.

Hawa ndio wanaotakiwa kutiwa msukosuko mpaka watapike nyongo.

Hawa ndio viongozi wa chama, kwa hiyo sura nzima ya chama wanaibeba wao.

Kama wanakuwa wapokea rushwa, chama chote ni uozo mtupu.

TAKUKURU wapambane na hawa, waachane kabisa na hao watoa vishawishi.

Hii rushwa inatolewa wakati gani na mahali gani?

Wajumbe wote wanapokuja kupiga kura ni lazima wadhibitiwe pasiwepo na mwanya wa kupokea chochote toka kwa yeyote, na hata ikibidi, wasachiwe kiasi cha pesa walichonacho mifukoni mwao - Nina hakika inawezekana kabisa kuwadhibiti hawa.
 
Nilikuwepo hapo hiyo siku. Sijui ilikuwaje sikurekodi. Kuna jamaa alipigwa na wananzengo mwanzo kabla ya tukio hili na pesa alizokuwa nazo ziligombaniwa.
Huyu Ngeleja no Ngeleja yupi? Aliyekua Waziri?
 
Mijadala yote hii inayohusu rushwa katika mchakato huu wa kuchuja wagombea inapoteza lengo kwa kuangalia upande mmoja tu wa sarafu na kutotilia mkazo upande wa pili.

Tatizo lipo kwa wajumbe; hao wawakilishi wa chama wanaokwenda kuwachuja watia nia.

Hawa ndio wanaotakiwa kutiwa msukosuko mpaka watapike nyongo.

Hawa ndio viongozi wa chama, kwa hiyo sura nzima ya chama wanaibeba wao.

Kama wanakuwa wapokea rushwa, chama chote ni uozo mtupu.

TAKUKURU wapambane na hawa, waachane kabisa na hao watoa vishawishi.
PCCB wenyewe hawana meno
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom